STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 29, 2012

KUMUONA JB MPIANA NI KWA 100,000



 JB Mpiana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu shoo yake itakayofanyika Leaders Club Novemba 30.
Mtangaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Said Kilumbanga (kulia) akiwa amepozi na wanenguaji wa  mwanamuziki kutoka Congo, JB Mpiana
DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII nguli wa muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kushuhudia shoo yake itakayopigwa kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Ijumaa hii, ambapo kiingilio kwa VIP A itakuwa sh 100,000 na kawaida sh 25,000.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, JB Mpiana alisema, anajikubali na kuithamini kazi yake ambayo anaifanya na kuahidi kuwapa raha wapenzi na wadau mbalimbali wa muziki hapa nchini ambao watajitokeza siku hiyo.

“Kwanza nimefurahia sana mapokezi ya jana, hivyo basi nitawapa raha siku hiyo na pia nawapongeza waandaaji kwa kuona umuhimu na kuniteua mimi kufanya nao kazi siku hiyo, nimekuja na kikosi changu kamili cha watu 25, hivyo basi nina imani siku hiyo itakuwa raha sana,” alisema Mpiana.

Mpiana aliwataka wanamuziki wa hapa nchini, kujituma na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuziheshimu pia, ili waweze kufikia mafanikio ambayo wamejipangia kuyafikia, kwa kuwa hata yeye alianzia huko na ndio sababu amefikia hapa alipo.

Naye Mkurugenzi wa QS J Mhonda Entertainment, Joseph Mhonda, alisema kila kitu kimekamilika na kudai kuwa, kwa sasa wanasubiri siku ifike ili watanzania wapate raha na kile ambacho wamekitarajia.
Mhonda alisema, viingilio siku hiyo itakuwa sh 25,000 kwa atakayenunua tiketi mapema, huku 30,000 kwa watakaonunulia mlangoni na sh 100,000 VIP A kwa watakaonunua mapema huku kwa mlangoni ni sh 150,000.

Aliongeza kuwa, Mpiana ataanza kufanya shoo ukumbi wa Triple A, jijini Arusha na baadaye jijini Mwanza katika ukumbi wa Villa Park huku wasanii mbalimbali wakitarajiwa kutumbuiza siku hiyo ambao ni Ney Wamitego, H Baba, Mashujaa pamoja na Mb Dog.

BONDIA TYSON FURY KUMVAA WLADIMIR KLITSCHKO MWAKANI



LONDON, England
“Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu tayari sasa kwa hilo. Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai
BONDIA mahiri Tyson Fury amepania kupanda ulingoni kupimana ubavu na Wladimir Klitschko kuwanuia ubingwa wa dunia kiangazi kijacho.
Fury, 24, bondia asiyepigika katika uzani wa ‘heavyweight,’ Jumamosi hii anapanda ulingoni kumvaa Mmarekani Kevin Johnson jijini Belfast, Ireland ya Kaskazini.
Na promota wa pambano la Jumamosi Mick Hennessy amedai kuwa, ushindi kwa Fury mwenye urefu wa futi 6.9, utampa fursa ya kuandaliwa pambano dhidi ya Klitschko - bingwa wa mikanda ya WBA, IBF, na WBO.
Hennessy alisema: “Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu tayari sasa kwa hilo.
“Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai.
“Ujerumani ni nchi inayoweza kuwa kipaumbele chetu kupigwa pambano hilo, lakini nimeshazungumza na wamiliki wa Uwanja wa Old Trafford au Croke Park,” alisema Hennessy.
You might also like:

