STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 30, 2014

Real Madrid yasisitiza Gareth Bale HAUZWI kokote!

Bale celebrates winning the FIFA Club World Cup earlier in December 
Gareth Bale
RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amesisitiza kuwa Gareth Bale hauzwi na kuzitaja taarifa kwamba amepokea ofa kutoka Manchester United ni upuuzi mtupu.
Bale, aliyejiunga na Real Madrid akitokea Tottenham kwa dau lililovunja rekodi ya uhamisho duniani ya karibu Pauni Mil. 85 Septemba 2013 amekuwa akidaiwa kuwa yu mbioni kurejea tena Ligi Kuu ya England.
United imedaiwa kuwa tayari kutoa Pauni 120 ili kumnyakua nyota huyo wa kimataifa wa Wales, lakini Perez amepuuza taarifa hizo na kudai Bale, 25 hawezi kuondoka Santiago Bernabeu.
Perez aliliambia gazeti la michezo la Marca: "Hatujapokea ofa yoyote kuhusu Gareth Bale, siyo klabu ya Manchester United wala klabu nyingine yoyote.,"
"Kadhalika hatutakuwa tayari kusikilizia ofa yoyote juu ya Bale kwani ni mchezaji muhimu mno kwetu," alisema Perez.
Bale amekuwa na wakati mzuri tangu ajiunge na kigogo hicho cha Hispania akiunda safu kali ya ushambuliaji akishirikiana na  Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
Nyota huyo wa zamani wa Southampton aliisaidia Real Madrid kunyakua taji la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafumua wapinzani wao wa Madrid, Atletico Madrid kwa mabao 4-1 katika fainali iliyozikutanisha timu hasimu za jiji moja.

No comments:

Post a Comment