Picha hii haihusiani na tukio la usiku wa jana, ila ilipigwa wakati serikali ilipositisha uchimbaji Mererani baada ya kutokea maafa ya watu zaidi ya 75 kudaiwa kufariki katika machimbo hayo. |
HABARI zilizopatikana kutoka Arusha, zinasema kuwa watu watano wamefariki katika machimbo ya madini ya Tanzanites, Mererani Arusha baada ya kuangukiwa na gema wakati wakiendelea kuchimba madini hayo.
Taarifa hizo zinasema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika mgodi unaomilikiwa na mfanyabiashara mmoja aliyetajwa kwa jina la Onesmo, ambapo inaelezwa walianza kufa wachimbaji wawili walioangukiwa na gema baada ya kulipua mwamba.
Baada ya watu hao kuangukiwa na gema hilo lililowafunika kifusi kilichoambana na majabari, wenzao watatu waliamua kujaribu kuwaokoa na wao kujikuta wakiporomokewa na gema jingine na kupoteza uhai wao
na miili ya watu hao ilifanikiwa kuopolewa na kupelekwa hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Miongoni mwa waliofariki ni wawili tu ndiyo waliobahjatika kutambuliwa mpaka sasa nao ni Ndianka na Ndekira na wengine juhudi zinaendelea kutokana na ukweli tukio lilitokea usiku.
Mungu azilaze roho za marehemu hali pema na awapo subira ndugu, jamaa na familia kwa ujumla kutokana na msiba huo uliowapata ndugu zao.
No comments:
Post a Comment