Waziri Mathayo, Nape kuwashuhudia Miyeyusho, Nassib PTA

Mabondia Francis Miyeyusho (kushoto) na Nassib Ramadhani watakaopigana Desemba 9


WAKATI mabondia Francis Miyeyusho na Nassib Ramadhani wakitarajiwa kupima uzito Desemba 8 kabla ya kuvaana kuwania ubingwa wa Mabara wa WBF, viongozi waalikwa watakaoshuhudia pambano hilo wamefahamika.
Promota wa pambano hilo litakalofanyika jijini Dar siku ya Desemba 9, Mohammed Bawazir aliiambia MICHARAZO, miongoni mwa viongozi hao waalikwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo.
Bawazir alisema mbali na Dk Mathayo, wengine waliothibitisha kushuhudia pambano hilo la uzani wa Bantam ni pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Katibu wa Itikidi na Uenezi-CCM, Nape Nnauye.
"Hao  ni baadhi ya viongozi wakuu tuliowatumia mwaliko na kutuhakikishia watahudhuria na tutamtangaza mgeni rasmi siku ya Desemba 6," alisema.
Promota huyo alisema wangependa mgeni rasmi katika pambano hilo awe mmoja wa viongozi wa juu wa Taifa na ndiyo maana wanaendelea kusubiri majibu ya mwaliko wao kabla ya kumtangaza jina katika mkutano wao ujao.
Juu ya maandalizi ya pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kutokana na ubora na rekodi za mabondia hao wawili, Bawazir alisema yanaendelea vema japo wamekwama kupata wadhamini wa kuwapiga tafu.
Bawazir alisema pamoja na hayo bado wanaendelea kuitoa wito kwa watu wenye mapenzi mema na mchezo wa ngumi kujitokeza kuwapa nguvu, huku akisema upimwaji wa uzito na afya kwa mabondia utafanyika Desemba 8.
"Maandalizi yaendelea vema japo wadhamini wanasuasua kujitokeza na mabondia wote watapimwa kupimwa uzito na afya zao Desemba 8, siku moja kabla ya kupanda ulingoni," alisema.
Pambano hilo litafanyika chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST na litatanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizi.
Michezo hiyo ya utangulizi ni kati ya Fadhili Majia vs Juma Fundi, Mohammed Matumla dhidi ya Doi Miyeyusho, Ibrahimu Class vs Said Mundi, Fred Sayuni dhidi ya Deo Samwel na Hassan Kidebe dhidi ya Baina Mazola.

Mwisho

Katina ataka Kim Poulsen akumbatiwe Bongo

Shija Katina enzi zake uwanjani akishangilia moja ya mabao yake

NYOTA wa zamani wa timu za soka za Kagera Sugeer, Moro Utd na Kipanga Zanzibar, Shija Katina, amewataka watanzania kumuunga mkono kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen, katika kazi yake akiamini anaweza kuifikisha mbali Tanzania.
Katina, ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Golden Bush, inayojiandaa na Ligi ya TFF wilaya ya Kinondoni, alisema Kim ni miongoni mwa makocha bora ambao Tanzania imewahi kuwapata hivyo anapaswa kuaminiwa na kupewa ushirikiano mzuri.
Alisema kitendo cha kuwapa nafasi vijana katika vikosi vya timu anazofundisha ni dalili nzuri kwamba kocha huyo ana malengo makubwa kwa Tanzania hivyo hapaswi kuyumbishwa.
"Kwa staili yake ya kukumbatia vijana ni nzuri kwa mustakabali wa soka la Tanzania hivyo watanzania tunapaswa kumuunga mkono na kumpa ushirikiano wa kutosha, huku wadau wa soka tukielekeza nguvu kwenye maandalizi ya timu yetu," alisema.
Alisema, japo Stars kufuzu kwake kwenye fainali za Kombe la Dunia za Brazil huenda ikawa ni kwa kubahatisha, lakini kwa  namna kocha huyo anavyofanya ni wazi anafikiria fainali za mbeleni zaidi kuliko hizo za 2014.
Katina, alisema mbali na ushirikiano wa kutosha, lakini pia Stars inapaswa kuandaliwa vema kwa mechi zao za kimataifa, ili kuweza kufanya vema badala ya kusubiri maandalizi ya zima moto biola timu kupewa mechi za kujipima nguvu.
Stars iliyopo kundi C katika uwaniaji wa fainali hizo za Kombe la Dunia, inatarajiwa kuanza kambi yake mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea mjini Uganda, ambapo Kim ameenda na Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara inayopigana kucheza robo fainali toka kundi lake.

Zahoro Pazi wa Azam azipotezea Simba, Yanga kisa...!

Zahoro Pazi akiwa katika pozi mbele ya gari lake

MSHAMBULIAJI wa Azam, Zahoro Pazi, ameweka bayana kwamba hana mpango wa kuzichezea Simba na Yanga kwa sasa kutokana na klabu aliyopo sasa nayo ni miongoni mwa klabu kubwa na zenye malengo ya dhati kisoka.
Pazi, aliyekaribia kutua Simba msimu wa 2010-2011 kwa mkataba wa miaka minne kabla ya 'dili' lake kukwama baada ya Simba kushindwa kutekeleza makubaliano yao na timu ya Mtibwa aliyokuwa anaichezea wakati huo, alisema Azam ni klabu yenye malengo.
Alisema kwa mchezaji yeyote mwenye malengo ya kufika mbali Azam ni klabu sahihi kuichezea, kutokana na kwamba ni klabu inayoioinyesha dhati ya kuleta mabadiliko ya soka nchini na kwa sasa imekuwa miongoni mwa klabu kubwa.
Pazi, ambaye anamaliza mkataba wa kuichezea Azam mwezi ujao, alisema anadhani alifanya maamuzi sahihi kuichezea klabu hiyo, huku akisema hata kama ataachwa katika timu hiyo basi ataelekeza nguvu zake kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
"Sifikirii kuzichezea Simba na Yanga kwa sasa, kama mkataba wangu hautaongezwa Azam basi nitaelekeza nguvu zangu kwenda kucheza soka la kulipwa nje. Japo Simba na Yanga ni klabu kubwa na kongwe, lakini hazina malengo kama Azam," alisema.
Mchezaji huyo ambaye ni mtoto wa kipa nyota wa zamani wa kimataifa aliyewahi kuwika Simba na Pilsner, Idd Pazi 'Father' alisema kipindi cha nyuma Simba na Yanga zilikuwa kimbilio la wengi kwa sababu hakukuwa na klabu yenye ushindani kama Azam.
Pazi, aliyetua Azam msimu uliopita baada ya kuitumikia Mtibwa Sugar, alisema Simba na Yanga ni timu nzuri na zoefu, lakini kukosekana mipango madhubuti kisoka  imezifanya zipige 'maktaimu' kwa muda mrefu licha ya ukongwe wao barani Afrika.

