STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 6, 2016

Simba yaongoza 1-0 dhidi ya URA, JKU yaifumua Jamhuri 3-0

KIPINDI cha pili cha pambano la michuano ya Kombe la Mapinduzi Kundi A limeanza kipindi cha pili sasa na Simba wanaongoza kwa bao 1-0.
Bao lao liliwekwa kimiani na Ibrahim Ajib, baada ya mabeki wa URA Uganda kuzembea kuokoa mpira langoni mwao na Ajib kufumua shuti lililotinga kimiani.
Pambano ni kali kweli kweli. Katika mchezo wa mapema jioni, JKU ilifumua Jamhuri Pemba kwa mabao 3-0.

Yanga wapewa Friends, Simba watupwa Moro Kombe la FA

Toto Africans wataumana na TP Lindanda, Pamba-Mwanza
African Lyon itakayoumana na Azam FC
Coastal Union

Mbeya City itatoka salama kwa Wenda FC
JKT Ruvu wanaoisubiri mshindi kati ya Lipuli na Kurugenzi Mafinga

Yanga itaifanyia nini Friends Rangers?
Kikosi cha Mgambo JKT

Azam wamepewa Lyon, watavuna nini
Simba wataifuatya Burkina Faso mjini Morogoro
 MICHUANO ya Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa tatu inatarajiwa kuendelea Januari 12 na wikiendi ya Januari 23-27 kwa timu 32 kuchuana kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.
Timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara zimeingia moja kwa moja mzunguko wa tatu ambapo Yanga yenyewe imepangwa kuumana na Friends Rangers, huku watani zao Simba wakipelekwa Morogoro kuvaana na Burkina Faso.
Timu nyingine 16 zilizofuzu kutoka raundi ya pili ni zile za Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF ni kwamba Jumamosi Januari 12, Majimaji itacheza dhidi ya JKT Mlale uwanja wa Majimaji mjini Songea, Januari 23 Pamba v Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, Ndanda FC v Mshikamano Nagwanda Sijaona Mtara, huku Burkinafaso wakiwakaribisha Simba SC katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Januari 24, Young Africans watacheza dhidi ya Friends Rangers uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Njombe Mji v Tanzania Prisons uwanja wa Amani Makambako, mjini Shinyanga Stand United watachuana dhidi ya Mwadui FC.
Mechi zingine ni Kagera Sugar v Rhino Rangers, Panone v Madini, Mtibwa Sugar v Abajalo, Lipuli/Kurugenzi v JKT Ruvu, Ashanti United v Azam FC, Africa Sports v Coastal Union, Geita Gold v Mgambo Shooting, Singida United v Mvuvuma na Wenda v Mbeya City.
Timu 15 zilizofuzu hatua ya tatu kutoka raundi ya pili ni Ashanti United, Friends Rangers, Panone, Geita Gold, Pamba, Mvuvuma, Burkinafaso, Rhino Rangers, Madini FC, JKT Mlale, Mshikamano FC, Njombe Mji, Wenda FC, Singida United, Abajalo huku mchezo mmoja kati ya Lipuli dhidi ya Kurugenzi ukichezwa leo Jumatano lakini ulishindwa kumalizika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuvunja mchezo dakika ya 23 na kesho Alhamisi utamaliza muda uliosalia ili kupata mshindi wa kufuzu raundi ya tatu.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

Ratiba kamili hii hapa:
Jan 12, 2016
MajiMaji v JKt Mlale -Majimaji Songea
 

Jan 23, 2016 
Pamba v Totyo Africans- CCM Kirumba, Mwanza
Burkina Faso v Simba- Jamhuri, Morogoro
Ndanda v Mshikamano- Nangwanda Sijaona, Mtwara
 

Jan 24, 2016
 Yanga v Friends Rangers- Taifa, Dar es Salaam.
Njombe Mji v Prisons-Mbeya- Amani, Makambako
Stand United v Mwadui- Kambarage Shinyanga
 

Jan 25, 2016
 Kagera Sugar v Rhino Rangers- Ali Hassan Mwinyi, Tabora
Panone v Madini- Ushirika, Moshi
 

Jan 26, 2016 
Mtibwa Sugar vAbajalo-Jamhuri, Morogoro
Lipuli/Kurugenzi v JKT Ruvu-Wambi, Mafinga
African Lyon v Azam-Karume, Dar es Salaam
African Sports v Coastal Union-Mkwakwani Tanga
Geita Gold Sports v Mgambo JKT- Nyankungu, Geita
 

Jan 27, 2016 
Singida Utd v Mvuvumwa- Namfua, Singida
 

Feb 10, 2016
Wenda v Mbeya City- Sokoine, Mbeya

Azam kutetea taji la Kagame visiwani Zanzibar

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye na Rais wa Heshima wa Cecafa, Leodger Tenga
AZAM FC watatetea taji lao la Kombe la Kagame visiwani Zanzibar, baada ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati, CECAFA kutangaza tarehe ya michuano hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kufanyika Julai – Agosti mwaka huu kisiwani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye amesema pamoja na michuano ya klabu kufanyika  Zanzibar mwaka huu, pia wamejipanga kuendesha michuano ya U17 itakayofanyika Mei huko Uganda, michuano ya Soka kwa Wanawake (Uganda), Mashindano ya vijana chini ya miaka 20 (Burundi) huku michuano ya Chalenji 2016 imepangwa kufanyika nchini Sudan.
Mwishoni mwa wiki uongozi wa Kamati ya Utendaji wa CECAFA ulikutana nchini Sudan na kufanya kikao chake cha kwanza chini ya Rais Dk. Mutasim Ghafar ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka nchini Sudan (SFA).
Katika kikao hicho, CECAFA ilitangaza kumpa Leodgar Tenga Rais wa heshima wa Cecafa huku pia wakisaini makubaliano ya uendelezaji wa soka la vijana na Chama cha Soka cha Saudi Arabia (SAFF) kupitia kwa Rais wake Ahmed Alharbi.
Azam ndio mabingwa wa watetezi wa Kagame waliotwaa Agosti mwaka jana jijini Dar es salaam, wakati Uganda ndio watetezi wa Kombe la Chalenji.