STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 8, 2013

Masoko Veterani watwaa Kombe la Mbunge wa Kilwa Kusini


Kombe walilonyakua kwenye michuano hiyo likionekana kwa karibu

Mgeni rasmi wa fainali hizo, DED Adoh Mapunda akijiandaa kumkabidhi 'mwali' nahodha wa Masoko Veterani baada ya timu yake kuilaza Transpoter kwa bao 1-0

Dole Tupu! Rahaa ya ushindi Meneja Pius Cheche akichekelea timu yake ya Masoko Veterani kunyakua ubingwa wa Jimbo la Kilwa Kusini

Transpoter wakikaguliwa na mwamuzi kabla ya kuanza kwa kipute kilichopelekea kulala bao 1-0

washindi wakikabidhiwa seti ya jezi

Washindi wakifurahia baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya Mbuzi mnyama

Hureee! nahodha wa Masoko akiinua kombe la ubingwa wa michuano hiyo sambamba na mgeni rasmi, DED Adoh Mapunda
http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AJBaimIAACsfUdqyxwptbT6HgNk&midoffset=2_0_0_1_966531&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
Hata watasha nao walikuwapo uwanjani kushuhudia fainali hiyo

http://thumbp4-ne1.thumb.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AA5bimIAAIsDUdq0hgsa%2FEyAbU0&midoffset=2_0_0_1_970261&partid=2&f=1215&fid=Inbox&w=480&h=331
Kikosi cha mabingwa wa michuano hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya fainali hiyo

 
TIMU ya soka ya Masoko Veterani ya Kilwa Kusini, juzi imefanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wa michuano ya kuwania Kombe la Mbunge wa Kilwa Kusini baada ya kuinyamazisha Transpoter kwa kuilaza bao 1-0 katika pambano kali la fainali ya michuano hiyo.
Bao pekee lililoipeperusha sherehe zilizoandaliwa na Transpoter katika ukumbi wa Kilwa By Night kulikokuwa kuangushwe Kiduku mwanzo mwisho, lilitupiwa kimiani katika dakika ya 75 na Salum Teru akimalizia kazi nzuri ya Yusuph Polisi aliyeingia dimbani badala ya Shaaban Kassali.
Kabla ya kupatikana kwa bao hilo timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu kusaka mabao tangu kipindi cha kwanza ambacho kiliishia kwa suluhu ya 0-0 hali iliyoendelea hata kipindi cha pili mpaka Masoko ilipofanikiwa kujipatia bao hilo la pekee kwenye pambano hilo.
Ushindi huo ulioshuhudiwa wa Mbunge wa Jimbo hilo, Said Bungari 'Bwege' na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa aliyekuwa mgeni rasmi, Adoh Mapunda, imewafanya Masoko Veterani kunyakua zawadi ya kombe, jezi na mnayama mbuzi.


No comments:

Post a Comment