Ajali hiyo imetokea leo eneo la Sinangula wakati likimkwepa mwendesha baiskeli na kwenda kuvamia mti na kupinduka na taarifa za awali zinasema watu zaidi ya 34 wamejeruhiwa na wawili kufa jambo taarifa za sasa zinadai ni abiria watatu wamepoteza maisha.
Ajali hiyo ni mfululizo wa matukio yaliyoteketeza roho za watanzania huku tukielekea WIKI YA USALAMA BARABARANI inayotarajiwa kuadhimishwa mjini Arusha.
Tufunge na kuomba Mungu atuepushilie janga hili ambalo ni janga la kitaifa na linaloua pengine kuliko hata maradhi tishio nchini kwa sasa.
MICHARAZO inatoa pole kwa wote waliopoteza ndugu, jamaa na rafiki zao kwenye ajali zote zilizotokea ndani ya mwezi huu wa Septemba na mingine ya nyuma na kuwaombea kila la heri walioachwa na majeraha kupona haraka kwa uwezo wa AlLAH SW. Inshallah
No comments:
Post a Comment