STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 26, 2014

Mashetani Wekundu wamgeukia beki wa Southampton

Luke Shaw anayenyatiwa na Manchester United

BAADA ya kukamilisha uhamisho wa Pauni milioni 37 wa kiungo Juan Mata kutoka Chelsea, klabu ya Manchester United inajiandaa kupeleka ofa ya Pauni milioni 23 kwa klabu ya Southampton ili kumsajili beki wa kushoto wa klabu hiyo, Luke Shaw.
United inajaribu 'kuipiga bao' Chelsea ambayo pia inamuania beki huyo mwenye miaka 18 kwa kupeleka ofa hiyo kesho Jumatatu.
Usajili wa Mata umeweka rekodi ya uhamisho wa klabu hiyo ya Pauni milioni 30.7 iliyokuwa ikishikiliwa na Dimitar Babatov waliyoiweka wakati wakimsajili mchezaji huyo kutoka Tottenham mwaka 2008, lakini Kocha wa United David Moyes, amepania kukiimarisha kikosi chake katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili kinachomalizika Januari 31.
Mbali na kijiandaa kupeleka ofa hiyo, Moyes juzi usiku alikuwepo uwanjani kwenye mchezo kati ya Borussia Monchengladbach na Bayern Munich akiwafuatilia mshambuliaji wa Bayern, Mario Mandzukic na kiungo wa Monchengladbach, Patrick Herrmann.
Moyes anaaha kutaka kukiimarisha kikosi chake ambacho 'kinayumba' kwenye ligi kuu.
United ipo nyuma kwa tofauti ya pointi 14 na vira wa ligi, Arsenal na hivyo kuondoa uwezekano wa kutetea ubingwa msimu huu.
Matumaini pekee ya United msimu huu yapo kwenye ligi ya mabingwa Ulaya lakini kuyumba kwa timu hiyo kwenye ligi na kikosi kisichokuwa na makali kunatilia shaka kufanya vizuri kwenye ligi hiyo yenye ushindani