STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, April 4, 2013

Mheshimiwa Temba ebu Toroka Uje

Mhe Temba


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Aman Temba 'Mheshimiwa Temba' amevunja ukimya kwa kufyatua wimbo wake mpya uitwao 'Toroka Uje'.
Katika wimbo huo Mhe Temba ameimba akishirikiana na wasanii  Aslay Is'haka 'Dogo Aslay' na Yessaya Ambikile 'YP'.
Huo ni wimbo wa kwanza kwa Temba tangu alipotoa kazi yake ya mwisho mwaka jana iitwayo Mariyo alioimba pamoja na Cheka Hija 'Bibi Cheka'.
Meneja wa kundi la TMK, Said  Fella alisema wimbo huo wa Temba unaozungumzia kijana anayemsihi mpenzi wake atoroke ili wakajirushe umetoka sambamba na video ya Aslay iitwayo 'Wahenga'.
Fella alisema kama zilivyo kazi za nyuma ya Temba wimbo huo ni moja na nyimbo kali ikizingiatiwa vichwa alivyoimba navyo ambavyo vimeutendea haki.
"Baada ya kimya kirefu tangu atoe ngoma yake ya Mariyo aliyoimba na Bibi Cheka, Mheshimiwa Temba amechia wimbo mpya uitwao 'Toroka Uje', " alisema Fella.
Fella alisema video ya wimbo huo ipo njiani ikiendelea kurekodiwa, huku video ya wimbo wa 'Maneno ya Wahenga' ya msanii Dogo Aslay imeshatoka rasmi.

No comments:

Post a Comment