STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, July 7, 2013

Wamasai wambaka mke wa mwenzao, ana miaka 15 tu!

Wamasai wakionyeshana umahiri wa kucheza ngoma

WATU wawili wenye asili ya kabila la Kimasai wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kwa tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 15 eneo la Goba, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Elisoloi Leid (17) na Jackson James (12), wote wakazi wa Goba jijini Dar es Salaam ambao wanatuhumiwa kumbaka mke wa mmasai mwenzao.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Wamasai hao walifanya kitendo hicho Jumatano wiki hii majira ya asubuhi, muda mfupi baada ya mwenye mke kuondoka kwenda kwenye shughuli zake.
Mmoja wa mashuhuda hao, John Isack alisema kuwa, wamasai hao walikutwa wakimbaka binti huyo wakati mafundi ujenzi walipofika asubuhi kuchukua vifaa vya ujenzi kwenye nyumba wanayoishi.
Alisema kuwa mafundi hao walikuta mlango wa nyumba umefungwa na walipogonga bila kufunguliwa walisikia sauti ya msichana ndani ikilia. Ndipo mmoja wa mafundi hao alipopiga teke mlango na kuwakuta wamasai hao wakimbaka binti huyo.
Kufuatia tukio hilo, baadhi ya wananchi eneo hilo walijitokeza na kuwazingira kwa kuwaweka chini ya ulinzi, huku wengine wakiwa wameshika silaha mbalimbali za jadi kuwatishia wasikimbie mpaka hapo polisi watakapokuja kuwachukua.
Wamasai hao walishikiliwa na wananchi hao kwa muda wa nusu saa na baadaye pikipiki mbili zilikodiwa ambapo moja ilimbeba binti huyo na nyingine watuhumiwa na kupelekwa kituo cha polisi cha Kawe kwa hatua zaidi.
Shuhuda mwingine Amina Mohamed, alisema kuwa unyama aliofanyiwa binti huyo umetokea siku chache baada ya kuja jijini Dar es Salaam kuishi na mume wake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja mume wa binti huyo kwa jina moja la Saaya.
Kamanda Wambura alisema Saaya aliwaleta watuhumiwa hao kutoka umasaini kwa lengo la kuwatafutia kazi za ulinzi. Alisema siku ya tukio, aliondoka asubuhi na kuwaacha wakiwa na mke wake, ndipo walipombaka. Kamanda alisema Saaya na mke wake waliondoka siku ya pili yake baada ya kutoa maelezo polisi kuelekea kijijini kwao.
Wambura alisema wanaendelea kuwashikilia wamasai hao kwa uchunguzi zaidi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
CHANZO: NIPASHE

Nagy Kaboyoka kugombea tena Same Mashariki

Nagy Kaboyoka

LICHA ya kugaragazwa mara mbili na mpinzani wake ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA, Naghenjwa 'Nagy' Kaboyoka, amesema hajakata tamaa na badala yake anajipanga kuwania tena katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
Nagy aliangushwa na Kilango katika uchaguzi wa ndani wa CCM mwaka 2005 wakati wakiwania uteuzi wa jimbo hilo kupitia CCM kabla ya mwaka 2010 kuhamia CHADEMA na kuchuana tena na kuangushwa katika uchaguzi uliodaiwa ulitawaliwa na malalamiko makubwa ya uchakachuaji wa kura.
Mwanamama huyo amesema pamoja na kufanywa mtimanyongo katika masuala ya kisiasa hajakata tamaa kwani anajipanga kushiriki uchaguzi ujao akiamini bahati itakuwa yake kutokana na ukweli anakubalika na wakazi wa jimbo hilo licha ya kushindwa kwenye uchaguzi uliopita.
Nagy alisema changamoto alizokutana nazo katika chaguzi mbili zilizopita za 2005 na 2010 imemchochea na kumpa nguvu zaidi ya kuwapigania wakazi wa jimbo hilo ambao, licha ya ahadi lukuki toka kwa chama tawala mambo bado yapo vile vile.
"Sijakata tamaa na harakati zangu za kuwatumikia wananchi, changamoto nilizokutana nazo zimezidi kunipa nguvu na kiu ya kujikita zaidi katika siasa, ili kuja kuwatumikia wananchi na hata kama sintapata bado nitaendelea kuwasaidia wananchi wenzangu kama ninavyofanya sasa kupitia asasi yangu ya WOYEGE," alisema.
Kuhusu uchaguzi uliopita, Mwanamama huyo alisema hataki kusema lolote kwani ataonekana anaendelea kulalamika, lakini wakazi wa jimbo wanajua kitu gani kilifanyika na anao,mba uzima na afya ifike 2015.
"Mimi unajua siyo mtu wa maneno, mie ni mtu wa vitendo ndiyo maana sitaki kuzungumzia kilichotokea kwenye uchaguzi uliopita kila mtu anafahamu kilichofanyika, najipanga kwa uchaguzi ujao panapo majaliwa kama chama changu kitanipendekeza tena," alisema Nagy.
Aidha aliongeza kuwa, harakati zake za kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo kupitia asasi yake haina maana ni mipango ya uchaguzi ujao, bali amekuwa akifanya hivyo hata alipokuwa akifanya kazi Ubalozi wa Denmark akiamini ana wajibu wa kuwatumikia wananchi hata nje ya masuala ya kisiasa.

