STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 30, 2014

Mwanasoka Bora Afrika kujulikana Januari 8 nchini Nigeria

http://www.football-marketing.com/wp-content/uploads/2012/01/PUMA-Yaya-Toure.jpg
Yaya Toure
SHIRIKISHO la Soka Afrika, CAF linatarajia kutoa tuzo kwa Wachezaji Bora kwa mwaka huu Januari 8 mjini Lagos Nigeria.
Kiungo wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, golikipa Vincent Enyeama wa Nigeria na kiungo Yaya Toure mmojawao ndiye atakayetwaa tuzo ya mwaka ya Mwanasoka Bora wa Afrika.

Mbali na hao pia wachezaji wengine watatu watachuana kwenye tuzo ya Mwanasoka Bora kwa wachezaji wa ndani ya Afrika
Wachezaji wanaowania tuzo hiyo ambayo ilikuwa ikishirikiliwa na Mohammed Aboutrika wa Misri ni;
Akram Djahnit (Algeria) El Hedi Belamieri( Algeria)Firmin Mubele Ndombe (DR Congo)
Kwa upande wa wanasoka wawanawake wanaowania tuzo hizo ni;
Annette Ngo Ndom (Cameroon) Asisat Oshoala (Nigeria) Desire Oparanozie (Nigeria)
Upande wa wanasoka chipukizi tuzo hiyo inawaniwa na Asisat Oshoala (Nigeria) Fabrice Ondoa (Cameroon),Uchechi Sunday (Nigeria)
Wanaowania tuzo ya kipaji kinachochipukia ni
Clinton N’jie (Cameroon) Vincent Aboubakar (Cameroon) Yacine Brahimi (Algeria)
Makocha wanaowania tuzo hizo za CAF ni;

Florent Ibenge (DR Congo) Kheireddine Madoui (ES Setif) Vahid Halilhodžić (kocha wa zamani wa Algeria)
Timu Bora ya Mwaka tuzo yake inawaniwa na; Algeria, Libya, Nigeria
Timu Bora ya Wanawake ya Mwaka ni;
Cameroon, Nigeria, Nigeria U-20
Klabu bora ya Mwaka
Al Ahly (Egypt) AS Vita (DR Congo) ES Setif (Algeria)
Huku Rais wa Tp Mazembe Moise Katumbi Chapwe akitarajiwa kupewa tuzo ya kiongozi bora wa michezo wa mwaka.

Real Madrid yasisitiza Gareth Bale HAUZWI kokote!

Bale celebrates winning the FIFA Club World Cup earlier in December 
Gareth Bale
RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amesisitiza kuwa Gareth Bale hauzwi na kuzitaja taarifa kwamba amepokea ofa kutoka Manchester United ni upuuzi mtupu.
Bale, aliyejiunga na Real Madrid akitokea Tottenham kwa dau lililovunja rekodi ya uhamisho duniani ya karibu Pauni Mil. 85 Septemba 2013 amekuwa akidaiwa kuwa yu mbioni kurejea tena Ligi Kuu ya England.
United imedaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 120 ili kumnyakua nyota huyo wa kimataifa wa Wales, lakini Perez amepuuza taarifa hizo na kudai Bale, 25 hawezi kuondoka Santiago Bernabeu.
Perez aliliambia gazeti la michezo la Marca: "Hatujapokea ofa yoyote kuhusu Gareth Bale, siyo klabu ya Manchester United wala klabu nyingine yoyote.,"
"Kadhalika hatutakuwa tayari kusikilizia ofa yoyote juu ya Bale kwani ni mchezaji muhimu mno kwetu," alisema Perez.
Bale amekuwa na wakati mzuri tangu ajiunge na kigogo hicho cha Hispania akiunda safu kali ya ushambuliaji akishirikiana na  Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
Nyota huyo wa zamani wa Southampton aliisaidia Real Madrid kunyakua taji la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafumua wapinzani wao wa Madrid, Atletico Madrid kwa mabao 4-1 katika fainali iliyozikutanisha timu hasimu za jiji moja.

