STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 21, 2014

Diamond, WEma wote Bei Kali bhanaa!



STAA wa nyimbo za 'Bum Bum' na 'Mdogomdogo' Nasibu Abdul 'Diamond' na mpenzie wake, Wema Sepetu 'Madam' wanatarajia kucheza filamu ya pamoja iitwayo 'Bei Kali'.
Filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kushutiwa hivi karibuni inazalishwa na kampuni ya Siumulizi African Entertainment ya msanii Simon Mwapagata 'Rado'.
Rado aliliambia MICHARAZO kuwa, filamu hiyo ya mapenzi itaanza kurekodiwa baada ya kuafikia na wenzao hao ambao wamekuwa gumzo kwa mashabiki wa burudani nchini.
Mkali huyo alisema mazungumza na wawili hao yapo katika hatua nzuri na kwamba itakuwa mara ya kwanza kwa nyota hao kuuza sura kwa pamoja katika filamu.
Rado alisema mbali na Diamond na Wema pia, ndani ya filamu hiyo atakuwepo yeye mwenyewe na wasanii wengine.
"Natarajia kutengeneza filamu mpya iitwayo 'Bei Kali' ambayo miongoni mwa washiriki wake ni Diamond na Wema Sepetu na kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ya mwisho," alisema.
Rado alisema ushiriki wa nyota hao ndani ya 'Bei Kali' utaifanya filamu hiyo kuendana na uhalisi wa jina lake kwani Diamond na Wema ni wasanii wa kiwango cha kimataifa.
"Kama wenyewe walivyo ghali, filamu ya Bei Kali inawafaa na mashabiki watarajie kumuona Diamond kivingine, kwa Wema hakuna maswali juu ya umahiri wake katika uigizaji," alisema.

Mfungo wakwamisha video ya Shaa

VIDEO ya wimbo mpya unaendelea kutamba hewani wa staa wa zamani wa kundi la Wakilisha, Sarah Kais 'Shaa' uitwao 'Subira' imekwama kutoka na sasa itatoka baada ya Idd.
Meneja wa msanii huyo, Said Fella 'Mkubwa' aliiambia MICHARAZO kuwa, video iliyotayarishwa na Adam Juma wa Next Level Production imeshindwa kuachiwa kupisha Mfungo.
Fella alisema kwa namna 'mauno' yaliyopo ndani ya video hiyo imemfanya asitishe kuiachia hewani kuhofia kuwaharibia 'swaumu' mashabiki wao na itaachiwa baada ya mfungo huo.
"Video ya Shaa iitwayo 'Subira' ambayo ilikuwa itokee na audio yake, tumeisitisha mpaka baada ya kumalizika mfungo kwa sababu ndani ya video hiyo kuna mauno sana," alisema.
Fella alisema hivyo mara baada ya kusherehekewa kwa sikukuu ya Eid el Fitri video hiyo itaachiwa hewani kwenda sambamba na audio yake ambayo imekuwa gumzo kwa sasa.
Wimbo huo wa Subira ni wa pili kwa Shaa tangu awe chini ya lebo ya Mkubwa na Wanaye, awali akitoka na singo iitwayo 'Sugua Gaga'.

Hivi ndivyo Stars ilipobanwa na Mambas Taifa

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Msumbiji katika mchezo uliofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji.
Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akiwa katikati ya mabeki wa timu ya taifa ya Msumbiji. 
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2. 
 Thomas Ulimwengu  akichuana na beki wa Msumbiji, Josemar Machaisse.
 Huniwezi…Mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu
akimtoka beki wa Msumbiji, Zainadine Junior.
 Mshambuliaji wa Stars, Khamis Mcha akiwa katika harakati za kufunga goli.
 Golikipa wa Stars, Deogratius Munishi akishangilia bao la pili la Taifa Stars kwa kuonyesha fulana yake iliyokuwa ikisomeka ‘Sisi ni Watoto wa Rais Kikwete’.
Picha zote na francisdande

'Kipusa' cha Kaole Kwanza kuleta mapinduzi Bongo'

