STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 8, 2013

Fella Atoa zawadi ya Ramadhani

Said Fella

MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family na Kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella amefyatua albamu mpya ya Kaswida ikiwa kama  zawadi kwa waumini wa Kiislam wanaojiandaa kufunga mwezi wa Ramadhani unaoanza wiki ijayo.
Fella alisema kaswida huyo ina nyimbo nne na zote zimeimbwa na Ustaadh Kundi na Asma Juma ikiwa ni muendelezo wake wa kuwapa zawadi waumini kwani hata mwaka jana alifanya kama hivyo kabla ya kuanza kwa mfungo huo wa Ramadhani.
"Wakati tukielekea kwenye mfungo wa Ramadhani, nimeachia albamu yangu ya pili ya nyimbo za Kaswida ambayo ilitarajiwa kuachiwa rasmi Jumanne uliyopita, nyimbo zake zote nne zikimbwa na Ustaadh Kundi na Asma Juma," alisema.
Fella alizitaja nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo iitwayo Kaswida Vol. 11 kuwa ni 'Ujana', 'Mungu Ametuagiza', 'Harusi' na 'Dunia Isitulaghai'.

No comments:

Post a Comment