STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 3, 2015

Kagera yashindwa kuzing'oa Yanga, Azam, Coastal yapigwa kidude

http://tplboard.co.tz/assets/uploads/files/ded5f-kagera-sugar1.png
Kagera Sugar walioshindwa kutamba mbele ya Ruvu Shooting
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/HMB_39851.jpg
Coastal Union waliopigwa kudude kimoja na JKT Ruvu
TIMU ya soka ya Kagera Sugar imeshinda kuzipiku Yanga na Azam kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kulazimishwa sare isiyo na mabao kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi dhidi ya wenyeji wa Ruvu Shooting, huku Coastal Union ikikubali kipigo nyumbani.
Kagera ilikuwa na nafasi ya kuzipiku Yanga na Azam ambazo zipo visiwani Zanzibar zikishiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi kwani kama ingeshinda mchezo wa leo ingefikisha pointi 16 na kulingana na Mtibwa Sugar na kuziondoa mabingwa hao wenza walio na pointi 14.
Hata hivyo suluhu hiyo imeisaidia timu hiyo kujimarisha kwenye nafasi ya nne ikilingana na Yanga na Azam na kutofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, Coastal Union ilikubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani Mkwakwani mbele ya maafande wa JKT Ruvu inayonolewa na kocha Fred Felix Minziro.
Ushindi huo umeifanya Ruvu uliotokana na bao la dakika ya 38 lililofungwa na Samuel Kamuntu umeifanya ikwee hadi nafasi ya sita ikiwa nyuma ya Polisi Moro wanaolingana nao pointi 13 baada ya maafande hao wa Morogoro kupata sare isiyo na magoli na Stand United katika pambano jingine lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri.
Wagosi wa Kaya wenyewe wameporomoka kwa kipigo hicho hadi nafasi ya sita wakiwa na pointi 12 baada ya mechi tisa walizocheza.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa pambano moja tu kati ya wenyeji Prisons Mbeya dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara wanaouguza kipigo cha bao 1-0 ilichopewa katika mechi yao ya wiki iliyopita dhidi ya Mbeya City.

No comments:

Post a Comment