STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, February 20, 2013

AZAM YAZIDI KUISOGELEA YANGA, SIMBA YAZINDUKA MBEYA

Azam

 
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam jioni ya leo imeendelea kuibana Yanga kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuisambaratisha JKT Ruvu kwa mabao 4-0, huku Simba wakizindukia Mbeya.
Wakati Azam ikipata ushindi huo mnono kwenye uwanja wa Chamazi jijini Dar na kufanya ifikishe pointi 36 sawa na Yanga na kutofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, Simba ilishinda kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya wenyeji wao Prisons kwa bao pekee la Amri Kiemba.
Ushindi huo wa Azam umeifanya kushinda mechi ya nne nne mfululizo katika ligi na kufikisha jumla ya mabao 14 ikiwa ni rekodi katika msimu ya hivi karubuni kwa ligi hiyo.
Mabao mawili ya Mcha Khamis 'Vialli' na John Bocco 'Adebayor' yaliifanya Azam kwenye mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 kabla ya kuongeza mengine mawili katika kipindi cha pili kupitia Vialli naAbdi Kassim 'Baby', huku JKT ikipoteza penati iliyopanguliwa na kipa Ally Mwadini, aliyekuwa ameisababisha.
Azam sasa inasubiriwa kuona kama itaing'oa Yanga kileleni siku ya Jumamosi watakapokutana wenyewe kwa wenyewe kwenye uwnaja wa Taifa, japo Yanga wapo nyuma kwa mechi moja na wanaongoza msimamo wa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, baada ya kupokea kipigo kwa Kagera Sugar katika mechi yao iliyopita Coastal Union leo ilizinduka kwa kuilaza JKT Oljoro mabao 2-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga kwa mabao ya Suleiman Kassim 'Salembe' na Mkenya Jerry Santo, huku Toto Africans wakiwa nyumbani kwao CCm Kirumba walikumbana na kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Africans Lyon.
Ushindi huo umeitoa Lyon mkiani na kuirejeshea nafasi hiyo Polisi Moro waliokuwa 'wameizoea' tangu duru lililopita kabla ya kuzinduka hivi karibuni.