STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, January 26, 2014

Zimbabwe yatinga nusu fainali CHAN, yailaza Mali 2-1

 
WALIOKUWA vinara wa kundi A katika michuano inayoendelea nchini Afrika Kusini, Mali usiku wa kuamkia leo imekijikuta kikifungashwa virago katika hatua ya robo fainali kwa kulazwa mabao 2-1 bila kutarajiwa na Zimbabwe.
Zimbambwe ambayo haikupewa nafasi kubwa ya kutamba kwenye michuano hiyo kulinganisha na timu za Afrika Magharibi na Kaskazini, ilipata ushindi huo wa kushtukiza katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Cape Town.
Bao la mapema kwenye dakika 11 lililofungwa na Sithole na jingine la kipindi cha pili la Mahachi katika dakika ya 56 yalitosha kuivuisha timu hiyo pekee kwenye ukanda wa Kusini hadi nusu fainali ya michuano hiyo akisubiri sasa mshindi wa mechi ya leo kati ya Gabon na Libya.
Mali iliyokuwa haijaonja kipigo katika michuano hiyo ilipata bao lake la kufutia machozi katika dakika ya 89 kupitia kwa Sinoyoko na kuwaacha wazimbabwe wakienda nusu fainali kilaini wakiungana na Nigeria iliyotangulia mapema jana kwa kuiduwaza Morocco iliyooongoza mabao matatu kipindi cha kwanza kwa kuilaza mabao 4-3 mchezo ulioenda hadi muda wa nyongeza baada ya Super Eagles kurejesha mabao matatu katika dakika 90 kabla ya kufunga na ushindi zikiwa zimesalia dakika 9 kumalizika kwa mchezo huo.
Robo fainali za mwisho zinatarajiwa kuchezwa leo kuanzia jioni amba[po Gabon itapepetana na Libya kabla ya Ghana kumalizana na DR Congo usiku ambapo timu mojawapo kati ya hizo itakwenda kucheza na NIgeria kwenye nusu fainali ya pili zitakazochezwa siku ya Jumatano.

No comments:

Post a Comment