Na Suleiman Msuya 'Kipimo'
JUMUIYA
ya Vijana ya Chama Cha Wananchi (JUVICUF) imewataka vijana wa chama hicho
kujitokeza kugombea katika chaguzi za vijana pamoja na ule wa Serikali za Mitaa
unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini kote.
Rai
hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa (JUVICUF) Hamidu Bobali wakati
akizungumza na mwandishi wa habari katika ofisi za chama cha CUF jijini Dar es
Salaam.
Alisema
chama kupitia (JUVICUF) kinatarajia kufanya chaguzi kuanzia matawi, kata,
wilaya na Taifa ambapo wilaya 45 za Tanzania Bara na 10 za Zanzibar zitashiriki
ili kupatikana kwa viongozi.
Bobali
alisema mikakati (JUVICUF) ni kuhakikisha kuwa chama kinajijenga vizuri kuanzia
ngazi za chini hasa ukizingatia kuwa ni wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa
na uchaguzi mkuu.
“Napenda
kutumia nafasi hii kuwahimiza vijana wa CUF kujitokeza katika chaguzi zote za
chama katika ngazi ya vijana ambazo zimeanza kufanyika sasa na mwezi ujao
Novemba ili mwezi Desemba tuweze kufanya uchaguzi mkuu wa vijana Taifa”, alisema.
Bobali
alisema uchaguzi huo wa Taifa unatarajiwa kuhusisha zaidi ya vijana 135 kutoka
Bara na 120 kutoka Zanzibar ambao watotokana na chaguzi katika ngazi za Wilaya.
Alisema
mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na wawakilishi kutoka Wilaya zote za
Tanzania Bara kama ilivyo Zanzibar ambayo italeta ushindani wa kisiasa hapa
nchini.
Naibu
Katibu huyo alisema pia JUVICUF inajipanga kufanya operasheni mbalimbali ambazo
zitakuwa na lengo la kuhamasisha vijana kujitokeza katika chaguzi na ufahamu
juu ya lengo la Wabunge wanaounga mkono Rasimu ya Jaji Warioba kutoka nje ya
Bunge.
Alisema
kuna hali ya sintofahamu kwa baadhi ya vijana na wananchi mbalimbali ya nini
sababu ya wajumbe wa UKAWA kutoka nje ya Bunge hivyo JUVICUF inaona ni wakati
muafaka wa kutoa elimu.
Bobali
alisema ni vema vijana wa vyama vinavyounga mkono UKAWA kuendelea kuwa na umoja
ili kuhakikisha kuwa juhudi za viongozi wao wa Kitaifa zinafikiwa ili waweze
kukomboa Taifa.
No comments:
Post a Comment