Rais wa KNVB Michael van Praag
aliwaambia waandishi wa habari kuhusu msimamo wao huo jana lakini
akakiri kuwa haoni kama kuna mtu anayeweza kumng’oa Blatter katika
nafasi hiyo.
Uholanzi mara kadhaa wamekuwa wakimpinga Blatter mwenye
umri wa miaka 78 ambaye alichukua madaraka hayo kutoka kwa Joao
Havelange mwaka 1998.
Katika mkutano mkuu wa FIFA uliofanyika nchini
Brazil kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia, KNVB ilimpasha
Blatter kuwa anatakiwa astaafu huku wakimtaka kuwajibika kutoka kashfa
mbalimbali zilizolikumba shirikisho hilo.
Lakini Blatter anaonekana bado
kutaka kuendelea kukomalia nafasi hiyo kwa kipindi kingine
kitakachomaliza mwaka 2019 akiwa na umri wa zaidi ya miaka 83, baada ya
rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini kuweka wazi
kuwa hatagombea kiti hicho.
Praag amesema bahati mbaya Platini amekataa
kugombea kwani ndiye mtu pekee ambaye angeweza kusimama na Blatter.
No comments:
Post a Comment