STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 6, 2016

Azam kutetea taji la Kagame visiwani Zanzibar

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye na Rais wa Heshima wa Cecafa, Leodger Tenga
AZAM FC watatetea taji lao la Kombe la Kagame visiwani Zanzibar, baada ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati, CECAFA kutangaza tarehe ya michuano hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kufanyika Julai – Agosti mwaka huu kisiwani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye amesema pamoja na michuano ya klabu kufanyika  Zanzibar mwaka huu, pia wamejipanga kuendesha michuano ya U17 itakayofanyika Mei huko Uganda, michuano ya Soka kwa Wanawake (Uganda), Mashindano ya vijana chini ya miaka 20 (Burundi) huku michuano ya Chalenji 2016 imepangwa kufanyika nchini Sudan.
Mwishoni mwa wiki uongozi wa Kamati ya Utendaji wa CECAFA ulikutana nchini Sudan na kufanya kikao chake cha kwanza chini ya Rais Dk. Mutasim Ghafar ambaye pia ni Rais wa Chama cha Soka nchini Sudan (SFA).
Katika kikao hicho, CECAFA ilitangaza kumpa Leodgar Tenga Rais wa heshima wa Cecafa huku pia wakisaini makubaliano ya uendelezaji wa soka la vijana na Chama cha Soka cha Saudi Arabia (SAFF) kupitia kwa Rais wake Ahmed Alharbi.
Azam ndio mabingwa wa watetezi wa Kagame waliotwaa Agosti mwaka jana jijini Dar es salaam, wakati Uganda ndio watetezi wa Kombe la Chalenji.

No comments:

Post a Comment