STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 21, 2014

Staina, Ney wa Mitego Kwenu Vipi?


MSANII mkali wa hip hop, Stamina, kutoka mji wa Morogoro, ameachia wimbo wake mpya uitwao 'Kwenu Vipi' ambao amemshirikisha mkali mwingine wa 'michano', Ney wa Mitego.
Wimbo huo tayari umeanza kusikika hewani kupitio vituo vya redio na mitandao ya kijamii ikiwa ni kazi mpya kwa Stamina tangu alipoachia wimbo wa mwisho uitwao 'Mguu Pande Mguu Sawa' alioimba na mshindi wa BSS, Walter Chilambo.
Kwa mujibu wa Stamina, wimbo huo umetengenezwa katika studio za Seductive Records chini ya mtayarishaji mkali wa nyimbo za 'Muziki Gani' na 'Salam Zao'.
Msanii huyo anasifika kwa umahiri wa kutunga mistari 'mitamu' katika nyimbo zake na amejipatia umaarufu mkubwa kupitia nyimbo zake kadhaa zinazoendelea kutamba kwa sasa nchini.
Baadhi ya nyimbo za Stamina alizoimba mwenyewe na kushirikisha wasanii wengine ni 'Kabwela', 'Alisema', 'Najuta Kubalehe', 'Wazo la Leo', 'Mwambie Mwenzio', 'Mke wa Baba', 'Jamvi la Wageni' na 'Mapenzi'.

No comments:

Post a Comment