Crsitiano Ronaldo kidume 2014, atwaa tuzo nyingine


MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemaliza mwaka kwa staili ya aina yake kwa kubeba tuzo nyingine ya mchezaji bora wa mwaka au Globe Soccer Awards huko Dubai.
Mreno huyo amekuwa na mwaka mzuri huku akivunja rekodi kwa kuwa na mabao mengi katika msimu mmoja wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati alipoiongoza Real Madrid kunyakuwa taji lake la 10 la michuano hiyo.
Ronaldo pia anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa mara ya pili mfululizo Januari 12 mwakani licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Lionel Messi na Manuel Neuer alioingia nao kwenye 3 Bora ya tuzo hiyo.
Mchezaji huyo ambaye alikuwepo mwenyewe kupokea tuzo hiyo katika sherehe zilizofanyika katika Hotel ya Atlantis Palm aliwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake na viongozi wa Real Madrid kwa ushirikiano wanaompa na kufanya kupata mafanikio hayo.
Aidhsa kocha wa Madrid Carlo Ancelotti naye alitunukiwa tuzo hiyo kama kocha wa bora wa mwaka kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo kwa mwaka huu

BABY MADAHA ANAKUJA NA SAINT & GHOST

http://api.ning.com/files/KtF8hZpsH-3lMXDW7ufVoIr4iNPkkwwMRNxku*jb0MDMU7Iz*sLL7Hfl9BdoYxrd9FpJEMbPW8DsGjHTHEQX05k1rl-IZhsZ/babymadaha.jpg
Baby Madaha
BAADA ya kutuymia muda mrefu akiwa amejichimbia Kenya kufanya shughuli zake za muziki, mwanadada Baby Madaha anajiandaa kuvunja ukimya kwenye soko la filamu kwa kuibuka na 'Saint & Ghost'  ambayo imesheheni nyota mbalimbali wa filamu nchini.
Akizungumza na MICHARAZO mapema leo, Baby Madaha alisema filamu hiyo inayotengenezwa kupitia kampuni yake, iitwayo Darkangel Film Production and Entertainment imewashirikisha wakali kama Kulwa Kikumba 'Dude', yeye (Baby Madaha), Hidaya Njaidi,  Grace Mapunda 'Mama Kawele', Ramadhani Ally 'Tafu', Ahmed Olotu 'Mzee Chillo' na wengine.
"Nimbo chimbo kwa sasa natengeneza filamu yangu iitwayo 'Saint and Ghost' ambayo naitengeneza kupitia kampuni yangu na inawashirikisha wasanii mbalimbali nyota nikiwamo mimi mwenyewe, Mzee Chillo, Mama Kawele, Mama Njaidi, Taffu, Dude na wengine na ni bonge la kazi la kuanzia mwaka 2015," alisema Baby Madaha.
Mwanadada huyo anayetamba na nyimbo kama 'Summer Holiday' akiwa na albamu mbili sokoni za Amore na Desperado' amejipatia umaarufu mkubwa katika uigizaji wa filamu baadhi ya kazi alizowahi kuzicheza ni 'Nani', 'Misukosuko3', 'Mpishi', House Na.44' na 'Ray of Hope' iliyoshinda tuzo ya kimataifa nchini Nigeria.

DECEMBER LIKIZO FESTIVAL KUFANYIKA KESHO MBEZI BEACH

TAMASHA la tatu la December Likizo Festival linatarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam likihusisha na maonyesho ya muziki, mavazi na filamu sambamba na semina mbalimbali juu ya kuboresha ufanisi wa vipaji vya sanaa.
Mratibu wa tamasha hilo, Steven Sandhu 'Triple S',  alisema kwa wiki nzima kumekuwa na shughuli mbalimbali za tamasha hilo na leo ndiyo kilele chake.
Sandhu ambaye ni mwanamitindo na muigizaji filamu alisema kilele cha tamasha (le grand Finale) la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach.
"Tamasha la tatu la 'December Likizo Festival kwa mwaka wa 2014 litafikia kilele kesho kwenye Landmark Hotel kwa maonyesho mbalimbali na kwa wiki nzima kuelekea kilele cga tamasha hilo kulikuwa na shughuli mbalimbali," alisema.
Sandhu alisema anashukuru uitikiaji wa wito kwa wasanii na washiriki wengine wa tamasha hilo na kuongeza imani yake kama ilivyokuwa kwa matamasha mawili ya nyuma ya mwaka 2012 na 2013, hata la mwaka 2014 litafana zaidi," alisema.