Azam Academy yaanza kwa kishindo michuano ya Rolling Stone

Azam Academy ilipokuwa ikijaindaa na michuano hiyo ya Rolling Stone
TIMU ya soka ya vijana ya Azam, Azam Academy, imeanza kwa kishindo michuano ya kimataifa ya vijana Afrika Mashariki na Kati, Rolling Stone baada ya kuikwanyua Eagle Rangers ya Tanga kwa mabao 3-0.
Azam ilijipatia mabao yake kupitia kwa wakali wake, Mange Chagula, Kevin Friday na Erick Haule na kuwaacha hoi vijana wenzao ambao wa Eagles iliyowahi kuchezewa na nyota kadhaa akiwamo Mchezaji Bora wa michuano ya Kombe la Taifa 2009, Salum Aziz Gillah aliyewahi kung'ara na Simba na Coastal Union.

Nani wa Man United kutimkia As Roma

Nani
MSHAMBULIAJI wa pembeni wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester United, Louis Nani anatarajiwa kujiunga na klabu ya AS Roma, wakala wa winga huyo kutoka Ureno, Jorge Mendes amefichua.
Wakala huyo alisema Nani mwenye miaka 26 yu njiani kuondoka Old Trafford na kujiunga na timu hio ya Italia, licha ya kwamba pia anahusisha na kunyemelewa na klabu za Galatarasay, Juventus, Arsenal na Real Madrid.
"Nani ni mchezaji mzuri na dunia yote inafahamu hili" alisema Mendes kabla ya kuongeza kuwa "Atajiunga na As Roma, kwa isiwe wakati Serai A ni bonge la Ligi bora duniani na jiji la Roma linavutia na kupendeza!" alisema Mendes.
Alisema alikuwa katika mipango ya kuonana na klabu ya United kwa lengo la kuweka mambo sawa ili Nani atimke zake katika klabu hiyo aliyobakisha mkataba wa mwaka mmoja tangu alipotua OT kwa kitita cha pauni Milioni 25.5 mwaka 2007.
Winga huyo amekuwa hana uhakika wa namba katika timu hiyo kwa misimu miwili iliyopita na kwamba aliwahi kuwekwa sokoni na kuelekea kutua Galatasaray kabla ya klabu hiyo ya Uturuki kushindwa kulipa kitita cha Pauni Milioni 8.5 kilichokuwa kikiitaka United.

Watu watano wafa machimbo ya Mererani

Picha hii haihusiani na tukio la usiku wa jana, ila ilipigwa wakati serikali ilipositisha uchimbaji Mererani baada ya kutokea maafa ya watu zaidi ya 75 kudaiwa kufariki katika machimbo hayo.
HABARI zilizopatikana kutoka Arusha, zinasema kuwa watu watano wamefariki katika machimbo ya madini ya Tanzanites, Mererani Arusha baada ya kuangukiwa na gema wakati wakiendelea kuchimba madini hayo.
Taarifa hizo zinasema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika mgodi unaomilikiwa na mfanyabiashara mmoja aliyetajwa kwa jina la Onesmo, ambapo inaelezwa walianza kufa wachimbaji wawili walioangukiwa na gema baada ya kulipua mwamba.
Baada ya watu hao kuangukiwa na gema hilo lililowafunika kifusi kilichoambana na majabari, wenzao watatu waliamua kujaribu kuwaokoa na wao kujikuta wakiporomokewa na gema jingine na kupoteza uhai wao na miili ya watu hao ilifanikiwa kuopolewa na kupelekwa hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Miongoni mwa waliofariki ni wawili tu ndiyo waliobahjatika kutambuliwa mpaka sasa nao ni Ndianka na Ndekira na wengine juhudi zinaendelea kutokana na ukweli tukio lilitokea usiku.
Mungu azilaze roho za marehemu hali pema na awapo subira ndugu, jamaa na familia kwa ujumla kutokana na msiba huo uliowapata ndugu zao.
 

