STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, September 10, 2014

Hii ni ajali nyingine iliyotokea asubuhi ya leo Lindi na kuua wawili

2fru
Ni taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga na kweli imehusisha kifaru cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) saa kumi na moja alfajiri ambapo kifaru kimoja chenye tairi kwenye msafara wa jeshi hilo kimeripotiwa kuacha njia na kugonga nyumba.
Shuhuda alieongea na Power Breakfast ya CloudsFM amesema ‘Imetokea Mnolela kijijini Lindi kwenye msafara huu wa jeshi ilitangulia Iveco moja na nyuma vifaru viwili na walipofika kwenye eneo la shule kuna kona mbaya sana ambayo mara nyingi magari huwa yanaanguka’
‘Kifaru kimoja kwenye huo msafara kilikosa njia na kuingia bondeni kikagonga nyumba ya kwanza kikamkanyaga mwenye nyumba kikagonga nyumba ya pili kikazama kwenye hiyo sebule, kwa harakaharaka waliofariki ni watatu, Wanajeshi watatu na mwenye nyumba ya kwanza na wengine ni majeruhi wa hali mbaya kabisa’
1fru
‘Msafara ulikua unatokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye kambi kuu, hii kona ni kali na aliejenga hii barabara amebakiza baadhi ya changarawe hakufagia kwahiyo mtu akikaribia changarawe zile mtu zinamvuta, hiki kifaru chenye tairi kilikua kwenye spidi kubwa sana usio wa kawaida ikamshinda ndio akatumbukia bondeni’ – Shuhuda
‘Mmoja wa waliofariki ni mama mwenye nyumba ya kwanza ambae alikua amelala kwenye chumba cha mbele ndio alikanyagwa na kufariki papohapo, walioumia ni Wanajeshi waliokua wamekaa juu ya kifaru hicho, wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara’ – Shuhuda
Kamanda Mpinga amethibitisha kutokea kwa hili tukio, unaweza kubonyeza play hapa chini kumsikiliza shuhuda mwenyewe na kamanda Mpinga.
Kwa msaada wa Millardayo.com

Bondia Djamel Dahou atua kuzipiga Moshi na Yazidu

http://mfs0.cdnsw.com/fs/Root/8ak85-IMG_0187.JPG
Bondia Djamel Dahou atakayepigana na Said Yazidu siku ya Ijumaa
BONDIA Djamel Dahou kutoka Algeria ametua nchini alfajiri ya jana tayari kwa ajili ya pambano lake la kuwania ubingwa wa Dunia dhidi ya Said Yazidu wa Tanzania litakalofanyika kesho mjini Moshi, Kilimanjaro.
Pambano hilo la raundi 12 litafanyika kwenye ukumbi wa YMCA na kusindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la kuwania ubingwa wa UBO Afrika.
Pigano hilo jingin la ubingwa wa UBO litakuwa kati ya Mtanzania Ali Ramadhan 'Alibaba' dhidi ya Mmalawi, Alick  Mwenda.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST, litakalosimamia pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Green Hill Promotion, Anthony Rutta alisema Dahou alitua alfajiri ya jana kwa Ndege ya Egypt Airways.
"Mpinzani wa Said Yazidu, Djamel Dahou ameshatua na anaelekea Kilimanjaro kwa ajili ya pambano lao la Septemba 12 kwenye ukumbi wa YMCA," alisema.
Rutta alisema pambano hilo litatanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la UBO Afrika la raundi 10 kati ya Alibaba na Mwenda wa Malawi.
Mengine ni kati ya Fatuma Yazidu dhidi ya Joyce Adam, Emmanuel Alex dhidi ya Ali Bugingo huku Pascal Bruno atazipiga na Cosmas Kibuga, George Allen atazipiga na Ssebo Husseni na Raymond Bwango dhidi ya Fadhil Mkinda.

Uholanzi yamtisha Sepp Blatter

http://vid.alarabiya.net/images/2014/07/27/837d0b74-5c15-435a-bd94-cc9250711bb9/837d0b74-5c15-435a-bd94-cc9250711bb9_16x9_600x338.jpgCHAMA cha Soka cha Uholanzi-KNVB kimedai kutompigia kura Sepp Blatter ambaye amethibitisha kugombea tena urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kipindi cha tano. 
Rais wa KNVB Michael van Praag aliwaambia waandishi wa habari kuhusu msimamo wao huo jana lakini akakiri kuwa haoni kama kuna mtu anayeweza kumng’oa Blatter katika nafasi hiyo. 
Uholanzi mara kadhaa wamekuwa wakimpinga Blatter mwenye umri wa miaka 78 ambaye alichukua madaraka hayo kutoka kwa Joao Havelange mwaka 1998. 
Katika mkutano mkuu wa FIFA uliofanyika nchini Brazil kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia, KNVB ilimpasha Blatter kuwa anatakiwa astaafu huku wakimtaka kuwajibika kutoka kashfa mbalimbali zilizolikumba shirikisho hilo. 
Lakini Blatter anaonekana bado kutaka kuendelea kukomalia nafasi hiyo kwa kipindi kingine kitakachomaliza mwaka 2019 akiwa na umri wa zaidi ya miaka 83, baada ya rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini kuweka wazi kuwa hatagombea kiti hicho. 
Praag amesema bahati mbaya Platini amekataa kugombea kwani ndiye mtu pekee ambaye angeweza kusimama na Blatter.

Ramsey aiweka roho juu Arsenal

Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf

Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ballMASHABIKI wa klabu ya Arsenal wapo roho juu baada ya kiungo wao mahiri, Aaron Ramsey kuumia kifundo cha mguu na kuwa hatarisni kulikosa pambano la mwishoni mwa wiki dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu ya England.
Kiungo huyo alipata  majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa Wales wa mabao 2-1 dhidi ya Andorra jana usiku baada ya kufanyiwa rafu na mchezaji wa Andorra ambapo alipatiwa matibabu, lakini akatolewa uwanjani.
Meneja wa timu, Chris Coleman alisema ukubwa wa  majeruhi utatangazwa saa 24 kuanzia jana usiku, na hali hiyo imempa maumivu ya kichwa, kocha Arsene Wenger
Chris Coleman alisema anaamini majeruhi ya Ramsey haiwezi kumuweka nje ya uwanja wa muda mrefu.

Kuziona Yanga, Azam buku 5 tu

KIINGILIO cha chini kwenye mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.

Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho cha sh. 5,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani na bluu vitakavyochukua jumla ya watazamaji 36,000 katika uwanja huo wenye viti 57,558.

Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.

MWAMUZI LUGENGE KUAGWA LEO
Mwamuzi wa daraja la kwanza (class one), Luteni Godwill David Lugenge aliyefariki dunia juzi (Septemba 7 mwaka huu) kwa ajali ya gari katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga anaagwa leo (Septemba 9 mwaka huu).

Mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo, baadaye leo saa 6 mchana utapelekwa nyumbani kwa kaka yake Kimara Bucha jijini Dar es Salaam ambapo shughuli za kuaga zitafanyika kabla ya safari ya kwenda mkoani Njombe kwa ajili ya mazishi.

Luteni Lugenge ambaye mwishoni mwa wiki alishiriki mitihani ya utimamu wa mwili kwa waamuzi wa Ligi Kuu, akiwa na ndugu yake Christopher Alexander Lunyungu katika gari dogo walipata ajali hiyo wakati wakienda mkoani Kilimanjaro.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambalo limetoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kwenye shughuli ya kuaga itawakilishwa na mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Saloum Umande Chama.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Luteni Lugenge, Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu nchini (FRAT) na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe

