STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 1, 2015

Yanga, Ndanda hapatoshi leo Taifa

Yanga
Ndanda FC
KLABU ya soka ya Yanga leo watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Ndanda Fc ya Mtwara katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambayo imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Moro itawakaribisha Ndanda kwenye dimba la Taifa, jijini Dar es Salaam huku wageni hao wa ligi ambao walitoka kuwatoa nishai Kagera Sugar.
Vijana wa Jangwani ambao walikuwa nafasi ya pili katika msimamo kabla ya mechi zilizochezwa jana, wametamba kushinda mchezo huo wakiwa na nia ya kujiweka pazuri kwenye mbio zao za kurejesha taji hilo.
Yanga inayonolewa na kocha Hans van der Pluijm ina pointi 18 baada ya mechi 10 wakati wapinzani wao wakikamata nafasi ya 12 wakiwa na pointi 13 wakianza kuchanganya kasi tofauti na walipoianza ligi hiyo.
Kocha wa Ndanda, Meja Abdul Mingange alinukuliwa kuwa anatarajiwa upinzani mkali toka kwa Yanga, lakini vijana wake wapo tayari kupigana ili kuendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kushinda mechi iliyopita.
Yanga itakayoiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, inakabiliwa na mechi nyingine ngumu katikati ya wiki dhidi ya Coastal Union.
Mechi hiyo ya Yanga na Coastal Union itachezwa siku ya Jumatano  kwenye uwanja wa Mkwakwani, ikiwa ni mechi ya kiporo baina ya timu hizo baada ya mechi ya awali kuahirishwa ili Yanga ishiriki Mapinduzi Cup.
Wanayanga wanahamu ya kutaka kuona timu yao ikipata matokeo mazuri leo na mechi ya Jumatano baada ya awali kuzinguliwa na sare mbili mfululizo dhidi ya Azam na Ruvu Shooting kabla ya kuilaza Polisi.
Pambano jingine litakalochezwa leo katika mfululizo wa ligi hiyo ni lile la Ruvu Shooting watakaoikaribisha Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani.
Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire ametamba kuwa vijana wao wanaonolewa na kocha Tom Olaba wapo tayari kuvuna pointi tatu baada ya kuwatioa nishai na kuvunja mwiko wa Mtibwa wa kutofungwa katika ligi walipowazabua mabao 2-1 wiki iliyopita ikiwa ni siku chache walipong'ang'ania Yanga na kutoka 0-0.

No comments:

Post a Comment