STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, September 20, 2013

Shafii Dauda achimba mkwara mzito, kisa...!

Shafii Dauda
MCHAMBUZI maarufu wa soka nchini, Shafii Dauda ameuchimba mkwara uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaodaiwa kutaka kuendelea kumwekea mizengwe katika kuwania uongozi ndani ya shirikisho hilo.
Dauda, ambaye ni miongoni mwa wagombea waliokuwa wameondolewa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF utakaofanyika mwezi ujao na kurudishwa na kamati ya Maadili ametema cheche hizo kupitia akaunti ya Facebook.
Mwanamichezo na mtangazaji huyo, amelazimika kuchimba mkwara huo baada ya kusisikia fununu za kutaka kuwekewa zengwe kama ilivyowahi kusikia awali na kujikuta kweli jina lake likitupwa kwa madai ambayo hayakuonekana kama ana hatia.
Dauda ameomba kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ambapo jina lake la wenzake kadhaa yalitemwa kabla ya Kamati ya Maadili ya TFF chini ya Jaji Jesse Mguto kuwarejesha tena kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 27.
Ebu isome mwenyewe ujumbe huo, ingawa kuna baadhi ya sarufi tumezirekebisha ili ziende sawia la lugha fasaha ya kiswahili;
"Siku chache za nyuma nilizisikia njama za baadhi ya viongozi wa TFF kutaka kuondoa jina langu kwenye mchakato wa uchaguzi wa TFF na kulipeleka kwenye kamati ya Maadili eti nili-publish barua ya FIFA kwenye blog yangu bila idhini yao, nikazipuuzia nikidhani ni stori tu za mitaani,muda ulipofika Taarifa ya TFF ikatoka kweli jina langu likapelekwa kwenye kamati ya Maadili kwasababu zile zile nilizozisikia kabla kwa watu,Kamati ya MAADILI ikaniita nikayasikiliza mashitaka ya Secretarieti ya TFF ambayo iliwakilishwa na Afisa Habari ndugu yangu Boniface Wambura ikanihoji namimi nikatoa utetezi wangu na hatimaye kamati ikaonelea sina kesi ya kujibu hivyo basi jina langu likarudishwa kwenye mchakato wa uchaguzi. Kutoka kwenye vyanzo vyangu mbali mbali ndani ya TFF eti sasa wanajipanga kesho kutoa PRESS ya kuliondoa tena jina langu eti kwa kigezo sina UZOEFU,sasa ninachowambia kama ni kweli yanayozungumzwa WASITHUBUTU kufanya hivyo kwani kwa mara nyingine tena watanipa pointi 3 za mezani.IJUMAA KAREEM!

Simba, Mbeya City uso kwa uso, Mtibwa yaifuata Prisons Mbeya, kivumbi za FDL nacho mmh!

Mbeya City
Simba
Na Boniface Wambura

BAADA ya kuifanyia mauaji ya kutisha Mgambo JKT, vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba kesho itaikaribisha Mbeya City ambayo iliyozidindia Yanga na Mtibwa Sugar katika mechi zake mbili zilizopita.
Simba itaialika Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu kwenye dimba la Taifa ikiwa ni muendelezo ya michezo ya ligi kuu (VPL) inayopingia raundi yake ya tano ambapo pia itashuhudiwa michezo mingine mitatu tofauti.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.


Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.


Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.


Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).


Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. 
Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.


Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. 
Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

NSSF YAIPIGA JEKI' ROCKY CITY MARATHON 2013

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini BMT, Dioniz Malinzi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mbio za Rocky Marathon.  
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa mbio za Rocky City Marathon uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo NSSF imedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15. 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleima Nyambui.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa uzinduzi wa mbio za Rocky Marathon 2013 Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, akizindua rasmi mbio za Rocky City Marathon 2013 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu ambao wamedhamini mbio hizo kwa kutoa sh.milioni 15. 
 Baadhi ya wadau.
Picha ya pamoja.
MSIMU wa tano wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa, ambapo mdhamini mkuu Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetaka kuwepo kwa mgawanyo wa majukumu kwa mbio za umbali tofauti ili kuharakisha uendelezaji wa vipaji vya wanariadha nchini.

