STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 13, 2013

Kilimanjaro Marathon yazinduliwa rasmi, zawadi zaanikwa

Mashindano ya 12 ya Kilimanjaro Marathon yanayotarajiwa kufanyika Moshi Machi 2, 2014 yamezinduliwa jijini Dar es Salaam leo.

Katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Ninayo furaha kutangaza kwamba huu utakuwa mwaka wa 12 kwa mbio za Kilimanjaro Marathon kufanyika chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager.

Kwa mara nyingine, ni fahari kubwa kwa Kilimanjaro Premium Lager kudhamini tukio hili maarufu na lenye msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo ya Tanzania.”

Kavishe alitangaza nyongeza ya asilimia 25 kwenye zawadi za fedha kwa washindi wa mbio za kilometa 42 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, ambapo jumla ya zawadi ya fedha itaongezeka kutoka Tsh milioni 15 hadi Tsh milioni 20, huku washindi wa kwanza, wa pili na wa tatu wanaume kwa wanawake wakipokea jumla ya Tsh milioni nane na kiasi kilichobaki kikigawanywa miongoni mwa washindi wanne hadi wa 10.

Kavishe alisema kwamba ni bahati kubwa kwa Kilimanjaro Premium Lager kudhamini mashindano haya yenye msisimko mkubwa katika kalenda ya michezo nchini Tanzania na kwamba Bia ya Kilimanjaro Premium Lager itatoa zawadi kubwa za fedha kwa wanariadha wakati wengine watabaki wana kumbukumbu isiyofutika ya ukaribu wa hali yajuu.

Ili kuwahamasisha na kuwapa motisha wanariadha wa Tanzania kuongeza viwango vyao na kutumia muda mfupi kumaliza mbio hizo, Kilimanjaro Premium Lager imetenga Shilingi milioni mbili kama bonasi au malipo ya nyongeza kwa wanariadha wa Tanzania watakaovunja rekodi kwenye mashindano hayo.

Zawadi zitakazotolewa kwenye 2014 Kilimanjaro Marathon zimenyumbulishwa kitakwimu kama ifuatavyo hapa chini;

2014 KILI MARATHON PRIZES
2013 KILI MARATHON PRIZES

MALE
FEMALE

MALE
FEMALE
1ST
4,000,000
4,000,000
1ST
3,000,000
3,000,000
2ND
2,000,000
2,000,000
2ND
1,500,000
1,500,000
3RD
1,000,000
1,000,000
3RD
850,000
850,000
4TH
900,000
900,000
4TH
650,000
650,000
5TH
600,000
600,000
5TH
500,000
500,000
6TH
400,000
400,000
6TH
350,000
350,000
7TH
350,000
350,000
7TH
250,000
250,000
8TH
300,000
300,000
8TH
200,000
200,000
9TH
250,000
250,000
9TH
150,000
150,000
10TH
200,000
200,000
10TH
100,000
100,000






SUB TOTAL
10,000,000
10,000,000
SUB TOTAL
7,550,000
7,550,000






GRAND TOTAL

20,000,000
GRAND TOTAL

15,100,000

Kavishe alisema anatarajia kwamba zawadi hizo za fedha zitawavutia wanariadha mashuhuri na kuwapa moyo wengine kuvunja rekodi za mashindano hayo.

Aliongeza kwamba Kilimanjaro Marathon imepiga hatua kutoka tukio la mkoa hadi kuwa mashindano makubwa ya kimataifa. “Tunatambuliwa na IAAF na Chama cha Kimataifa cha Mbio za masafa Marefu. Licha ya mafanikio haya, tunaendelea kujitahidi kuboresha mbio hizi mwaka hadi mwaka,” alisemaKavishe.

Tunashukuru kwa jinsi walivyoungwa mkono na Wizara ya Michezo na mamlaka za Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Riadha Tanzania, Chama cha Mbio za Ridhaa Kilimanjaro, pamoja na wadhamini wenzawao ambao ni Vodacom (5km Fun Run), GAPCO, Simba Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, FNB Bank, UNFPA, TanzaniteOne na Kilimanjaro Water kwa kusaidia kuikuza Kilimanjaro Marathon kuwa moja ya mashindano makubwa zaidi ya mbio za masafa marefu barani Afrika.

Future Young Taifa Stars yainyoa Stars 1-0

Mshambulia wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (kulia) akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars, Kabanda katika mchezo kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Kiungo wa Taifa Stars, Athuma Idd "Chuji" akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars,Paul Nonga.
Beki wa Stars Erasto Nyoni (kushoto), akichuana na mshambuliaji wa Future Young Taifa Stars, Simon Msuva.
Erasto Nyoni akipimana ubavu na Simon Msuva.
Chuji akimtoka Paul Nonga.
Uniwezi bwana mdogo......Chuji akichuana na Paul Nonga wa Future Young Taifa Stars.
Makocha wakijadiliana jambo wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wakishuhudia mechi hiyo kupitia katika jengo la Machinga Complex.
Msuva akitoka baada ya kuumia.
Moja ya hekaheka.

Mwili wa Dk Mvungi kuletwa Ijumaa kuzikwa Jumatatu

Dk Mvungi alipokuwa akisafishwa kwenda Afrika kusini kwa matibabu zaidi
MWILI wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, Dk Sengondo Mvungi (61) unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa tayari kwa ajili ya mazishi yake, huku Chama cha NCCR-Mageuzi kikiwataka watanzania kuwa na utulivu kufuatia kifo cha kiongozi wao huyo muhimu.
Akitoa taarifa ya ratiba ya mazishi ya Dk Mvungi, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia alisema wamesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo ambaye alikuwa kiungo muhimu.
Mbatia alisema Dk. Mvungi ameacha pengo kubwa ndani ya chama ambalo halitazibika kutokana na kukitumikia kwa moyo mmoja.
Alisema baada kukaa kama chama, familia na serikali, walikubalina na kwamba mwili wake uwasili Novemba 15 mwaka huu toka Afrika Kusini na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo ambako utahifadhiwa.
Novemba 16 mwaka huu, mwili huo utapelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam saa 3:00 asubuhi hadi 6:00 mchana kwa ajili ya ibada ya kumwombea.
Mbatia alisema baada ya ibada, mwili huo utapelekwa katika Viwanja vya Karimjee kwa ajili ya watu mbalimbali kutoa heshima ya mwisho kuanzia saa 6:30 mchana hadi 10: 00 jioni.
Baada ya hatua hiyo, mwili huo utapelekwa nyumbani kwake Kibamba kupumzishwa ili siku ya Jumapili  Novemba 17  uweze kusafirishwa kijijini kwao Kisangara – Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili maziko yatakayofanyika  Novemba 18 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salma jana walikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika nyumbani kwa marehemu Dk.  Mvungi kwa ajili ya kuhani.
Rais Kikwete walifika nyumbani hapo saa 6:00 mchana ambapo alipata fursa ya kumpa pole mke wa marehemu, Anna Mvungi, wanafamilia na wananchi waliofika katika msiba huo.
Pia viongozi kadhaa wa serikali, siasa, wanasheria na wananchi wengine walifika nyumbani hapo kuomboleza msiba huo.
Salamu za rambi rambi zimekuwa zikitolewa na watu mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa na asasi za kijamii kufuatia kifo cha Dk Mvungi aliyevamiwa na kucharangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa majambazi Novemba 3 nyumbani kwao Kibamba Msakuzi.
Dk Mvungi alifariki mchana wa jana akipatiwa matibabu nchini Afriuka Kusini alkikopelekwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI).