| Mashabiki wa Simba wanaosubiri kuipa sapoti timu yao Jumapili jioni dhidi ya Mtibwa Sugar |
Kulikuwa na dalili za Simba kuvaana na Yanga kama matokeo yangeisha kwa sare ya 0-0, lakini bao la Mkude liliweka mambo sawa na sasa vijana wa Msimbazi watakuwa wakinoa makucha yao ili kuvaana na Mtibwa waliocheza nao fainali za mwaka jana na kuichapa kwa mikwaju ya penalti.
Yanga wenyewe itakuwa na kibarua dhidi ya URA ambayo mapema jioni ya leo ilipata ushindi wa baoa 1-0 dhidi ya Jamhuri.
Kama Yanga na Simba zitavuka hatua hiyo zitaumana Jumatano usiku kwenye fainali ikirejea fainali za mwaka 2011, ambazo Simba ilitwaa taji lake la pili kwa kuizabua Yanga mabao 2-0.

IKIWA na kibarua kigumu wikiendi hii dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Sunderland imetangaza kumsajili beki wa Bayern Munich, Jan Kirchhoff kwa ada ambayo haikuwekwa wazi.
KLABU ya Borussia Dortmund imedai ulikuwa ni uamuzi wa Adnan Januzaj mwenyewe kurejea Manchester United na kukiri dili lake halikuwa na manufaa kwa klabu yoyote. 

KLABU ya Yanga inasubiri kujua itacheza na nani kati yake na watani zao Simba au URA ya Uganda katika mechi za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
HONGERA. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani.
