STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 14, 2012

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA KATIKA VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA



Rais Jakaya Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa uliofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Qur an.
Rais Jakaya Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa.
Rais Jakaya Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam M Mkosimonga, uharibifu uliofanywa kwenye kanisa hilo huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa.
Rais Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam M. Mkosimonga  uharibifu uliofanywa kwenye kanisa hilo wakati wa vurugu za Waislamu jana.
Rais Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es Salaam na Pwani, Mkosimonga uharibifu uliofanywa kwenye kanisa hilo huko Mbagala wakati wa vurugu za Waislamu jana Ijumaa.
You might also like:

Messi aing'arisha Argentina

Lionel Messi wa Argentina


MENDOZA, Argentina
Lionel Messi aliiongoza Argentina kuilaza timu ngumu ya Uruguay katika nusu saa ya mwisho ya mchezo kwa mabao mawili ya kifundi katika ushindi wa 3-0 jana ambao umeibakiza kileleni mwa msimamo wa kundi la Amerika Kusini la michuano ya awali ya Kombe la Dunia.
Argentina inaongoza kundi la timu tisa la Amerika Kusini ikiwa na pointi 17 katika mechi nane ambazo ni nusu ya kampeni. Colombia na Ecuador zipo pointi moja nyuma, Uruguay na Chile tano nyuma yake.
Messi alitengeneza na kumalizia goli lake la kwanza katika dakika ya 66, alipotoa pasi kwa Angel Di Maria kabla ya kukimbia kwenda kuusukumizia wavuni mpira huo uliompita Fernando Muslera.
Argentina ilipata bao la pili dakika tisa baadaye kwa muvu nyingine kwenye wingi ya kushoto, Messi akimpa pasi tena Di Maria ambaye alirudisha mpira huo kwa 'tachi' ya kwanza ambapo Sergio Aguero aliugusa na kutumbukia nyavuni.
Goli la tatu katika dakika ya 80 lilitokana na mpira wa kijanja wa adhabu ndogo wa Messi, ambaye aliudanganya ukuta wa Uruguay kwa kupitisha mpira huo chini yao na kufunga wakati wenyewe wakiruka wakitaraji atalenga lango kwa juu.
Kilikuwa kisasi kizuri kwa Messi, ambaye sasa amefunga magoli 12 katika mechi saab zilizopita za timu ya taifa, na Argentina ambayo ilitolewa na Uruguay kwa penalti katika fainali za mwaka 2011 za Copa America ambazo washiriki hao wa nusufainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 walikuja kutwaa ubingwa.
Reuters

Simba hawashikiki Bara licha ya kunasa kwa Coastal Union


Mabingwa wa ligi kuu ya Bara Simba jana walipunguzwa kasi na Coastal Union hapa Tanga, lakini angalau wakamudu kuendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo mpaka robo ya msimu, kufuatia sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Kwa sare hiyo dhidi ya Coastal iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kwa zaidi ya dakika 20, Simba imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Bara baada ya kufikisha pointi 17 kutokana na michezo saba. Wenyeji wamefikisha pointi 10.
Azam imejichimbia katika nafasi ya pili, pointi moja nyuma ya Simba baada ya jana kuifunga Polisi Morogoro bao 1-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, huku ikiwa na mechi moja mkononi.
Simba ambayo ilishinda michezo minne mfululizo kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Yanga na kurejea kushinda katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Oljoro, ingeweza kuwa imepoteza mechi yake ya kwanza jana kama Coastal iliyoonyesha soka maridadi ingekuwa makini.
Hemedi Morocco, kocha wa Coastal Union, alisema anashukuru kupata pointi moja licha ya timu yake kushindwa kutumia vizuri nafasi nyingi za kufunga ilizotengeneza.
Kocha wa Simba Milovan Cirkovic aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo kuwa Coastal ilicheza vizuri, lakini pia hakufurahishwa na uchezaji wa mshambuliaji wake wa kulipwa kutoka Ghana Daniel Akuffor.
Chipukizi Haruna Chanongo alikaribia kuipatia Simba bao la kuongoza katika dakika ya 12 baada ya shuti lake kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.
Kama Chanongo angefunga, Nsa Job angeweza kuwa ameisawazishia Coastal Union katika dakika ya 39 wakati shuti lake lililopotoka nje akiwa katika nafasi nzuri, kutokana na krosi ya Selemani Kassim ambaye alikuwa amemtoka beki Pascal Ochieng.
Siku ya mshambuliaji wa kati Job ilimalizika vibaya dakika 20 hivi kabla ya filimbi ya mwisho hata hivyo, baada ya kutolewa uwanjani na muamuzi Haji Mbelwa kutokana na kosa la pili la kadi ya njano dhidi ya mabeki wawili wa kati wa Simba.
Katika kosa la kwanza, Job ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba, alimchezea vibaya Shomari Kapombe kabla ya kumfanyia madhambi Ochieng katika kipindi cha pili.  
Timu zilikuwa:
COASTAL: Jackson Chove, Said Sued, Juma Jabu, Mbwana Hamisi, Jamal Machelenga, Jerry Santo, Mohammed Athumani, Selemani Kassim, Green Atupele, Nsa Job, Razak Khalfani (Lameck Dayton dk.45).
SIMBA: Juma Kaseja, Said Nasoro, Amiri Maftah, Pascal Ochieng, Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi (Uhuru Selemani dk.58), Felix Sunzu, Daniel Akuffor (Salum Kinje dk.72), Haruna Chonongo.
Kutoka Morogoro Idda Mushi anaripoti kwamba bao la Azam lilifungwa na Kipre Tchetche katika dakika ya 54 hivyo kuiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kukaa kileleni kama itashinda mechi yake ya mkononi.
Kocha wa Azam Boris Bunjak alielezea kutoridhishwa na ukubwa wa ushindi huo kutokana na Polisi kuwa timu ya mkiani.
John Simkoko, mwalimu wa Polisi alisema makosa madogo madogo ya mchezaji mmoja mmoja na si timu, ndiyo yaliyowagharimu.

