STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 4, 2013

Real Madrid 'yaua' Ulaya, Borrusia Dotmund yabanwa

Ronaldo akishangulia bao lake
IKIWA dimba la nyumbani la Bernabeu, klabu ya Real Madrid usiku wa kuamkia leo imeifanyia 'mauaji' timu ya Galatasaray kwa kuifumua mabao 3-0.
Pambano hilo la Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lilichezwa mjini Madrid, Hispania ambapo vijana wa Jose Mourinho walijitengenezea nafasi nzuri ya kutinga Nusu Fainali.
Cristiano Ronaldo alianza kuifungia Madrid bao la kwanza mapema kipindi cha kwanza dakika ya tisa kabla ya Karim Benzema kufunga la pili dakika ya 29. 
Gonzalo Higuain aliyetokea benchi kipindi cha pili alifunga la tatu kwa kichwa dakika ya 73 na kuwafanya Madrid wajiandae kwenda Uturuki wakiwa na tiketi ya nusu fainali
Didier Drogba aliyeiongoza Chelsea kutwaa taji hilo la Ulaya msimu uliopita jana hakuonyesha makeke yake licha ya kupoteza nafasi mbili za wazi.
Katika pambano jingine la michuano hiyo, Mabingwa wa Ujerumani, Borrusia Dotmund ilishindwa kutamba ugenini nchini Hispania baada ya kung'ang'aniwa na Malaga.
Timu hizo zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu ya bila kufungana na kutoa nafasi kubwa kwa Borrusia kujitengenezea mazingira ya kufuzu ikiwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment