STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 2, 2015

News Alert! Polisi Dar wanasa Panya wawili, yatoa hofu wakazi Dar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWuSZq8hYuK9PCN1VrRQiyUvXtvljEAjuMAv3svwJWRxL-3XQwVyxUZlubZ41CcD93C401JPyYVoRTTb30RoQxxjonlkBoNwXZhZUDvLp1oypp_HowlFLw3ixI6eUKsEf9YfcftNzAgLsq/s1600/Kova1(30).jpg
Kamanda Kova
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewaondoa hofu wakazi wa jiji hilo juu ya kuzagaa kwa habari za uvamizi wa kundi la vijana wahuni la Panya Road, ingawa Kamanda wa Polisi Suleima Kova amekiri kutokea tukio hilo na vijana wawili wameshatiwa mbaroni mpaka sasa.
Akihojiwa muda mfupi na kituo cha TBC1, Kamanda Kova alisema kuwa usambazaji wa taarifa juu ya kundi hilo zimekuzwa sana na kuleta hofu kutokana na uvumi uliosambazwa na kuwataka wananchi wasiwe na hofu.
Kamanda Kova alisema jeshi la Polisi limedhibitiwa tangu walipoanzisha fujo zao na wawili walishatiwa mbaroni na sasa wanaendelea kuwataja wenzao ili kuwasaka walioibua taharuki hiyo.
"Uvumi huu wa kutumiana meseji na kutumia mitandao ya kijamii imeleta taharuki na kukuza jambo kinyume na uhalisia, lakini nataka kuwamabia wakazi wa Dar wasiwe na hofu jeshi la Polisi limewadhibiti na vijana wapo kazini kuhakikisha mambo yanaendelea kuwa shwari,'" alisema Kamanda Kova.
Tangu jioni kulikuwa na taarifa za kuwepo kwa matukio ya uporaji na uvamizi uliokuwa ukidaiwa kufanywa na Panya Road, ingawa DC wa KIinondoni, Jordan Rugimbana alifafanua mapema kabla ya Kamnada Kova kumaliza utata hivi punde. akisisitiza kuwa Dar ni shwari na watu walale kwa amani na utulivu kwa kuwa yeye Kamanda na vijana wake wapo kazini na Panya Road au wahalifu wengine hawawezi kuwazidi ujanja.

No comments:

Post a Comment