Yaillah Toba! Ajali nyingine tena yachukua roho za watu

JANGA la ajali za barabarani zimeendelea kupukutisha roho za watanzania baada ya basi la Super Feo lililokuwa linatokea Songea kwenda Mbeya kupata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.
Ajali hiyo imetokea leo eneo la Sinangula wakati likimkwepa mwendesha baiskeli na kwenda kuvamia mti na kupinduka na taarifa za awali zinasema watu zaidi ya 34 wamejeruhiwa na wawili kufa jambo taarifa za sasa zinadai ni abiria watatu wamepoteza maisha.
Ajali hiyo ni mfululizo wa matukio yaliyoteketeza roho za watanzania huku tukielekea WIKI YA USALAMA BARABARANI inayotarajiwa kuadhimishwa mjini Arusha.
Tufunge na kuomba Mungu atuepushilie janga hili ambalo ni janga la kitaifa na linaloua pengine kuliko hata maradhi tishio nchini kwa sasa.
MICHARAZO inatoa pole kwa wote waliopoteza ndugu, jamaa na rafiki zao kwenye ajali zote zilizotokea ndani ya mwezi huu wa Septemba na mingine ya nyuma na kuwaombea kila la heri walioachwa na majeraha kupona haraka kwa uwezo wa AlLAH SW. Inshallah

Vijana CUF wahimiza kuchangamkia uchaguzi mkuu

http://3.bp.blogspot.com/-Vg1FlLMzmC8/UGVoED0VOGI/AAAAAAAByBI/GI-uXRyYJ-s/s320/tz%7Dcuf.gif 
Na Suleiman Msuya 'Kipimo'
JUMUIYA ya Vijana ya Chama Cha Wananchi (JUVICUF) imewataka vijana wa chama hicho kujitokeza kugombea katika chaguzi za vijana pamoja na ule wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini kote.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa (JUVICUF) Hamidu Bobali wakati akizungumza na mwandishi wa habari katika ofisi za chama cha CUF jijini Dar es Salaam.
Alisema chama kupitia (JUVICUF) kinatarajia kufanya chaguzi kuanzia matawi, kata, wilaya na Taifa ambapo wilaya 45 za Tanzania Bara na 10 za Zanzibar zitashiriki ili kupatikana kwa viongozi.
Bobali alisema mikakati (JUVICUF) ni kuhakikisha kuwa chama kinajijenga vizuri kuanzia ngazi za chini hasa ukizingatia kuwa ni wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwahimiza vijana wa CUF kujitokeza katika chaguzi zote za chama katika ngazi ya vijana ambazo zimeanza kufanyika sasa na mwezi ujao Novemba ili mwezi Desemba tuweze kufanya uchaguzi mkuu wa vijana Taifa”, alisema.
Bobali alisema uchaguzi huo wa Taifa unatarajiwa kuhusisha zaidi ya vijana 135 kutoka Bara na 120 kutoka Zanzibar ambao watotokana na chaguzi katika ngazi za Wilaya.
Alisema mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na wawakilishi kutoka Wilaya zote za Tanzania Bara kama ilivyo Zanzibar ambayo italeta ushindani wa kisiasa hapa nchini.
Naibu Katibu huyo alisema pia JUVICUF inajipanga kufanya operasheni mbalimbali ambazo zitakuwa na lengo la kuhamasisha vijana kujitokeza katika chaguzi na ufahamu juu ya lengo la Wabunge wanaounga mkono Rasimu ya Jaji Warioba kutoka nje ya Bunge.
Alisema kuna hali ya sintofahamu kwa baadhi ya vijana na wananchi mbalimbali ya nini sababu ya wajumbe wa UKAWA kutoka nje ya Bunge hivyo JUVICUF inaona ni wakati muafaka wa kutoa elimu.
Bobali alisema ni vema vijana wa vyama vinavyounga mkono UKAWA kuendelea kuwa na umoja ili kuhakikisha kuwa juhudi za viongozi wao wa Kitaifa zinafikiwa ili waweze kukomboa Taifa.