STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 3, 2015

New Alert! Polisi yawanasa Panya Road 36

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRFCKTrOSS6jQnrp-2w6J_KAENIsfm6tqqgJBEGvkXRlu4ZT6sIiNADLj1Mp7001DbrJDkTOTAD64AZsWES5iZkPYt7wtn1J0jgKfMpgrWCV7iFj1Z-88iz0YGNxnvpUE5rzYqkilwbLX8/s1600/4.jpg
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Suleiman Kova
JESHI la Polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi na kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.
  Kufuatia tukio hilo waandishi wa habari wamezunguka maeneo mbalimbali ya jiji yaliyodaiwa kukumbwa na tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo ya magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi  na taarifa kusambaa maeneo mengine.
Katika maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha huku wengine wakishauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe mbili chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.
  via..ITV

Kocha afichua Ronaldo kurudi Manchester Utd

http://img2.timeinc.net/people/i/2012/specials/sma/athletes/cristiano-ronaldo-1-435.jpg
Ronaldo
KOCHA Msaidizi wa zamani wa klabu ya Manchester United, Mike Phelan amesema kuwa nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anaweza kusikiliza kama klabu hiyo ikijaribu kumnunua tena.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno ametengeneza mahusiano mazuri na mashabiki wa klabu hiyo katika kipindi alichoichezea kabla ya kujiunga na Madrid kwa kitita cha paundi milioni 80.
Phelan anaamini kuwa Ronaldo anaweza kurejea United kwani alifurahia katika kipindi chote alichokuwepo hapo kwasababu ndio maisha yake ya soka yalipoanza kung’ara.
Pamoja na hayo Phelan anadhani kwasasa itakuwa mapema mno kwa Ronaldo kurejea Old Trafford hususani kutokana na mafanikio aliyopata na hadhani kama klabu hiyo inaweza kumruhusu.

Equatorial Guinea kumpa ulaji Becker

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/2/2e/Esteban_Becker_Churukian.jpg/150px-Esteban_Becker_Churukian.jpg
Kocha Becker
WENYEJI wa michuano ya Mataifa ya Afrika, AFCON inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Januari 15, Guinea ya Ikweta wanajiandaa kumpa ulaji kocha Estaban Becker kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na Andoni Goikoetxea waliyemtema.
Chama cha soka nchini humo, kiliamua kutomuongeza mkataba kocha huyo Goikoetxea uliomalizika Desemba 31 mwaka jana.
Rais wa chama hicho Andres Jorge Mbomio amedai kuwa wameamua kutomuongeza mkataba kocha huyo baada ya kukiuka masharti ya mkataba wa kwanza kwa kushindwa kusafiri na kikosi cha timu kwenda Ureno Desemba 16.
Guinea Ikweta iliyookoa jahazi la michauno huyo kwa kuipokea Morocco waliogoma kwa dai la tishio la ugonjwa wa Ebola, ina wiki mbili kuandaa kikosi chao kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambapo wao watafungua dimba na Congo Brazzaville Januari 17 mwaka huu.

David Moyes amuita Steven Gerrard Real Sociedad

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/fw0doU3LIH0xHkBkFbvYfA--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9ZmlsbDtoPTM3NztpbD1wbGFuZTtweG9mZj01MDtweW9mZj0wO3E9NzU7dz02NzA-/http://media.zenfs.com/en_GB/Sports/Eurosport/1382031-29636997-2560-1440.jpg
David Moyes akipeana mkono na Steven Gerrard
MENEJA wa zamani wa Manchester United, David Moyes amemfungulia milango Steven Gerrard kujiunga na klabu ya Real Sociedad mwishoni mwa msimu huu.
Moyes alikuwa na msimu mbaya wakati akiinoa United msimu wa 2013-2014 hali iliyopelekea kutimuliwa lakini sasa amepewa nafasi nyingine kwa kupewa kibarua cha kuinoa klabu hiyo ya Hispania.
Baada ya Gerrard kutangaza uamuzi wake wa kuondoka Liverpool baada ya mkataba kumalizika, Moyes amempa nafasi ya kufikiria kujiunga na Sociedad ili kupata changamoto mpya.
Moyes mwenye umri wa miaka 51 amesema Gerrard amecheza kwa mafanikio katika klabu yake hiyo na timu ya taifa ya Uingereza hivyo itakuwa ngumu kuziba pengo lake na kama angependa kwenda Hispania kucheza soka anajua kuwa anaweza kumpigia simu.
Naye meneja wa Southampton Ronaldo Koeman pia amedai kuwa katika kikosi chake kutakuwa na nafasi ya Gerrard kama atataka kujiunga nao.

