STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 8, 2016

Sunderland wanasa kifaa toka Bayern Munich

https://i.guim.co.uk/img/media/714c8f8cc7ab15b56bb5fb6c9eb01c24b719ae6c/0_149_5128_3080/master/5128.jpg?w=620&q=85&auto=format&sharp=10&s=daec3160be3fec2cb53a6ae0d3112b65IKIWA na kibarua kigumu wikiendi hii dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Sunderland imetangaza kumsajili beki wa Bayern Munich, Jan Kirchhoff kwa ada ambayo haikuwekwa wazi.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25, alianza soka lake katika timu ya Mainz kabla ya kujiunga na Bayern mwaka 2013, akiwa pia amecheza kwa mkopo Schalke ametua kwa Paka Weusi hao kabla ya kuvaana na Arsenal kwenye mechi ya mzunguko wa tatu wa michuano ya Kombe la FA.
Meneja wa Sunderland, Sam Allardyce aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa Jan ni mchezaji mzuri na mwenye uzoefu pamoja na umri mdogo alionao hivi sasa. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anaamini beki huyo atazoea haraka mazingira katika klabu hiyo na kuwasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea msimu huu.
Sunderland iko katika mapambano ya kutoshuka daraja wakishika nafasi ya 19 katika msimamo wakiwa na alama 15 katika michezo 20 waliyocheza.

No comments:

Post a Comment