Rock City Marathon zinaratibiwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), ambapo Ofisa Uhusiano wa NSSF inayodhamini mbio hizo kwa mwaka wa nne sasa, Juma Kintu aliliomba Shirikisho la Riadha Tanzania RT kugawana majukumu na wadau.

“Sisi kama NSSF tuko tayari kudhamini na kuchangia maendeleo ya riadha nchini, ndio maana tunasisitiza mgao wa majukumu kwa wakimbiaji wa umbali fulani kusimamiwa na taasisi au kampuni moja, ili kusaidia maendeleo ya haraka na makuzi sahihi ya vipaji,” alisema Kintu.

Pamoja na NSSF, wadhamini wengine wa Rock City Marathon 2013 zitakazofanyika jijini Mwanza Oktoba 27 ni pamoja na PPF, Airtel, African Barrick, Nyanza Bottlers, Sahara Media, Precission Air, Bank M, New Mwanza Hotel na Umoja.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, aliyekuwa mgeni rasmi, alisema mchezo wa riadha nchini unaelekea kuangamia na jitihada za kuunusuru zinahitajika.

“Ni aibu kuwa mchezo wa riadha nchini unaelekea kufa wakati viongozi waliopewa mamlaka ya kuhakikisha unaendelea wanashuhudia. Ni wakati wa kuamka kuunusuru mchezo huu ambao katika miaka ya 1970 mpaka 1980 uliiletea nchi yetu heshima kubwa.

Kwa upande wake, Rais wa RT, Suleiman Nyambui aliwataka waratibu wa marathon kote chini kuhakikisha wanakuwa na mbio fupi za vijana ili kupanua wigo wa kuzalisha vipaji vipya, vitakavyoliletea sifa taifa na kushinda mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Naye Mgurugenzi Mtendaji wa Capital Plus, Ellen Otaru Okoedion, aliishukuru Serikali kwa ahadi ya ushirikiano, lakini akaitaka kuhakikisha inakaa mezani na (kina Nyambui) RT, ili kujadili njia sahihi zitakazofanikisha kupatikana kwa kina ‘Nyambui wapya.’

Aidha, Mratibu wa tukio hilo, Mathew Kasonta alisema kuwa mbio hizo zitajumuisha  kilometa tano kwa wakimbiaji kutoka katika makampuni, kilometa tatu kwa wenye ulemavu, kilometa tatu kwa watu wazima (zaidi ya miaka 55) na kilometa mbili kwa watoto wenye umri kati ya miaka 7 mpaka 10.

Msiba tena! Mwanajeshi mwingine wa Tanzania afariki Congo

http://4.bp.blogspot.com/-T65esf8KL6k/Uh_cjsRA_gI/AAAAAAAAovQ/Q0CnrE4IYWQ/s640/mwamnyange.jpg
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamnyange

MSIBA tena! Hizi ni habari za kusikitisha kusikia, ila ni kwamba  shujaa mwingine wa Tanzania amefariki dunia katika harakati za kulinda amani ya waafrika wenzetu. 
Habari zilizotolewa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) zinasema mwanajeshi anayetambulika kwa jina la Private Hugo Munga, ambaye alijeruhiwa kwenye shambulio lilisababisha Meja Khatibu kufariki dunia, naye amefariki.
Mwanajeshi huyo alikuwa nchini South Africa kwa ajili ya matibabu, lakini kwa bahati mbaya Tanzania imempoteza shujaa huyu. 
Mwili wake unatarajiwa kufikishwa hapa nyumbani kesho ukitokea nchini South Africa.
1j
2j

Polisi Dar wapiga marufuku maandamano ya Wapinzani, kisa...!

http://2.bp.blogspot.com/-lTP5tlaQdX8/TqptaqAKbAI/AAAAAAAAAK0/vVbVnC8IrhI/s1600/Kova1%252814%2529.jpg
Kamanda Suleiman Kova
JESHI la Polisi Jijini Dar es Salaam limeyapiga marufuku maandamano ya umoja wa vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA yaliyopangwa kufanyika kesho Jumamosi.
Maandamano hayo yaliyokuwa  yamepangwa  kuanzia Tazara hadi Jangwani kisha Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali .

Taarifa  iliyotolewa  na Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova kupitia ITV   imeeleza kuwa Polisi wamechunguza na kugundua kwamba  maandamano  hayo  yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano. 