Nnyota wa Simba, Yanga washindwa kutambiana 'mchangani'

Onesmo Waziri 'Ticotico' (4) wa Golden Bush akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa wahenga Fc (kulia) huku Abdallah Msheli akiwa tayari kumsaidia

Katina George (14) wa Golden Bush akijaribu kufunga bao mbele ya msitu wa mabeki wa Wahenga Fc katika pambano lao lililochezwa jana Sinza, Dar es Salaam.

NYOTA wa zamani wa klabu za Simba na Yanga jana walishindwa kutambiana baada ya timu walizokuwa wakizichezea za Golden Bush na Wahenga Fc kutoshana nguvu ya kutoka sare ya 1-1 katika pambano la kirafiki.
Wazir Mahadhi, Abdul Ntiro, Ally Yusuf  'Tigana', Abdallah Msheli na Steven Marashi walioichezea Golden Bush ya Mabibo walishindwa kuwazidi ujanja wenzao Mengi Matunda na Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' wa Wahenga ya Sinza katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa TP, Sinza.
Nyota hao walionyesha bado wamo katika usakataji soka kwa jinsi walivyokuwa wakikimbiza dimbani ili kuzisaidia timu zao, lakini mpaka wakati wa mapumziko Wahenga ndio waliokuwa wakiongoza kwa bao 1-0.
Bao lao lilifungwa na Mohammed Ibrahim katika dakika ya 38 baada ya kufanikiwa kuihadaa ngome ya Golden Bush iliyokuwa chini ya Msheli na kumchambua kipa Steven Marashi kwa shuti la karibu.
Kipindi cha pili Golden Bush chini ya nahodha wake Onesmo Wazir 'Ticotico', iliingia kwa kasi baada ya kufanya mabadiliko kadhaa na kufanikiwa kurejesha bao hilo katika dakika ya 64 kupitia Dau 'Messi' aliyemegewa pande zuri Ally Yusuf  'Tigana'.
Licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya kosa kosa nyingi, mpaka kipyenga kilichokuwa kikipulizwa na Ally Mayay Tembele kilipolia matokeo yalikuwa yamesalia kama awali kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Mwisho

Waliovamia maeneo ya shule Ilala kukiona

Afisa Mipango Miji wa Ilala, Paul Mbembela akisisitiza jambo alipozungumza na wakazi za Kitunda

Baadhi ya watu waliohudhuria mkutano huo

Mmoja wa wakazi wa Kitunda akiuliza swali ili apate ufafanuzi juu ya hatma ya makazi yao katika eneo wanaloishi
WAKAZI wote waliovamia na kujenga ndani ya maeneo ya shule wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam wametahadharishwa kuanza kuondoka wenyewe kabla ya kuchukuliwa hatua za kuondolewa kwa lazima katika maeneo hayo.
Aidha serikali na Manispaa hiyo ya Ilala imeweka bayana kwamba haitakuwa na huruma wala kuwaonea haya wavamizi wa maeneo hayo ya shuleni wakati wa zoezi la kuwaondoa kwa lazima.
Afisa Mipango Miji wa Ilala, Paul Mbembela, ndiye aliyeyasema hayo juzi katika mkutano wa pamoja kati ya ofisi yake na wakazi wa Kitunda, nje kidogo ya Dar es Salaam.
Mbembela alisema Manispaa haitakuwa na huruma na wale wote waliovamia na kujenga ndani ya maeneo ya shule kwa madai waliofanya hivyo wamevunja sheria na hawapaswi kuchekewa.
"Tutakuwa wakali kwa wale wote waliovamia na kujenga katika maeneo ya shule, kuchekea jambo hilo ni kutaka kuwafanya vijana na watoto wete wawe mbumbumbu kwa kushindwa kusoma katika mazingira mazuri," alisema.
Aliongeza kuwa, wananchi wote wanaojitambua kuwa wamefanya hivyo waanze mapema kuchukua uamuzi wa kuondoka wenyewe kwa hiari katika maeneo hayto kabla ya Manispaa ya Ilala haijaenda kuwatoa kwa nguvu.
Afisa huyo, alisema kumekuwa na desturi ya watu kuvamia maeneo ya shule ya kuweka makazi au sehemu za biashara na kusababisha wanafunzi kushindwa kusoma kwa utulivu, kitu ambacho Manispaa yao haipo tayari kuvumilia.
Alisema wananchi wanapaswa kutambua kuwa shule ni moja ya vitu muhimu vinavyopaswa kutochezewa kwani ndiko kunakozalisha viongozi na wataalam kwa baadaye wa taifa hivyo kila mmoja ana jukumu la kuzilinda shule.

Mwisho

Wakazi Kitunda wahakikishiwa makazi ya kudumu mradi wa viwanda



Afisa Mipango Miji wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela akifafanua jambo katika mkutano wake na wakazi wa Kitunda waliojenga makazi yao ndani ya mradi wa viwanda uliotengwa na serikali miaka kadhaa iliyopita

Prisca Bassu mmoja wa wakazi wa Kitunda akiuliza swali katika mkutano huo

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni B, Novatus Nyiratu akifafanua jambo katika mkutano huo wa jana

Mkazi mwingine wa eneo la Kitunda akiuliza swali

Sehemu ya umma uliohudhuria mkutano huo wa jana kujua mustakabali wa waliojenga ndani ya mradi wa viwanda

Nataka kujua tusiokuwa na leseni za makazi inajuwaje hatma yetu? Ndivyo mmoja wa wakazi hao alihoji katika mkutano huo

Ibrahim Ismail naye alisimama na kuuliza swali

Hata kinamama nasi tumo kwa maswali

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kitunda Kati, Seleman Abdallah Mtama akieleza jambo kabla ya kuufunga mkutano huo







UONGOZI wa Manispaa ya Ilala, umewatoa hofu na kuwahakikishia wakazi wa eneo la Kitunda, waliojenga na kuweka makazi ndani ya eneo lililotengwa kwa ajili ya mradi wa viwanda kwamba kamwe hawataondolewa.
Pia uongozi huo umewahakikishia wakazi hao kuwa maeneo yao yatapimwa upya na kumilikishwa ardhi ili yawe makazi yao ya kudumu mara taratibu za kubadilisha matumizi ya eneo hilo zilizoanza zitakapokamilika.
Akizungumza na wakazi hao katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa serikali za mitaa ya Kipunguni B na Kitunda Kati, uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kipunguni, Afisa Mipango Miji Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela alisema wakazi hao hawapaswi kuwa na hofu.
Mbembela alisema licha ya kwamba wakazi wa eneo hilo wapo ndani ya ardhi iliyotengwa kwa miaka mingi na serikali kwa ajili ya mradi wa viwanda, bado hawana hofu kwa vile unafanyika mchakato wa kubadilishwa matumizi yake.
Alisema katika mabadiliko hayo ya matumizi, wakazi waliojenga na kumiliki viwanja katika eneo hilo watafanyiwa utaratibu wa kupimwa maeneo yao na kisha kumilikishwa upya kihalali na mradi huo wa viwanda utahamishiwa maeneo mengine ya viwanja vya serikali vilivyopimwa tayari.
Afisa huyo aliyataja baadhi ya maeneo ambayo mradi huo unaweza kuhamia ni pamoja na Buyuni, Chanika na kwingineko katika manispaa ya Ilala ambayo tayari yameshapimwa na kutengwa.
Aliwasisitiza wakazi hao waliowatuma viongozi wa serikali zao za mitaa katika ofisi za manispaa kuhakikisha wanaipa ushirikiano kamati hiyo katika zoezi la kuwatambua wamiliki halali wa sasa waliopo katika eneo hilo ili kurahisisha mchakato wa kuyapima na kuwamilikisha upya.
Kabla ya ufafanuzi huo wananchi wa maeneo hayo kupitia serikali zao za mitaa walikuwa na hofu kubwa ya kubomolewa na kupoteza mali zao katika eneo hilo baada ya kubainika eneo hilo lilitengwa kwa mradi wa viwanda.
Baadhi ya wananchi katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kitunda Kati, Seleman Mtama na ile ya Kipunguni B, Novatus Nyiratu walitaka kujua hatma yao iwapo watatimuliwa katika eneo  hilo.
Miongoni mwa wakazi hao, Ibrahim Ismail, Prisca Bassu walitaka kufahamu iwapo wananchi ambao hawana hati au leseni ya makazi katika eneo hilo hatma yao itakuwaje na kuelezwa watasaidiwa  kumilikishwa bila ya tatizo mradi wahakikiwe na kamati yao.