STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 3, 2013

WAFANYAKAZI STRABAG WAFUNGIWA NJE NA UONGOZI KISA....NI WA MRADI WA MABASI YA KWENDA KASI

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), ya Strabag, wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia makao makuu ya kampuni hiyo, Ubungo, Dar es Salaam asubuhi hii baada ya uongozi wa kampuni hiyo kuwafungia nje, kutokana na mgomo wa kudai maslahi zaidi kufanyika    KAMANDA WA MATUKIO

KAMANDA WA MATUKIO BLOG

IRINGA YAINYANYASA RUVUMA COPA COCA-COLA


TIMU ya soka ya mkoa wa Iringa imeanza kwa kishindo michuano ya Copa Coca-Cola kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo (Septemba 3 mwaka huu) kuitandika Ruvuma mabao 4-0.

Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa dakika ya 14 na Justin Luvanda huku Alphonce Kalinga akifunga la pili dakika ya 43.

Mabao mengine yalifungwa na Juma Rogani katika dakika ya 49 na Luvanda akafumania tena nyavu dakika ya 59.

Hiyo ni mechi ya pili mfululizo kwa Ruvuma kupoteza ambapo ya kwanza ililala mbele ya wenyeji Mbeya kwa mabao 3-0.

Shafii Dauda 'abaniwa' TFF, 40 wapitishwa kugombea

http://4.bp.blogspot.com/_doacCzzR-lE/TAZqn9IwpHI/AAAAAAAACJU/KdVXdI0QmOY/s1600/shafi+dauda.JPG
Shafii Dauda aliyeenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa TFF
 Na Boniface Wambura
Kamati ya Uchaguzi imepitisha majina ya waombaji 40 kati ya 58 kwa ajili ya uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utakaofanyika mwezi ujao.

Waliopitishwa katika orodha hiyo ya awali kwa upande wa Bodi ya Ligi ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).

Kwa upande wa Kamati ya Uendeshaji (Management Committee) ni Kazimoto Miraji Muzo na Omar Khatib Mwindadi. Walioondolewa kwa vile si wenyeviti wa klabu za daraja la kwanza kama kanuni zinavyotaka ni Michael Njuweni Kaijage, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.

Kanda namba moja (Kagera na Geita) aliyepitishwa kuwania nafasi ya ujumbe Kamati ya Utendaji ya TFF ni Kaliro Samson wakati Abdallah Hussein Musa ameondolewa kwa kutojaza fomu ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi.

Jumbe Oddessa Magati, Mugisha Galibona na Vedastus Lufano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba mbili (Mara na Mwanza). Samwel Nyalla ameondolewa kwa kutojaza kikamilifu fomu namba 1 ya maombi ya kugombea uongozi wa TFF kwa kutoonesha malengo yake.

Waliopitishwa katika Kanda namba tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Swain a Mbasha Matutu wakati Stanslaus Nyongo ameondolewa kwa kukosa sifa ya uongozi wa angalau uzoefu wa miaka mitano kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.

Kanda namba nne (Arusha na Manyara) wamepitishwa wote watatu; ambao ni Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali. Kanda namba tano (Tabora na Kigoma) nao wamepitishwa wote; Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo.

Blassy Kiondo amepitishwa peke yake kuwania ujumbe Kanda namba sita (Katavi na Rukwa) huku Ayoub Nyaulingo aliondolewa kwa kutokuwa na uzoefu uliothibitika wa miaka mitano katika uongozi wa mpira wa miguu.

Naye Nazarius Kilungeja, Kamati ilikataa maombi yake ya kugombea ujumbe kutokana na vitendo vyake visivyo vya kimichezo ambavyo kwa kiasi kikubwa vilisababisha migogoro kwenye Mkoa wa Rukwa, hivyo suala lake litawasilishwa kwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.

Kanda namba saba (Iringa na Mbeya) waliopitishwa ni David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve na Lusekelo Elias Mwanjala. Cyprian Kuyava hakupitishwa kwa vile hana uzoefu wa uongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF huku Ayoub Shaib Nyenzi akiondolewa kwa kushindwa kuthibitisha uraia wake.

Elliud Peter Mvella ameondolewa kwa kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa. Suala lake limewasilishwa katika Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.

Waliopitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge wakati Kamanga Tambwe ameondolewa kwa vile alipatikana na hatia ya kushiriki kwenye tuhumu za rushwa kwa waamuzi na kufungiwa na TFF.

Kanda namba tisa (Lindi na Mtwara) waombaji wote watatu wameptishwa. Waombaji hao ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder. Pia waombaji wote wa Kanda namba kumi (Dodoma na Singida), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima na Charles Komba wamepitishwa.

Waombaji wanne kati ya watano wamepitishwa kwa Kanda namba 11 (Morogoro na Pwani). Waliopitishwa ni Farid Mbarak, Geofrey Nyange, Juma Abbas Pinto na Twahil Twaha Njoki.

Riziki Juma Majala ameondolewa kwa vile akiwa mtendaji mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) alishindwa kusimamia Kanuni za Ligi kwa kuruhusu timu ambayo si mwanachama wa wanachama wa COREFA kucheza ligi, hivyo kusababisha mgogoro mkubwa kiasi cha mwananchi mmoja kufungua kesi ya kusimamisha Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL). Suala lake litawasilishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.

Kanda namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) wamepitishwa waombaji wote wawili. Waombaji hao ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.  Waombaji wawili kati ya watano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam).

Wagombea wawili kati ya watano wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 13 (Dar es Salaam).  Wagombea hao ni Alex Crispine Kamuzelya na Muhsin Said Balhabou.

Walioondolewa ni Omar Isaack Abdulkadir kutokana na vitendo vyake vya kutoheshimu na kutotekeleza maagizo ya TFF kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF. Atapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.

Shaffii Kajuna Dauda ameondolewa kwa kutumia nyaraka ya mawasiliano baina ya FIFA na Rais wa TFF bila idhini na kuiweka hadharani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, hivyo kukiuka maadili kwa kumiliki nyaraka ambazo hazikuwa kwenye mamlaka yake. Suala lake linapelekwa katika Kamati ya Maadili.

Naye Wilfred Kidao ameondolewa kwa kutumia nyaraka za Kamati ya Utendaji ya TFF bila ridhaa ya kamati, hivyo kukosa uadilifu. Suala lake linawasilishwa kwenye Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais, waombaji wote watatu wamepitishwa. Waombaji hao ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Wallace John Karia.

Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emil Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Rais. Omari Mussa Nkwaruro ameondolewa kwa kuwasilisha cheti chenye utata, hivyo kukiuka utashi wa Ibara ya 27(7) ya Katiba ya TFF. Pia aliwasilisha taarifa za uongo kuhusu uzoefu na kukiuka Kanuni za Maadili, hivyo suala lake linapelekwa Kamati ya Maadili.

Naye Richard Julius Rukambula ameondolewa kwa hakukidhi matakwa ya kugombea uongozi kwa mujibu wa Ibara ya 12(2)(e) ya Katiba ya TFF inayokataza masuala ya mpira wa miguu kupelekwa katika mahakama za kawaida. Hivyo naye anapelekwa katika Kamati ya Maadili kwa hatua stahiki.

Tutaitaka nafasi ya pili kwa Gambia-Kim

Kocha Kim Poulsen
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema wanaipa umuhimu mkubwa mechi ya mwisho ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia kwa lengo ni kuhakikisha wanamaliza wakiwa wa pili katika kundi hilo.

Mechi hiyo itachezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul, Gambia ambapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiem Lager itaondoka kesho (Septemba 4 mwaka huu) saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Dakar, Senegal.

Kim amesema wanataka kushinda ugenini, kwani licha ya kuwa wameshatolewa lakini ushindi utawaongezea pointi kwa ajili ya viwango (rankings) vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na pia kuepuka kuanzia ngazi ya awali ya mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa fainali za 2015.

“Tunacheza mechi hii tukiwa katika mazingira magumu, kwani wengi wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ni majeruhi. Sijawahi kukutana na hali hii tangu nilipoanza kuifundisha Taifa Stars, lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Kim.

Amesema kwa mipango ya timu yake mechi hiyo ni muhimu tofauti na wengi wanavyofikiria, na uamuzi wake wa kumwita beki Henry Joseph amezingatia mambo mengi ya kiufundi ikiwemo nafasi anayocheza na uzoefu wa mchezaji aliyekuwa akicheza nchini Norway katika klabu ya Kongsvinger IL.