Masogange aanza kufurahia 'uhuru' wa dhamana aliyopewa 'Kwa Mabida'

Mcheki katika picha hizi alizotupia leo mtandaoniPicha hizi Amezipiga akiwa Gym leo asubuhi zinazidi kutoa ushahidi kuwa yupo Mtaani ...au jela za South Mambo ndio hivi ? We unasemaje?

Waziri Mukangara mgeni rasmi Redd's Miss Tanzania

Vimwana wanaotarajiwa kuchuana kesho kwenye shindano la Redd's Miss Tanzania 2013
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shindano la urembo la taifa mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2013' litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar se Salaam.
Gazeti la kila siku la NIPASHE linalochapishwa na Kampuni ya The Guardian Ltd ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo litakalotoa mwakilishi wa nchi katika fainali za Urembo za Dunia (Miss World).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, alisema jana wanatarajia  kiongozi huyo wa serikali kushuhudia shindano hilo na kwamba amesharidhia kuwa mgeni rasmi.
Lundenga alisema kila kitu kimekamilika na kuwataka wadau wa sanaa ya urembo kusubiri kushuhudia shindano lililo bora zaidi ya miaka iliyopita.
"Maandalizi yamekamilika na kama ni chakula, sasa kinachosubiriwa ni kukila tu," alisema kwa kifupi mratibu huyo ambaye kampuni yake imekuwa ikiandaa shindano hilo tangu 1994.
Alisema shindano hilo litapambwa na burudani kutoka kwa mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa kike nchini, Judith Wambura 'Lady Jay Dee' ambaye kwa sasa anatamba na vibao vyake vya Yahaya na Joto Hasira, Mike Rose wa Uganda na kikundi cha ngoma za asili cha Mama Afrika.
Shindano hilo linatarajiwa kushirikisha warembo 30 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakaowania taji linaloshikiliwa na Brigitte Alfred, kutoka Kanda ya Kinondoni jijini ambaye kwa sasa yuko Indonea akijiandaa kupanda jukwaani kuwania taji la dunia ifikapo Septemba 28, mwaka huu.
Hata hivyo, warembo watano wameshatinga hatua ya 15 bora baada ya kutwaa mataji madogo yaliyoshindanishwa wakiwa kambini.
Warembo hao ni Severina Lwinga, kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam ambaye ni Redd's Miss Personality, Prisca Clement (Redd's Miss Tanzania Talent), Clara Bayo (Redd's Miss Sports Woman ), Happiness Watimanywa (Redd's Miss Photogenic) na Narietha Boniface ambaye ni Redd's Miss Tanzania Top Model.
Mshindi wa taji hilo mwaka huu atabeba dhamana ya kuiwakilisha nchi katika shindano la urembo la dunia mwakani na zawadi ya Sh. milioni nane pamoja na gari lenye thamani ya Sh. milioni 15.

Homa ya pambano la Man Utd, City yaanza

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01507/kompany_1507398a.jpg
Vincent Kompany
http://www.independent.co.uk/incoming/article8668976.ece/BINARY/original/wayne-rooney.jpg
Wayne Rooney


