STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 21, 2014

Diamond, WEma wote Bei Kali bhanaa!STAA wa nyimbo za 'Bum Bum' na 'Mdogomdogo' Nasibu Abdul 'Diamond' na mpenzie wake, Wema Sepetu 'Madam' wanatarajia kucheza filamu ya pamoja iitwayo 'Bei Kali'.
Filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kushutiwa hivi karibuni inazalishwa na kampuni ya Siumulizi African Entertainment ya msanii Simon Mwapagata 'Rado'.
Rado aliliambia MICHARAZO kuwa, filamu hiyo ya mapenzi itaanza kurekodiwa baada ya kuafikia na wenzao hao ambao wamekuwa gumzo kwa mashabiki wa burudani nchini.
Mkali huyo alisema mazungumza na wawili hao yapo katika hatua nzuri na kwamba itakuwa mara ya kwanza kwa nyota hao kuuza sura kwa pamoja katika filamu.
Rado alisema mbali na Diamond na Wema pia, ndani ya filamu hiyo atakuwepo yeye mwenyewe na wasanii wengine.
"Natarajia kutengeneza filamu mpya iitwayo 'Bei Kali' ambayo miongoni mwa washiriki wake ni Diamond na Wema Sepetu na kwa sasa tupo kwenye mazungumzo ya mwisho," alisema.
Rado alisema ushiriki wa nyota hao ndani ya 'Bei Kali' utaifanya filamu hiyo kuendana na uhalisi wa jina lake kwani Diamond na Wema ni wasanii wa kiwango cha kimataifa.
"Kama wenyewe walivyo ghali, filamu ya Bei Kali inawafaa na mashabiki watarajie kumuona Diamond kivingine, kwa Wema hakuna maswali juu ya umahiri wake katika uigizaji," alisema.

No comments:

Post a Comment