Wachezaji majeruhi katika kikosi hicho ni Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Athuman Idd na John Bocco.

Vilevile wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu hawatakuwemo kwenye safari baada ya klabu yao ya TP Mazembe kutuma taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo mchana ikidai ni wagonjwa.
Wachezaji wanaoondoka kwenda Banjul ni Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.

Hatimaye Arsenal 'yavunja' benki

* Ozil asaini miaka mitano Arsenal

http://www.independent.co.uk/incoming/article8794558.ece/ALTERNATES/w460/mesut-ozil-getty.jpg
Kifaa kipya kilichotua Arsenal, hatimaye
LONDON, Uingereza
MESUT Ozil amekamilisha uhamisho uliogharimu paundi milioni 42 wa kutua Arsenal baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano.
Arsenal wamevunja rekodi yao ya uhamisho katika kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye alifanyiwa vipimo kwa mara ya pili jana baada ya kuafiki malipo binafsi na klabu hiyo.
Ozil amesaini mkataba utakaomfanya alipwe paundi mshahara wa 130,000 kwa wiki utakaomweka Emirates hadi mwaka 2018 baada ya Real Madrid kumruhusu kuondoka.
Atakuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Arsenal, wakati kocha Arsene Wenger akitoa paundi zaidi ya 20,000 katika kusajili mchezaji mmoja kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Zoezi la usajili barani Ulaya ulikamilika usiku wa kuamkia leo ambapo wachezaji kadhaa wamehama na kutua katika klabu mbalimbali.
Baadhi ya wachezaji waliohama ni Marouane Fellaini aliyetua Manchester United kumfuata kocha wake wa zamani, David Moyes kutoka Everton kwa kitita cha pauni Milioni 27, Victor Moses aliyetoka Chelsea kwenda Liverpool kwa mkopo, Romelu Lukaku aliyetoka Chelsea kwenda West Brom kwa mkopo.
Orodha kamili ya nani katoka wapi na kaenda wapi itawajia baadaye kidogo hapa hapa MICHARAZO.

MWANAMKE ANASWA NA SARE ZA JWTZ


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Saida Mohamed (30), mkazi wa Mwasonga Kigamboni, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). 


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 31, mwaka huu, katika eneo la Mwasonga, Kigamboni.

Alisema Saida alikamatwa na suruali saba, mashati saba ya kombati, kofia 10, shati mbili nyepesi, fulana mbili na kofia moja aina ya bareti, vyote vikiwa mali ya JWTZ.

Alisema mtuhumiwa huyo, alikuwa na begi moja la kuwekea nguo za jeshi, cheo kimoja cha Koplo na mikanda miwili ya kijeshi.

Alisema uchunguzi unaendelea juu ya mwanamke huyo ili kubaini sababu za kumiliki sare za jeshi, kabla ya kufikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, polisi wamemkamata Husein Mkondoa (25), mkazi wa Gongolamboto Mzambarauni, akiwa anaendesha pikipiki huku akiwa amevaa nguo za kiraia na kofia ngumu ya kijani yenye nembo ya Polisi.

Alisema polisi walimtilia mashaka na kumkamata mtuhumiwa na anaendelea kuhojiwa.

“Naomba kutoa onyo kwa watu wote wenye silaha na sare za jeshi wazisalimishe kwa polisi au ofisi yoyote ya Serikali, msako wa kuwakamata wahalifu utakuwa endelevu na tutaingia nyumba hadi nyumba kuwatafuta wahalifu.

“Sambamba na operesheni hii, licha ya kubadilisha uongozi katika kituo cha Polisi Ubungo, tumeamua kutupia macho vitendo vya utapeli katika eneo la Ubungo Bus Terminal, ambalo watu wengi wanajifanya askari.

“Licha ya hilo, tumeunda kikosi cha kutumia video kamera na kamera za picha mnato ili kubaini na kuchukua hatua na nyendo mbalimbali ili kujenga ushahidi wa wahalifu hao wasiepuke mkono wa sheria,” alisema Kova.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kuchonga hati mbalimbali zinazotaka kufanana na za Serikali.

