STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 21, 2014

Mfungo wakwamisha video ya Shaa

VIDEO ya wimbo mpya unaendelea kutamba hewani wa staa wa zamani wa kundi la Wakilisha, Sarah Kais 'Shaa' uitwao 'Subira' imekwama kutoka na sasa itatoka baada ya Idd.
Meneja wa msanii huyo, Said Fella 'Mkubwa' aliiambia MICHARAZO kuwa, video iliyotayarishwa na Adam Juma wa Next Level Production imeshindwa kuachiwa kupisha Mfungo.
Fella alisema kwa namna 'mauno' yaliyopo ndani ya video hiyo imemfanya asitishe kuiachia hewani kuhofia kuwaharibia 'swaumu' mashabiki wao na itaachiwa baada ya mfungo huo.
"Video ya Shaa iitwayo 'Subira' ambayo ilikuwa itokee na audio yake, tumeisitisha mpaka baada ya kumalizika mfungo kwa sababu ndani ya video hiyo kuna mauno sana," alisema.
Fella alisema hivyo mara baada ya kusherehekewa kwa sikukuu ya Eid el Fitri video hiyo itaachiwa hewani kwenda sambamba na audio yake ambayo imekuwa gumzo kwa sasa.
Wimbo huo wa Subira ni wa pili kwa Shaa tangu awe chini ya lebo ya Mkubwa na Wanaye, awali akitoka na singo iitwayo 'Sugua Gaga'.

No comments:

Post a Comment