STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 1, 2014

Inter Milan yapigwa 4-2 na Roma, Gervinho atupia moja

http://www.iberita.com/wp-content/uploads/2014/11/Jadwal-Liga-Italia-2014-Terbaru-Pekan-Ini-30-November-dan-1-2-Desember-2014.jpg
AS Roma wakishangilia moja ya mabao yao yaliyoizamisha Inter Milan
KLABU ya Inter Milan usiku wa jana imeshindwa kufurukuta nyumbani kwa AS Roma baada ya kubanduliwa mabao 4-2 katika pambano kali la Ligi Kuu ya Italia, Serie A.
As Roma iliwakaribisha wapinzani wao kwa bao la dakika ya 21 kupitia kwa Gervinho kabla wa wageni hao kusawazisha kupitia kwa Ranocchia dakika ya 36.
WWEnyeji waliongeza bao la pili dakik achache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia kwa Holebas kabla ya funga nikufunge kuendelea kwa Inter Milan kurejesha bao hilo kwa mkwaju wa Osvaldo dakika ya 57.
Magoli mawili ya Pjanic ya dakika ya 60 na 90 yaliisaidia wenyeji kuibuka na ushindi huo na kuendelea kuwafukuza Juventus waliopo kileleni wakitofautiana pointi tatu, Juve wakiwa na 34 na Roma 31 zote zikiwa zimecheza mechi 13kila moja.

Macho vya Vishal, Pingu videoni, audio njiani

Pingu na Vishali katika pozi

Vishali
BAADA ya kuachia video ya 'Macho' inayoendelea kutamba hewani, msanii Vishal Milanzi 'Vishal' yupo katika maandalizi ya kutengeneza kazi nyingine mpya atakayoanza kuirekodi mara baada ya kurusha hewani 'audio' ya wimbo huo wa Macho alioimba na mzoefu Pingu.
Akizungumza na MICHARAZO, Vishal alisema alitanguliza video hewani na wiki ijayo ndiyo ataachia 'audio' kabla ya kuanza mipango ya kurekodi kazi nyingine mapya akimshirikisha pia Pingu mmoja wa wasanii wa muda mrefu nchini anayetamba na nyimbo mbalimbali.
"Niliamua kutanguliza video hewani, kabla ya 'audio' yake na ninashukuru mashabiki wameikubali kazi na imenitia moyo wa kuanza kutengeneza kazi nyingine mpya. Kazi hizo zitafuata baada ya 'audio' ya 'Macho' kutoka," alisema Vishal.
Msanii huyo alidokeza kuwa wimbo huo atakaouachia hewani wiki ijayo umerekodiwa studio za Triple One Records kwa Kizo One na video yake imetengenezwa Rubby Videos na ‘Audio' na zitatengenezwa katika studio nyingine kwa lengo la kuipa vionjo tofauti.

Barcelona yaipumia Real Madrid, Messi apigwa

Otamendi falls to the floor in theatrical fashion, but Neymar had forcefully moved his head towards the Valencia man's jaw
Kulaaa! Neymar akimlamba kichwa beki wa Valencia aliyemchezea kitemi kabla
Players of both Valencia and Barcelona then got involved in a heated discussion after the incident
Mzozo baina ya wachezaji wa Valencia na Barcelona
Messi looks to get Barcelona on the attack during the second half of their clash with ValenciaKLABU ya Barcelona imezidi kuwapumulia wapinzani wao Real Madrid baada ya usiku wa jana kupata ushindi mwembamba ugenini dhidi ya Valencia huku nyota wake Lionel Messi akipigwa na chupa uwanjani.
Barcelona walioivaa Valencia katika uwanja wa Mestalla walipata ushindi huo kupitia bao la 'jioni' lililofungwa na Sergio Busquets dakika ya 90, kabla ya Lionel Messi kupigwa na chupa. Katika pambano hilo lilishuhudiwa undava ukitembezwa uwanjani kwatai Neymar alipompiga kichwa Nicolas Otamendi baada ya beki huyo kuanza kumcheza ‘kitemi’ Mbrazil huyo. Otamendi alimchezea kibabe Neymar kwenye eneo la hatari, lakini alipokwenda kumuinamia kumuomba msamaha, alilambwa kichwa ‘kishikaji’ kabla ya kuibuka mzozo uliohusisha wachezaji wote.
Hata hivyo Neymar hakuchukuliwa hatua zozote na refa wa pambano hilo, David Fernandez.
Ushindi huo umeifanya Barcelona kufikisha pointi 31, mbili nyuma ya Real Madrid wanaoongoza msimamo ambao walishinda mabao 2-1 ugenini siku ya Jumamosi dhidi ya Malaga.

Mkurugenzi Zugo Sports ahimiza wanawake kujifunza Martial Arts

Zuwena Idd Kipingu akionyesha umahiri kwa kunyanyua chuma katika gym yake
WANAWAKE na wasichana wamehimiza kujenga utamaduni ya kupenda kujifunza na kucheza michezo ya mapigano kwa lengo la kuwasaidia kuwaepusha na matukio la kudhalilishwa mitaani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Klabu ya Michezo ya Zugo, Zuwena Idd Kipingu, alipozungumza na blogu hii na kudai ili kuepukana na kubakwa au kuporwa na unyanyasaji mwingine wasichana na wanawake wanapaswa kujifunza na kucheza michezo ya mapigano (Martial Arts).
Zuwena alisema michezo hiyo mbali na kuwaweka kuwa fiti pia itawasaidia kwa ulinzi wao binafsi pale wanapovamiwa au kukumbana na wahalifu mahali popote.
"Wanawake na wasichana wamekuwa wakifanyiwa uonevu na baadhi ya wanajamii kwa kuwaona ni wanyonge na legelege ni fursa yao kujifunza michezo kama ya karate, Judo, Kung-fu au ngumi ili kujiweka fiti na kukomesha unyanyasaji dhidi yao," alisema.
Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Wanawake, Maendeleo ya Vijana na Ajira kwa Wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) alisema klabu yake ipo tayari kuwapa mafunzo wanawake wanaohitaji kufanya hivyo.
"Klabu yangu ya Zugo Sports, inafundisha michezo mbalimbali, lakini wengi wao ni wanaume, nilidhani ni wakati wanawake na wasichana wakachangamka ili kujisaidia kwa mambo mengi."
Alisema mbali na kupata ulinzi binafsi katika matukio madogo madogo, lakini pia michezo itawafanya wawe na afya njema pamoja na kujitengenezea mazingira mazuri ya ajira.
Mwanadada huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa Taekwondo na aliyewahi kung'ara kwenye michezo ya kunyanyua vitu vizito na ngumi, alisema wanawake wasijiweke nyuma.
"Wasijiweke nyuma au kutishwa na madai kwamba ukicheza michezo kama hiyo hataweza kuzaa, huo ni uongo mimi nimeanza michezo hii mwaka 1980 na nina watoto saba kwa sasa," alisema.
Aliongeza kuwa, michezo ni afya, hivyo ni wajibu hata kwa wazazi kuwazoesha watoto wao kuicheza ili kuiweka miili yao salama na kuepukana na maradhi madogo madogo.