STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 1, 2015

Real Madrid yamtoa nishai David Moyes

Bale (centre) takes Real Sociedad's Yuri Berchiche at Bernabeu stadium in Madrid
Bale akipambana mbele ya vijana wa Real Sociedad
KOCHA wa zamani wa Manchester United, David Moyes anayeinoa kwa sasa Real Sociaded hana hamu na vinara wa La Liga, Real Madrid baada ya kuwashuhudia vijana hao wa Santiago Bernabeu wakiitoa nishai timu yake kwa kuicharaza mabao 4-1 katika pambano la Ligi Kuu ya Hispania usiku wa jana.
Moyes aliyeiongoza Sociaded kuilaza Barcelona bila kutarajiwa hivi karibuni alishuhudia vijana wake wakipotea Bernabeu licha ya kutangulia kufunga la mapema dakika ya kwanza tu tangu kuanza kwa mchezo huo.
Aritz Elustondo aliiandikia wageni bao dakika ya kwanza akimalizia kazi nzuri ya Rubén Pardo kabla ya James 'Bond' Rodríguez kulisawazisha dakika mbili baadaye akimlazia kazi ya Marcelo.
Beki mfungaji wa Real Madrid, Sergio Ramos aliionmgeza timu yake bao la pili dakika ya 37 na kudumu hadi mapumziko wenyeji wakiwa mbele kwa mabaoi 2-1.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema aliwapa furaha mashabiki wa Real Madrid ambao walimkosa nahidha wao, Cristiano Ronaldo anayetumikia adhabu ya kandi nyekundu aliyopata katika mechi hiyo iliyopita kufanya undava uwanjani aliingozea timu hiyo bao la tatu dakika ya 52 akiunganisha krosi ya Gareth Bale.
Benzema alirudi tena kambani dakika ya 76 akifunga bao la nne na kuifanya Real Madrid kuzidi kujikuta kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 20, pointi nne zaidi ya wanaowafukuzia Barcelona wanaocheza leo na Atletico Madrid walioshinda jana ugenini kwa mabao 3-1.
Matokeo mengine ya mechi hiyo, Rayo Vallecano ilikubali kichapo nyumbani cha mabao 2-1 mbele ya wageni wa Deportivo La Coruna, Atletico Madrid wakishinda ugenini mabao 3-1 dhidi ya Eibar, Granada wakishinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Elche na Celta Vigo wakiilaza Cordoba kwa bao 1-0.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezo ifuatayo;
Levante vs  Athletic Bilbao (saa 8 mchana)
Almería vs Getafe (saa 1 usiku)
Sevilla vs Espanyol (saa 3 usiku)
Barcelona vs Villarreal (saa 5 usiku)

Yanga, Ndanda hapatoshi leo Taifa

Yanga
Ndanda FC
KLABU ya soka ya Yanga leo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Ndanda Fc ya Mtwara katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambayo imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro itawakaribisha Ndanda kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam huku wageni hao wa ligi ambao walitoka kuwatoa nishai Kagera Sugar.
Vijana wa Jangwani ambao walikuwa nafasi ya pili katika msimamo kabla ya mechi zilizochezwa jana, wametamba kushinda mchezo huo wakiwa na nia ya kujiweka pazuri kwenye mbio zao za kurejesha taji hilo.
Yanga inayonolewa na kocha Hans van der Pluijm ina pointi 18 baada ya mechi 10 wakati wapinzani wao wakikamata nafasi ya 12 wakiwa na pointi 13 wakianza kuchanganya kasi tofauti na walipoianza ligi hiyo.
Kocha wa Ndanda, Meja Abdul Mingange alinukuliwa kuwa anatarajiwa upinzani mkali toka kwa Yanga, lakini vijana wake wapo tayari kupigana ili kuendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kushinda mechi iliyopita.
Yanga itakayoiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, inakabiliwa na mechi nyingine ngumu katikati ya wiki dhidi ya Coastal Union.
Mechi hiyo ya Yanga na Coastal Union itachezwa siku ya Jumatano  kwenye uwanja wa Mkwakwani, ikiwa ni mechi ya kiporo baina ya timu hizo baada ya mechi ya awali kuahirishwa ili Yanga ishiriki Mapinduzi Cup.
Wanayanga wanahamu ya kutaka kuona timu yao ikipata matokeo mazuri leo na mechi ya Jumatano baada ya awali kuzinguliwa na sare mbili mfululizo dhidi ya Azam na Ruvu Shooting kabla ya kuilaza Polisi.
Pambano jingine litakalochezwa leo katika mfululizo wa ligi hiyo ni lile la Ruvu Shooting watakaoikaribisha Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire ametamba kuwa vijana wao wanaonolewa na kocha Tom Olaba wapo tayari kuvuna pointi tatu baada ya kuwatioa nishai na kuvunja mwiko wa Mtibwa wa kutofungwa katika ligi walipowazabua mabao 2-1 wiki iliyopita ikiwa ni siku chache walipong'ang'ania Yanga na kutoka 0-0.