Giza laghubika kuhusu hali ya Mzee Mandela

Full statement – Clarification on the health of Nelson Mandela
Mzee Nelson Mandela
IKIWA takribani mwezi mmoja sasa tangu Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, akimbizwe hospitalini akiwa mahututi kutokana na ugonjwa wa mapafu, taarifa zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa madaktari bingwa wanaomtibu, wamegundua ugonjwa mwingine mwilini mwake. 
Nje ya Hospitali ya Medi Clinic iliyoko Pretoria, ambako waandishi wa habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari duniani wamefurika wakifuatilia mwenendo wa afya ya Mandela, juzi na jana, zilivuja taarifa kuwa Mandela ambaye anaishi kwa msaada wa mashine maalumu inayomwezesha kupumua, madaktari wake wamebaini kuwa figo zake zimeshindwa kufanya kazi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, madaktari bingwa wanaomtibu wameanza kupambana na ugonjwa huo kwa kumuwekea mashine ya kusaidia figo zake kufanya kazi na kwamba wanaang

alia uwezekano wa kuzibadilisha bila kusababisha madhara mengine katika mwili wake ambao sasa unalindwa dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Tayari Shirika la Utangazaji CNN, ambalo lina timu ya waandishi wake nje ya Hospitali ya Medi Clinic, limekwishatangaza taarifa za kubainika kwa ugonjwa huo na kwamba madaktari wamemuwekea kipimo kinachowezesha figo zake kufanya kazi.

Kabla ya kupatikana kwa taarifa hizo, ilielezwa kuwa madaktari wake walibaini hawawezi kuyatibu mapafu ya Mandela kutokana na madhara makubwa yaliyonayo na badala yake wamemuweka chini ya uangalizi wao maalumu wakihakikisha kuwa hapatwi na magonjwa nyemelezi yanayoweza kuhatarisha uhai wake.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumezidisha wasiwasi wa mwenendo wa afya ya Mandela kwa waandishi wa habari walioko Hospitali ya Medi Clinic, ambapo wengi wamekuwa wakijitahidi kuzifikia mamlaka zinazohusika ili kutoa taarifa rasmi pasipo mafanikio kutokana na usiri uliopo.

Wakati zikipatikana taarifa za kugunduliwa kwa tatizo jipya kwa Mandela, baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, jana vilimkariri mmoja wa marafiki zake wa karibu kwa muda mrefu, Denis Goldberg, akieleza kuwa mashine zinazomsaidia Mandela kupumua haziwezi kuondolewa.

Goldberg alikaririwa akieleza kuwa alipewa taarifa za uwezekano wa kuondolewa kwa mashine hizo ili kumwezesha Mandela kupumzika, lakini madaktari wake walikataa kuziondoa kwa kueleza wanaweza kuziondoa iwapo watabaini sehemu muhimu za mwili wake hazifanyi kazi tena.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Afrika Kusini, Goldberg, aliyekuwa mpinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi, ambaye alimtembelea Mandela hospitalini Jumatatu iliyopita, alisema suala hilo lilijadiliwa na kufikia tamati kuwa mashine hizo hazitaondolewa.

Kauli hii ya Goldberg inapingana na ile iliyotolewa mapema wiki hii, ikikariri nyaraka zilizotolewa mahakamani na Makaziwe Mandela, mtoto mkubwa wa kike wa Mandela, ambazo pamoja na mambo mengine, zilieleza kuwa familia ilishauriwa na madaktari ikubali mashine hizo ziondolewe ili aweze kupumzika badala ya kuzidi kumuongezea maumivu.

Familia na ugomvi wa utajiri wake

Wakati Mandela akiwa mahututi hospitalini, familia yake imekuwa katika vita ya kugombea mahali panapostahili kuwa eneo maalumu la kuzika miili ya wanafamilia hiyo, vita ambayo inatafasiriwa na wengi nchini hapa kuwa kiini chake ni kutaka kurithi utajiri mkubwa alionao.

Hilo limethibitishwa pia na mjukuu wake mkubwa wa kiume, Mandla Mandela, ambaye katika mkutano wake wa hivi karibuni na waandishi wa habari baada ya kushindwa kesi ya ugomvi wa makaburi, alitaja utajiri wa Mandela kuwa moja ya sababu za ugomvi huo.

Hata hivyo, Mandla, kijana tajiri na chifu wa Mzove, ambaye alifunguliwa kesi na shangazi yake, Makaziwe na kuungwa mkono na wanafamilia 15, wakimtuhumu kuvamia eneo la makaburi la familia nyakati za usiku na kuiba mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela, hatua ambayo inadaiwa ililenga kujihalalishia udhibiti wa mazishi ya rais mstaafu huyo.

Wakati kesi hiyo ikiendelea katika Mahakama Kuu ya Mthatha ya Jimbo la Eastern Cape, Mandla alikuwa akishutumiwa kusababisha mgogoro wa kifamilia kwa lengo la kutaka kumzika Mandela kwenye makazi yake ya Mzove, baada ya kufa ili alitumie kaburi lake kuchuma fedha kutokana na biashara ya utalii ya kuzuru kaburi hilo.

Madai mengine yaliyoibuka dhidi ya Mandla yalimhusisha na kuuza haki ya kutangaza mazishi ya Mandela kwa kituo kimoja cha utangazaji cha kimataifa na kuvuna mamilioni ya Rand.

Kwa upande mwingine, Makaziwe naye amedaiwa kuingia katika vita na mpwa wake, Mandla kwa sababu ya kutaka kurithi utajiri wa baba yake atakapofariki.

Makaziwe, mwenye umri wa miaka 60 sasa, kama ilivyo kwa Mandla, naye anadaiwa kuwa na utajiri mkubwa, huku akiwa anaishi nje ya Afrika Kusini, lakini hayuko tayari kuona mali za baba yake zikiangukia mikononi mwa mjukuu.

Mandela anatajwa kuwa na fedha nyingi katika mfuko wake wa Mandela Foundation pamoja na sehemu nyingine ambazo atakayezirithi atakuwa bilionea.

Sherehe ya kutimiza miaka 95

Jijini Johannesburg na katika mji mkuu wa Pretoria, wengi wanaamini kuwa Mandela hatakufa mpaka atakapotimiza miaka 95, ifikapo Julai 18 mwaka huu.

Makundi ya Waafrika Kusini ambayo yamekuwa yakikusanyika sehemu mbali mbali za nchi kumuombea afya njema na hata mmoja mmoja waliozungumza na gazeti hili, walisema wanamuomba Mungu amjalie kufikisha umri wa miaka 95 akiwa hai.

Taarifa nyingine zilizokusanywa na gazeti hili zinaonyesha kuwa Serikali ya Pretoria ya Rais Zuma inafanya kila linalowezekana kuhakikisha Mandela haagi duniani kabla ya kusherehekea umri wa miaka 95.

Inaelezwa kuwa sherehe hizo zitakuwa kubwa kwa sababu Mandela atakuwa ameandika historia ya kuwa mtu mweusi aliyeishi miaka mingi zaidi katika karne hii, na kwamba, baada ya kutimiza umri huo, hata kama Mungu ataamua kumchukua, uwezekano wa kutokea kwa vurugu utakuwa mdogo kwa sababu kila mmoja atakuwa na kumbukumbu ya sherehe ya miaka 95 ya Mandela na kwamba wengi watakuwa wanamuombea. CHANZO MTANZANIA

Wawili wafa, 182 wanusurika ajali ya ndege ya Asiana Airlines







WATU wawili wamefariki na wengine zaidi ya 180 kunusurika kufa katika ajali iliyohusisha ndege aina ya Boeing 777 ya kampuni ya Asiana Airlines, iliyoanguka ardhini katika kiwanja cha Kimataifa ccha Ndege cha San Francisco, Marekani.
Kwa mujibu wa CNN, ndege hiyo ilianguka na kulipuka moto ndani kwa ndani na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine 182 kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
Taarifa zaidi zinasema miongoni mwa abiria waliokuwa katika ndege hiyo ni wanafunzi wa sekondari 26 kutoka China ambao walikuwa wameenda katika mji huo kwa ajili ya kambi ya mapumziko kipindi hiki cha majira ya joto.

Kaseba aachia Bongo Mafia

BINGWA wa zamani wa dunia wa Kick Boxing Japhet Kaseba 'Champion' ameingia katika ulingo wa fani ya filamu baada ya kuachia mtaani filamu ya 'action' iitwayo 'Bongo Mafia' aliyoigiza na wasanii kadhaa wakongwe wa fani hiyo.

Filamu hiyo iliyorekodiwa na kukamilika hivi karibuni ipo mtaani kwa sasa baada ya kuachiwa wiki iliyopita ili mashabiki wa fani hiyo wapate burudani ambayo wamekuwa wakiikosa katika filamu za mapigano.
Picha hiyo ni mfululizo za filamu nyingine zilizopo njiani ambapo aliidokeza MICHARAZO kuwa 'Daddy Sin' kazi yake nyingine ipo katika maandalizi ya kutoka baada ya 'Bongo Mafia'.
Katika filamu hiyo ya sasa Kaseba kaigiza na wakali kama Dotnata Poshi, Ahmed Khalfan 'Kelvin', Abdallah Mkumbira 'Muhogo Mchungu', Pendo Njau, Rongers 'Master Shivo'  na wakali wengine.