Mwenyekiti wa Kaole Kwanza, Ndimbagwe Misayo 'Thea'
Baadhi ya wasanii wa Kaile Kwanza katika picha ya pamoja na waalikwa wakati wa uzinduzi wa igizo lao la Kipusa hivi karibuni
Baadhi ya wasanii wa Kaile Kwanza katika picha ya pamoja na waalikwa wakati wa uzinduzi wa igizo lao la Kipusa hivi karibuni
MWENYEKITI wa kundi la Kaole Kwanza linaloundwa na nyota wa zamani wa Kaole Sanaa Group, Ndimbagwe Misayo 'Thea' amelitabiria igizo lao la 'Kipusa' kuleta mapinduzi makubwa katika fani ya uigizaji hasa michezo ya kwenye runinga.
Thea alisema hadithi ya igizo hilo linalotarajiwa kuanza kuonekana hewani hivi karibuni na namna wasanii walioshiriki walivyoitendea haki mbele ya kamera inampa 'jeuri' ya kuamini tamthilia ya 'Kipusa' itafunika sana ikianza kurushwa.
Akizungumza na MICHARAZO, Thea alisema mseto wa wasanii wazoefu na chipukizi chini ya muongozaji mahiri nchini Christant Mhenga na jinsi simulizi la igizo hilo lilivyo ni wazi litafunika na kuleta mapinduzi katika fani ya uigizaji siku za usoni.
Thea alisema Kaole Kwanza hawakukurupuka kuamua kuandaa kazi hiyo ambayo tayari ipo katika hatua ya mwisho kabla ya kurushwa na kituo kimojawapo nchini cha runinga baada ya mazungumzo ya pande mbili kwenda vizuri mpaka sasa.
"Hakukurupuka, tulikaa chini na kufikiria namna ya kusaidia kupeleka mbele gurudumu la fani ya uigizaji na kuibuka na 'Kipusa' tunataka kuwaonyesha wengine uwezo tulionao, pamoja na kusaidia kuingia kwenye ushindani wa kimataifa," alisema Thea.
Mwenyekiti huyo pia alifafanua kuwa wameamua kutumia jina la Kaole Kwanza kwa sababu asilimia kubwa ya wasanii waliibukia na kutamba kupitia Kaole Sanaa na hawakufanya hivyo kwa lengo la kuibua malumbano na wasanii wengine.
"Sisi ni Kaole Kwanza, chimbuko letu ni Kaole Sanaa...Wanaolalamika kuhusu sisi labda wana yao na hatuko kwa ajili ya kulumbana na mtu sisi kazi yetu kuwapa burudani mashabiki wa sanaa," alisema Thea baada ya kuulizwa swali kuhusu uongozi wa Kaole Sanaa kulalamika utambulisho wa kundi hilo jipya kama Kaole.

Staina, Ney wa Mitego Kwenu Vipi?


MSANII mkali wa hip hop, Stamina, kutoka mji wa Morogoro, ameachia wimbo wake mpya uitwao 'Kwenu Vipi' ambao amemshirikisha mkali mwingine wa 'michano', Ney wa Mitego.
Wimbo huo tayari umeanza kusikika hewani kupitio vituo vya redio na mitandao ya kijamii ikiwa ni kazi mpya kwa Stamina tangu alipoachia wimbo wa mwisho uitwao 'Mguu Pande Mguu Sawa' alioimba na mshindi wa BSS, Walter Chilambo.
Kwa mujibu wa Stamina, wimbo huo umetengenezwa katika studio za Seductive Records chini ya mtayarishaji mkali wa nyimbo za 'Muziki Gani' na 'Salam Zao'.
Msanii huyo anasifika kwa umahiri wa kutunga mistari 'mitamu' katika nyimbo zake na amejipatia umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake kadhaa zinazoendelea kutamba kwa sasa nchini.
Baadhi ya nyimbo za Stamina alizoimba mwenyewe na kushirikisha wasanii wengine ni 'Kabwela', 'Alisema', 'Najuta Kubalehe', 'Wazo la Leo', 'Mwambie Mwenzio', 'Mke wa Baba', 'Jamvi la Wageni' na 'Mapenzi'.