DR Congo, wenyeji watangulia Nusu Fainali Afrika

Javier Balboa akishangilia moja ya mabao ya wenyeji Guinea ya Ikweta
Referee Rajindraparsad Seechurn is shielded from angry Tunisia players by security personal
Polisi wakimuokoa refa baada ya wachezaji wa Tunisia kuchukizwa na penati waliopewa wenyeji dakika za jioni
Guinea's midfielder Javier Balboa (bottom-R) celebrates with teammates after scoring their second goal
Wenyeji Guinea ya Ikweta wakishangilia ushindi wao dhidi ya Tunisia
Democratic Republic of the Congo's forward Jeremy Bokila (C) celebrates his goal in Bata
DR Congo wakipongezana walipowaduwaza majirani zao Congo-Brazzaville
Mbokani and Sagesse Babele go flying as they compete for the ball in a hotly contested game
Ilikuwa kama Vita baina ya Congo-Brazzaville na DR Congo
TIMU za DR Congo na wenyeji Guinea ya Ikweta zimekuwa timu za kwanza kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kushinda mechi zao za Robo Fainali bila kutarajiwa.
DR Congo walityoka nyuma ya mabao 2-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Congo-Brazzaville katika mchezo uliochezwa mapema kabla ya wenyeji kuwang'oa kwenye muda wa ziada mabingwa wa zamani wa Afrika Tunisia kwa mabao 2-1.
Congo-Brazzaville walianza kuwashtua majirani zao dakika 10 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili pale Ferebory Dore alipofunga bao la kuongoza kabla ya Thievy Bifouma kuongeza la pili dakika ya 62 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa DR Congo.
Hata hivyo DR Congo hawakukata tamaa baada ya kufungwa mabao hayo mawili na badala ake kucharuka na kurejesha bao moja baada ya jingine kupitia wachezaji wake nyota, Dieumerci Mbokani aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 65 na 90, Jeremy Bokila dakika ya 75, na   Joel KImwaki aliyefunga bao la tatu dakika ya 81 na kuivusha timu yao nusu fainali tangu 1988.
Katika meechi ya pili iliyochezwa pia kwenye uwanja huo wa Bata usiku wenyeji waliwaduwaza Tunisia kwa kuwalaza mabao 2-1 wakichomoa bao dakika ya jioni na kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1 kabla ya kufunga bao la ushindi kwenye muda wa nyongeza wa dakika 30.
Tunisia walianza kuandika bao lililokuwa likionekana kama limewavusha hatua ya nusu fainali kupitia kwa Ahmed Akaichi katika dakika ya 70, lakini Guinea ya Ikweta ilichomo dakika za ziada za pambano hilo kabla ya halijamalizika kupitia kwa Javier Balboa aliyefunga kwa penati, iliyozua zogo kwa wachezaji wa Tunisia kumlalamikia mwamuzi kiasi cha Polisi kuamua kuingilia kati kumuokoa mwamuzi huyo.
Dakika ya 102 Balboa tena aliwatoa kimasomaso wenyeji wa kufunga bao la pili ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuifanya Guinea ya Ikweta kufuzu kwa mara ya kwanza hatua hiyo na sasa wanasubiri mshindi kati ya Ghana na Guinea wanaocheza leo kwenye robo fainali nyingine wa michuano hiyo.
DR Congo wenyewe watasubiri kujua watacheza nani hatua ya nusu fainali kati ya Ivory Coast na Algeria ambazo zitakamilisha mechi za robo fainali usiku wa leo kwenye uwanja wa Malabo.