TAARIFA kutoka nchini Afrika Kusini zinasema wanawake wawili wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Oliver Tambo wakitokea Tanzania, wakiwa na dawa za kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa nchi himo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa dawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za dawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
“Tulipowakagua mizigo yao mabegi sita na kufanikiwa kukuta kilo si chini ya 150 za Crystal Meth zilizokuwa zikiingizwa nchini humu (Afrika Kusini)," alisema Muller.
Hata hivyo wanawake hao wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi la nchini hiyo, hawakutajwa majina yao wala uraia wao mpaka sasa kwa lengo la kutoharibu upepelezi.

No comments:
Post a Comment