Arsene Wenger awakata maini wanaotamani aondoke Arsenal

http://www.arsenal.com/assets/_files/scaled/510x250/aug_10/gun__1281108157_20100806_wenger_membersday1.jpg
Kocha Arsene Wenger
KOCHA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewakata maini wanaodhani fujo wanazomfanyia zinaweza kumfanya aiteme timu hiyo.
Wenger amesisitiza kuwa asingeweza kuondoka katika timu hiyo hata kama wangeshindwa kunyakuwa Kombe la FA msimu uliopita. 
Arsenal walimaliza ukame wao wa vikombe wa miaka tisa kwa kuifunga Hull City kwa mabao 3-2 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa Wembley Mei mwaka jana. 
Akiulizwa na wanahabari kama angeondoka kwa kushindwa kunyakuwa Kombe la FA, Wenger amesema isingewezekana kwani hakuona umuhimu huo. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa katika mechi 1000 alizoisimamia Arsenal ameshinda 600 hiyo inamaanisha ana wastani wa ushindi kwa asilimia 60 hivyo haoni sababu ya kujiuzulu kwani anafanya kazi yake vyema. 
Wenger amesema anaheshimu mkataba wake na ataendelea kuutumikia mpaka hapo wakati wake utakapofika.

Huyu ndiye Mwanasheria Mkuu Mpya wa Serikali

Mwanasheria Mpya wa Tanzania, George Mcheche Masaju
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 
3 Januari, 2015

Simba yaona mwezi Mapinduzi, Mtibwa yabanwa

Kikosi cha Simba

Hekaheka katika pambano la Mtibwa na JKT (Picha: ZanziNews)
BAO la shuti kali la umbali wa mita 40 lililowekwa kimiani na kiungo Said Ndemla limeiwezesha Simba kufufua matumaini yao katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi mbele ya Mafunzo.
Simba ambao ilitoka kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa katika pambano lao la kwanza ilishuka dimbani ikiwa inaongozwa na kocha wake mpya, Mserbia Goran Kapunovic na ilienda mapumziko ikiwa suluhu dhidi ya timu hiyo ya visiwani Zanzibar.
Katika kipindi cha pili kilikuwa chenye kasi zaidi kwa timu zote na Simba ilipata bao pekee lililofungwa na Ndemla katika dakika ya 54 baada ya kuipokea pasi ya Hassan Kessy na kufumua shuti kali lililomshinda kipa Hashim Haruna na kuwapa faraja mashabiki wa Msimbazi ambao walikuwa hawana raha baada ya timu yao kupokea kipigo cha Mtibwa ikiwa ni siku chache tangu ilale kwenye ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.
Katika pambano jingine la michuano hiyo lililochezwa mapema, Mtibwa Sugar na JKU zilishindwa kutambiana baada ya kwenda sare ya 1-1 huku Mtibwa ikijilaumu kwa kukosa penati iliyopotezwa na Mussa Hassan Mgosi aliyetangulia kuifungia Mtibwa bao kabla ya JKU kurejesha kupitia kwa Amour.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa pambano la mapema litakalowakutanisha mabingwa watetezi KCCA ya Uganda dhidi ya Mtende kisha Yanga kuvaana na  Polisi Zanzibar jioni na usiku kushuhudia Azam ikipepetana na KMKM.

Kagera yashindwa kuzing'oa Yanga, Azam, Coastal yapigwa kidude

http://tplboard.co.tz/assets/uploads/files/ded5f-kagera-sugar1.png
Kagera Sugar walioshindwa kutamba mbele ya Ruvu Shooting
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/HMB_39851.jpg
Coastal Union waliopigwa kudude kimoja na JKT Ruvu
TIMU ya soka ya Kagera Sugar imeshinda kuzipiku Yanga na Azam kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare isiyo na mabao kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi dhidi ya wenyeji wa Ruvu Shooting, huku Coastal Union ikikubali kipigo nyumbani.
Kagera ilikuwa na nafasi ya kuzipiku Yanga na Azam ambazo zipo visiwani Zanzibar zikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi kwani kama ingeshinda mchezo wa leo ingefikisha pointi 16 na kulingana na Mtibwa Sugar na kuziondoa mabingwa hao wenza walio na pointi 14.
Hata hivyo suluhu hiyo imeisaidia timu hiyo kujimarisha kwenye nafasi ya nne ikilingana na Yanga na Azam na kutofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Coastal Union ilikubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani Mkwakwani mbele ya maafande wa JKT Ruvu inayonolewa na kocha Fred Felix Minziro.
Ushindi huo umeifanya Ruvu uliotokana na bao la dakika ya 38 lililofungwa na Samuel Kamuntu umeifanya ikwee hadi nafasi ya sita ikiwa nyuma ya Polisi Moro wanaolingana nao pointi 13 baada ya maafande hao wa Morogoro kupata sare isiyo na magoli na Stand United katika pambano jingine lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri.
Wagosi wa Kaya wenyewe wameporomoka kwa kipigo hicho hadi nafasi ya sita wakiwa na pointi 12 baada ya mechi tisa walizocheza.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa pambano moja tu kati ya wenyeji Prisons Mbeya dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara wanaouguza kipigo cha bao 1-0 ilichopewa katika mechi yao ya wiki iliyopita dhidi ya Mbeya City.