KATIKA kile kinachoonekena kama ni kuanza kupanda kwa 'homa ya pambano' baina ya wapinzani wa mji wa Manchester, Manchester United na Manchester City waachezaji wa timu hizo wameanza kutambiana.
Beki nmahiri wa Manchester City, Vincent Kompany amesema anasubiri kwa hamu kucheza dhidi ya Wayne Rooney keshokutwa Jumapili na anatumai kwamba mshambuliaji huyo wa Manchester United atakuwa katika kiwango chake cha juu.
Rooney amefunga magoli matatu katika mechi mbili tangu aliporejea katika kikosi kwa kwanza baada ya kupata jeraha la katika paji la uso lililomweka nje ya uwanja lakini nahodha huyo Man City alipuuza mitazamo kwamba anatamani kuona kiwango cha mshambuliaji huyo kinakuwa chini katika mechi yao ya mahasimu wa mji wa Manchester Jumapili.
"Hapana. Unahitaji kucheza dhidi ya wachezaji walio katika kiwango chao cha juu kabisa," aliwaambia waandishi wa habari. "Hivyo ndivyo ninavyoona. Daima nataka kucheza dhidi ya wachezaji wanaokuwa katika kiwango chao bora kabisa.
"Nina furaha sana kwa Wayne kwamba yuko katika kiwango cha juu. Huu ndiyo utamu wa Ligi kuu ya England, unacheza dhidi ya washambuliaji wakubwa wakati wote, lakini kuna wachezaji wengi wa kuchunga katika timu zote."
David Moyes na Manuel Pellegrini wanaelekea katika mechi yao ya kwanza ya watani wa jadi wa mji wa Manchester wakiwa kama makocha wa timu hizo, ingawa Mscotland huyo alishinda mechi nne mfululizo kwenye Uwanja wa Etihad baina ya mwaka 2008 na 2010 wakati akiifundisha Everton.
Lakini Kompany haamini kama matokeo hayo ya zamani yana mchango wowote katika kitakachotokea Jumapili.
"Ni timu tofauti, ni msimu tofauti na naweza kusema kwamba huwezi kutabiri matokeo ya mechi hii ya watani wa jadi," aliongeza. "Hakuna mtu aliyetabiri kwamba tungeshinda 6-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford (katika msimu wa 2011-12), kwamba wangetufunga kwenye Uwanja wa Etihad au kwamba tungeshinda Old Trafford (msimu uliopita). Nadhani hicho ndicho mashabiki wanachopenda. Mechi isiyotabirika.
"Ni mechi ambayo daima unaisubiri. Sidhani kama watu wa mjini Manchester tu bali duniani kote wanajiandaa kufurahia mechi hiyo.
"Ni mechi ambayo inavutia kwa mengi. Sijawahi kuichukulia poa na najiona kubarikiwa kucheza katika mechi hizo. Unafanya kila uwezalo kuhakikisha unacheza vyema katika mechi hizi."
 

Tottenham, Swansea, Fiorentina 'zaua' Ulaya

Goal king: Jermain Defoe scored twice in the first half as Spurs cruised to victory
Defoe akishangilia moja ya mabao yake ya jana
Up and running: Swansea celebrate after Wilfried Bony scored the club's first European goal
Swansea City wakishangia moja ya mabao yao yalioizamisha Valencia
WAKATI Swansea wakishinda ugenini dhidi ya wenyeji wao Valencia ya Hispania, 'Vijogoo' vya Londo ya Kaskazini, Tottenham Hotspur wenyewe wameikandika Tromso kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani katika mechi za Ligi ndogo ya UEFA.
Valencia iliyomaliza mchezo huo ikiwa pungufu baada ya mchezaji wake Adil Rami kutolewa dakika 10 kabla ya pambano kuisha ilijikuta ikilala nyumbani kwa mabao ya Wilfried Bony, Michu na Jonathan de Guzman.
Katika mchezo wa Spurs dhidi ya Tromso, washindi walipata mabao yake kupitia Jermain Defoe aliyefunga mara mbili na jingine la Christian Eriksen.
Mechi nyingine  timu ya St. Gallen iliishinda 2 - 0 dhidi ya Kuban' Krasnodar,        Dinamo Zagreb ikalala nyumbani 2-1 mbele ya Chornomorets kama ilivyokuwa kwa PSV iliyonyukwa mabao 2-0 nyumbani na Ludogorets.
Nayo timu ya Salzburg iliisasambua Elfsborg kwa mabao 4-0, Standard Liège ikalala 2-1 kwa Esbjerg, Zulte-Waregem na Wigan zikatoka suluhu, Maribor ikalala 5-2 kwa Rubin Kazan' na Fiorentina ikashinda nyumbani 3-0 djhidi ya Paços de Ferreira.
Mechi nyingine matokeo yake ni kama ifuatavyo;
Pandurii Târgu Jiu  0-1 Dnipro Dniprop…    
Eintracht Fran…    3-0  Bordeaux    
Maccabi Tel Aviv    0-0  APOEL    
Dynamo Kyiv     0-1  Genk    
Thun     1-0  Rapid Wien    
Freiburg    2-2  Slovan Liberec    
Estoril     1-2  Sevilla    
Real Betis    0-0  Olympique Lyonnais
Vitória Guimarães   4-0  Rijeka    
Apollon     1-2 Trabzonspor    
Lazio     1-0  Legia Warszawa
Sheriff    0-0  Anzhi    
PAOK     2-1  Shakhter Karagandy    
Maccabi Haifa   0-1 AZ