Maafisa
wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi
mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa
madarakani Mohammed Morsi walikua wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa
hapo. Watu wengine 300 wamejeruhiwa. Kundi
la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale
linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia. Brotherhood imelaumu
jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao
na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi
Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia
wenzake.
Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.
Waandamanaji
hao wanasema vikosi maalum viliwafyatua risasi baada ya swala ya fajir
huku wengine wakishambuliwa walipokusanyika nje ya makao ambako bwana
Morsi anadhaniwa kuzuiliwa wakitaka watawala kumwachilia huru.
Msemaji wa
chama cha Muslim brotherhood amesema kuwa idadi ya waliofariki katika
ghasia hizo imefikia 30 huku zaidi ya watu 500 wakijeruhiwa.
Lakini
katika taarifa yake, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa kundi moja la
kigaidi lilikuwa likijaribu kuingia katika kambi hiyo na kumuua
mwanajeshi mmoja.
Limeongezea zaidi ya watu 200 walitiwa mbaroni wakimiliki silaha kama vile visu.
Duru kutoka wizara ya afya zilisema kuwa afisaa mmoja wa jeshi aliuawa.
Bwana Morsi,
aliyekuwa rais wa kwanza wa kiisilamu kuchaguliwa kidemopkrasia Misri,
aling'olewa mamlakani na jeshi, siku ya Jumatano baada ya kufanyika
maandamano makubwa.
Mmoja wa
waandamanaji Mahmud al-Shilli, aliambia shirika la habari la AFP kuwa
wanajeshi waliwarushia gesi ya kutoa machozi lakini kikundi cha wanaume
waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliwafyatulia risasi.
Katika
taarifa iliyosomwa kwenye vyombo vya yhabari vya serikali, jeshi
lililaumu kikundi cha watu wlaiokuwa wamejihami ambao limesma ni mgaidi
waliokuwa na njama ya kuvamia kambi ya jeshi.
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment