STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 21, 2014

'Kipusa' cha Kaole Kwanza kuleta mapinduzi Bongo'

Mwenyekiti wa Kaole Kwanza, Ndimbagwe Misayo 'Thea'
Baadhi ya wasanii wa Kaile Kwanza katika picha ya pamoja na waalikwa wakati wa uzinduzi wa igizo lao la Kipusa hivi karibuni
Baadhi ya wasanii wa Kaile Kwanza katika picha ya pamoja na waalikwa wakati wa uzinduzi wa igizo lao la Kipusa hivi karibuni
MWENYEKITI wa kundi la Kaole Kwanza linaloundwa na nyota wa zamani wa Kaole Sanaa Group, Ndimbagwe Misayo 'Thea' amelitabiria igizo lao la 'Kipusa' kuleta mapinduzi makubwa katika fani ya uigizaji hasa michezo ya kwenye runinga.
Thea alisema hadithi ya igizo hilo linalotarajiwa kuanza kuonekana hewani hivi karibuni na namna wasanii walioshiriki walivyoitendea haki mbele ya kamera inampa 'jeuri' ya kuamini tamthilia ya 'Kipusa' itafunika sana ikianza kurushwa.
Akizungumza na MICHARAZO, Thea alisema mseto wa wasanii wazoefu na chipukizi chini ya muongozaji mahiri nchini Christant Mhenga na jinsi simulizi la igizo hilo lilivyo ni wazi litafunika na kuleta mapinduzi katika fani ya uigizaji siku za usoni.
Thea alisema Kaole Kwanza hawakukurupuka kuamua kuandaa kazi hiyo ambayo tayari ipo katika hatua ya mwisho kabla ya kurushwa na kituo kimojawapo nchini cha runinga baada ya mazungumzo ya pande mbili kwenda vizuri mpaka sasa.
"Hakukurupuka, tulikaa chini na kufikiria namna ya kusaidia kupeleka mbele gurudumu la fani ya uigizaji na kuibuka na 'Kipusa' tunataka kuwaonyesha wengine uwezo tulionao, pamoja na kusaidia kuingia kwenye ushindani wa kimataifa," alisema Thea.
Mwenyekiti huyo pia alifafanua kuwa wameamua kutumia jina la Kaole Kwanza kwa sababu asilimia kubwa ya wasanii waliibukia na kutamba kupitia Kaole Sanaa na hawakufanya hivyo kwa lengo la kuibua malumbano na wasanii wengine.
"Sisi ni Kaole Kwanza, chimbuko letu ni Kaole Sanaa...Wanaolalamika kuhusu sisi labda wana yao na hatuko kwa ajili ya kulumbana na mtu sisi kazi yetu kuwapa burudani mashabiki wa sanaa," alisema Thea baada ya kuulizwa swali kuhusu uongozi wa Kaole Sanaa kulalamika utambulisho wa kundi hilo jipya kama Kaole.

No comments:

Post a Comment