Bondia Djamel Dahou atakayepigana na Said Yazidu siku ya Ijumaa |
Pambano hilo la raundi 12 litafanyika kwenye ukumbi wa YMCA na kusindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la kuwania ubingwa wa UBO Afrika.
Pigano hilo jingin la ubingwa wa UBO litakuwa kati ya Mtanzania Ali Ramadhan 'Alibaba' dhidi ya Mmalawi, Alick Mwenda.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST, litakalosimamia pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Green Hill Promotion, Anthony Rutta alisema Dahou alitua alfajiri ya jana kwa Ndege ya Egypt Airways.
"Mpinzani wa Said Yazidu, Djamel Dahou ameshatua na anaelekea Kilimanjaro kwa ajili ya pambano lao la Septemba 12 kwenye ukumbi wa YMCA," alisema.
Rutta alisema pambano hilo litatanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la UBO Afrika la raundi 10 kati ya Alibaba na Mwenda wa Malawi.
Mengine ni kati ya Fatuma Yazidu dhidi ya Joyce Adam, Emmanuel Alex dhidi ya Ali Bugingo huku Pascal Bruno atazipiga na Cosmas Kibuga, George Allen atazipiga na Ssebo Husseni na Raymond Bwango dhidi ya Fadhil Mkinda.
No comments:
Post a Comment