STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 8, 2013

Arsenal nayo yamnyatia Suarez wa Liverpool


Luis Suarez

IKIWA katika hatua ya mwisho ya kumnyakua Gonzalo Higuani, klabu ya Arsenal imetajwa kuwa mbioni kumfukizia mshambuliaji nyota wa Liverpool na Uruguay, Luis Suarez kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao.
Klabu hio ya Arsenal ambayo ina misimu kadhaa haijanyakua taji lolote, imeomba kumnunua Suarez kwa paundi milioni 30.
Hata hivyo duru za kisoka zinasema kuwa  maombi yamekataliwa na Liverpool ikitaka wakali hao wa London ya Kaskazini kuongeza mkwanja zaidi iwapo wana nia ya kweli ya kumnyakua 'mtukutu' huyo wenye shabaha ya magoli.
Mshambuliaji huyo amekuwa na wakati mgumu nchini England kutokana na kuandamwa na vyomvo vya habari hasa kutokana na matukio kadhaa ya hivi karibuni aliyoyafanya kiasi cha kufungiwa kucheza soka kwa nyakati tofauti.
Tukio la awali lilikuwa ni la kibaguzi alilodaiwa kumfanyia beki wa Manchester United kabla ya kuonekana akimng'ata kiganja beki wa Chelsea. Branislav Ivanovic na kufungiwa kucheza mechi nane wakati tukio la kwanza alikosa mechi 109 na faini juu.
Suarez ameshaweka wazi dhamira yake ya kutaka kuondoka Liverpool, huku Real Madrid ilijaribu bahati yake kwa kutuma maombi ya kumsajili mshambuliaji huyo kabla ya Chelsea na Arsenal kuingia kwenye mbio hizo za kunasa saini yake.

No comments:

Post a Comment