
Baada ya Diego Costa kuifungia Chelsea bao la kuongoza, timu hiyo ilinyimwa penati na refa Phil Dowd wakati Jan Vertonghen aliposhika mpira katika eneo la hatari, na baadae kuja kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 5-3.
Mourinho alimlaumu mwamuzi huyo kwa kushindwa kutoa penati hiyo kwani ingewapa nafasi nzuri ya kushinda mchezo huo.
Hata hivyo baadhi wachambuzi wa soka wameshindwa kukubaliana na Mourinho wakidai kuwa haikustahili kuwa penati hivyo mwamuzi alikuwa sahihi.
Chelsea ambao walikuwa wakiongoza kwa tofauti ya alama nane katika msimamo wa Ligi Kuu Novemba mwaka jana sasa wako juu ya Manchester City kutokana na mpangilio wa herufi kufuatia kipigo hicho cha jana.
Ligi hiyo ya England itaendelea tena wiki ijayo baada ya wikiendi hii kuwa mapumziko kupisha michuano ya Kombe la FA.
No comments:
Post a Comment