Kamishina Kova, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shadrack Samwel (27) mkazi wa Mbagala Sabasaba na Mwangi Samwel (38) mkazi wa Kimara Baruti.

Alisema watu hao, hawana ofisi maalumu hivyo hufanya shughuli hiyo sehemu yoyote na ofisi zao kuu ni mkoba pamoja na gari ambalo wanatembelea, lenye namba za usajili T 397 ADX aina ya Crester.

“Watuhumiwa hawa, tuliwakuta na mihuri 27 ambayo ni ya Serikali na taasisi binafsi, mihuri ya mawakili wa kujitegemea na wa serikalini, mhuri wa Jeshi pamoja na mhuri wa Serikali za mitaa.

“Pia tumewakamata na nakala mbalimbali za SUMATRA, ikiwemo karatasi za kukagulia magari, pleti namba za magari pamoja na nakala mbalimbali za ofisi hiyo,” alisema.

Katika hatua nyingine, polisi wanawashikilia watu watano, akiwamo Enea Dawsoni, ambaye ni mfanyakazi katika Kapuni ya Ndege ya Fast Jet, kwa jaribio la kutaka kupora fedha kiasi cha Sh 60,000,000 katika Kampuni hiyo.

Alisema watuhumiwa hao walinaswa katika Mtaa wa Samora na iligundulika walikuwa wana mawasiliano ya simu.

“Baada ya kuwakamata watu hawa, Polisi walielekea katika ofisi hizo na baada ya kufika walichukua simu ya watuhumiwa hao na kuona ujumbe mfupi wa maneno, ulioeleza kuwa fedha zipo karibu na chooni.

“Polisi walichukua simu ya wahalifu na walipopiga simu hiyo iliyokuwa na mawasiliano na majambazi hao, simu iliita kwa sauti kubwa ndani ya maungo ya mmoja kati ya watumishi wa Fast Jet.

“Mtumishi Enea Dawson alikuwa ameficha simu hiyo sehemu za siri katika nguo zake ambapo aliumbuka na kugundulika kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na majambazi hao,” alisema Kova.


MPEKUZI

Nyilawila ajifua akimtaka Mashali ulingoni

Bondia Karama Nyilawila akijifua mazoezini akidai anataka kuzipiga na Thomas Mashali, aliyenyakua ubingwa wa WBF-Afrika kwa kumnyuka Mada Maugo hivi karibuni.
Bondia Karama Nyilawila akijifua kumsubiri Thomas Mashali, baada ya kuwahi kumkejeli yeye na Mada Maugo kwamba ni kama 'midori' kwake.
Bondia Karama Nyilawila kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Shadrack Ignas wakati wa mazoezi yanayoendelea katika klabu yao iliyopo Sinza Makaburini, Dar es salaam. Nyilawila anafanya mazoezi kwa ajili ya kutaka kupigana na Mashali.

Hivi ndivyo visura vya Redd's Miss Tanzania 2013

HAPPINESS WATIMWANYA, Kisura huyu tayari keshanyakua taji la kwanza jana la Redd's Miss Photogenic 2013 na kupata nafasi ya kutinga nusu fainali ya shindano la taifa la Miss Tanzania 2013. Taji hilo ni kati ya mataji matano yanayowaniwa kwenye shindano hilo la urembo la Tanzania

 

                                                                    ALICE ISAAC
ANASTAZIA DONALD

CLARA BAYO

                                                             DAYANA LAIZER
                                                                             DORICE MOLLEL
ELIZABETH PERTY

                                                                  ESHYA RASHID
GLORY STEPHEN

                                                           HAPPINESS WATIMANYWA
                                                                            JACKILINE LUVANDA
JANETH AWET

JOYCE SHAYO


LATIFA MOHAMMED

                                                                              LINA ALLAN

LUCY CHARLES

                                                                     LUCY JAMES

                                                                       LUCY TOMEKA
                                                                         MARY CHEMPONDA
MIRIAM MANYANGA

                                                                        NANCY MOSHI
NARIETHA BONIFACE


                                                                          NEEMA MARITI
                                                                NICE JACK HERMAN
PHILLIOS LEMI

PRISCA PAUL

                                                                      SABRINA JUMA
SALSHA ISDORY

SARAH PAUL


SEVERINA LWINGA

                                      SVETLANA NYAMEYO