http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AGjkimIAAAiSUdrDdwAAAGIpNMM&midoffset=2_0_0_1_971450&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimkabishi nahodha wa Staki Shari taji la ubingwa wa michuano ya Bonnah Cup, huku Diwani wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa akishuhudia katikati.
MKUU wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amewasisitiza wadau mbali mbali kuwekeza katika mpira wa miguu kwani hutoa ajira nyingi kwa vijana na kuwafanya wajipatie kipato.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kufunga mashindano ya Bonnah Cup yaliyoandaliwa na diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Mkuu wa wilaya alisema kuwa kwa miaka ya sasa mpira umekuwa kimbilio kubwa la ajira kwa vijana kwani huweza kuwasaidia kujiingizia kipato.
Mushi alisema kuwa pamoja na wadau kuwekeza katika mpira wa miguu, Tanzania itaweza vile vile kukuza vipaji ambavyo huwa vinapotea.
“Tanzania tuna vipaji vingi sana vya mpira wa miguu, tatizo ni vipaji hivyo kuvumbuliwa hivyo nawaombeni wadau mbali mbali kutoka sekta zote kujitokeza kuweza kuwekeza katika tasnia hii, ambapo tutawezesha vijana wetu kujipatia ajira,” alisema
Timu ya Stakishari kutoka Mogo iliifunga timu ya Vipaji Halisi kutoka eneo la Airport katika fainali na kukabidhiwa kombe pamoja na kiasi cha sh. 500,000 huku mshindi wa pili alipata Sh. 300,000 na mpira moja na mshindi wa tatu alipata sh. 100,000 na mpira.
Jumla ya timu 20 kutoka Kata ya Kipawa zilishiriki katika mashindano hayo.
Muandaaji wa mashindano hayo diwani wa kata hiyo Bonnah Kaluwa  alisema “Lengo kubwa ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta vijana pamoja iliwaweze kufahamiana na kushirikiana lakini pia kuinua vipaji vya vijana katika mchezo wa mpira wa miguu. Vijana wengi wanaocheze katika ligi hapa nchini wamechipukia katika kata ya Kipawa.  “ Napenda kuendeleza na kukuza vipaji wa vijana iliwaweze kufikia kiwango cha juu zaidi katika mchezo huu”, alisema
Said Mkuwa, Mwenyekiti wa mashindano hayo aliongeza: 
“Tunamshukuru sana diwani kuandaa mashindano haya kwa ajili ya vijana, alisema  
Nimefurahi kwamba mashindano yamekwenda vizuri tangu mechi za mwanzo hadi fainali na vijana wameshirikiana vizuri katika michezo yote”