KWA MASHABIKI WA WENGE MUSICA BCBG

Liverpool yaendelea 'maajabu' EPL, yaifumua Swansea City 4-1

The 26-year-old is mobbed by his Liverpool team-mates after helping his side towards a vital three points at Anfield
Liverpool wakishangilia mabao yao
Moreno now has two Premier League goals to his name since joining Liverpool from Sevilla in the summer
Moreno akishangilia bao la kuongoza la Livwerpool
Reds midfielder Lallana runs towards the Kop in celebration of his second half goal
Adam Lallana akishangilia moja ya mabao yake mawili
Three Swansea players look on as Lallana sends a left-footed finish past Fabianski to send Liverpool into a commanding lead
Lallana akiwatesa mabeki wa Swansea
MABAO mawili yaliyofungwa na Adam Lallana na moja la kujifunga la beki wa Swansea City imeiwezesha Liverpool kupata ushindi wake wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England.
Ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Anfield, Liverpool ilianza pambano hilo kwa mashambulizi langoni mwa wageni wao na kuandika bao la kwanza katika dakika ya 33 kupitia kwa Alberto Moreno aliyemalizia kazi ya Henderson.
Kipindi cha pili kilikuwa na mafanikio zaidi kwa vijana wa Branden Rodgers baada ya Lallana kuandika bao la pili dakika ya 51 kabla ya Swansea kuandikisha bao lao pekee dakika moja baadaye kupitia Gief Sigurdsson.
Adam Lallana alirudi tena kambani kwa kuandika bao la tatu la Liverpool dakika ya 61 na dakika tano baadaye beki wa Swansea City, Shelvey alijifunga katika harakati za kuokoa mpira na kuifanya Liverpool kupaata ushindi mnono wa mabao 4-1 na kuchupa hadi nafasi ya nane katika msimamo wa ligi hiyo.
Liverpool wamefikisha pointi 28 sawa na Swansea lakini imefanikiwa kuwashusha wapinzani wao kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ushindi huo wa Liverpool wa mabao manne ni wa kwanza tangu nyota wao, Lusi Suarez kutimkia Barcelona.

Kumekucha! Patrick Phiri atimuliwa Simba, Kopunonic amrithi

Patrick Phiri (kushoto) aliyetimuliwa Simba wiki kadhaa baada ya Yanga kumtimua Marcio Maximo
http://umwungeri.com/wp-content/uploads/2014/09/1331248128Goran-Kopunovic.jpg
Kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic
BAADA ya Yanga kumtimua kocha wao Marcio Maximo kutokana na kipigo cha mechi yao na mtani wao Simba kwenye mechi ya 'bonanza' ya Nani Mtani Jembe2, Simba nao wamefuata mkumbo huo baada ya kutangaza kumtimua kocha wao Mzambia, Patrick Phiri.
Simba imemfukuza kocha huyo kutokana na kutoridhishwa na matokeo iliyopata timu yao katika msimu huu ikiwamo kipigo cha bao 1-0 ilichopewa na Kagera Sugar mwishoni mwa wiki.
Kocha huyo aliyemrithi Zdravkov Logarusic aliyetimuliwa mapema amekuwa hana matokeo mazuri tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu.
Hii ni mara ya tatu kwa Phiri kuifundisha Simba tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu ameiongoza katika michezo 22 na kushinda nane, kati ya hizo ni moja tu ya Ligi Kuu na moja ya Nani Mtani Jembe.
Aidha taarifa zinasema kuwa Mserbia Goran Kopunovic kutoka Polisi Rwanda ndiye atakayeinoa Simba na kocha huyo atawasili kesho Jumatano.
Kocha huyo mpya aliyewahi kuzinoa timu za APR atakuja na msaidizi wake Mnyarwanda Jean Marie Ntagawabila na kumaanisha kuwa hata kocha msaidizi wa Simba aliyekuwa na Phiri, Suleiman Matola naye ameenda na maji katika maamuzi yaliyofikiwa na uongozi wa juu wa Simba.
Simba na Yanga kwa muda mrefu sasa zimekuwa na utamaduni wa kutimua na kuajiri makocha wapya kila mara bila kujali vipindi wanavyokuwa na timu zao, jambo ambalo linadaiwa limekuwa likiwachanganya wachezaji kwa kushindwa kunasa mafunzo ya makocha wanaoletwa na kabla ya kuzoeana nao hutimuliwa.
Bahati mbaya ni kwamba klabu hizo zimekuwa zikitimua makocha hata wakati timu zao zikiwa katika nafasi nzuri tofauti na inavyoshuhudiwa Ulaya klabu zikiwatimua makocha kutokana na timu kufanya vibaya.