ZANZIBAR HEROES USO KWA USO NA AMAVUBI YA NIYONZIMA

Zanzibar Heroes

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MASHUJAA wa visiwani, Zanzibar Heroes leo wanatupa kete yao ya pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa kumenyana na Rwanda katika mchezo wa Kundi C, utakaoanza saa 12:00 jioni Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
Mchezo huo utatanguliwa na mchezo mwingine, kati ya Malawi na Eritrea ambao utaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja huo.
Zanzibar walilazimishwa sare ya bila kufungana na Eritrea katika mchezo wa kwanza, wakati Malawi ilifungwa mabao 2-0 na Rwanda.
Zanzibar wanahitaji kushinda mechi ya leo, ili kuweka hai matumaini ya kuingia Robo Fainali ya michuano hii, ingawa mbele ya Rwanda huo utakuwa mtihani mgumu kwao.
Moja kati ya burudani zinazotarajiwa kwenye mechi hiyo ni kushuhudia wachezaji wawili wa klabu moja, Yanga SC ya Dar es Salaam, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, wakichuana leo, tena wote wakiwa manahodha wa timu zao za taifa.
Baada ya sare katika mechi ya kwanza, Cannavaro pamoja na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa sare hiyo, lakini pia ameahidi watajituma na kufanya vizuri katika mechi zijazo.  

CHANZO:BIN ZUBEIRY

KALI YA MWAKA: MTOTO AMUUA MAMAYAKE KWA KUMPIGA NGUMI!


Akina mama waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)

Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
 
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya firauni, unaweza kusema hadithi kumbe nikweli ,Mkazi wa  Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele  Julius amemuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25 mwaka huu.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana  mwingine hali iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi  Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na kijana  mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi huo .

Amesema wakati  mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga ngumi na mateke mwilini.

Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka kupoteza uhai wake.

Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama yake marakwamara .

Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata) umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi.
Chanzo:Mjengwa.

MAN UTD YAZIDI KUPETA ENGLAND, LIVERPOOL CHALI

Robin va Persie akiifungia bao timu yake ya Manchester United dhidi ya West Ham jana (Picha kwa hisani ya BBC Sports)


BAO pekee lililoifungwa katika dakika ya kwanza na mshambuliaji nyota wa Kiholanzi, Robin van Persie jana lilizidi kuifanya Manchester United kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza West Ham bao 1-0, huku Liverpool wakilala ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Ushindi huo wa pili mfululizo kwa Man United ulipataika kwenye dimba lao la Old Trafford na kuwafanya wajikusanyie pointi 33, moja zaidi ya mabingwa watetezi  Manchester City waliopata ushindi ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji wao Wigan Athletic.
Mabao ya City, yalifungwa na James Milner katika dakika ya 69 kabla ya Mario Baloteli kuongeza la pili dakika tatu baadae na kuwafanya mabingwa hao kuendeleza rekodi yao ya kuitopoteza mechi yoyote katika ligi hiyo mpaka sasa ikijikusanyia pointi 32 na kushika nafasi ya pili.
Katika pambano jingine lililochezwa kwenye uwanja wa White Hart Line, mjini London, Tottenham iliilaza Liverpool mabao 2-1 na kuzidi kuwafanya mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Ulaya kwa timu za Uingereza kuzidi kuyumba kwenye ligi kuu ya England.
Magoli ya Tottenham ya jana yalifungwa na Aaron Lennon dakika ya 7 tu ya mchezo kwa kumalizia kazi nzuri ya kiungo Gareth Bale, ambaye alifunga mwenyewe bao la pili kwa Tottenham dakika ya 16 na kufanya hadi mapumziko wenyeji wawe mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji na kushambuliana kwa zamu Liverpool wakionyesha dhamira ya kurejesha mabao hayo, ambapo Bale katika harakati za kuokoa mabao alijikuta akiifungia wageni bao la kufutia machozi.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa jana  Southampton ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Norwich City,    Stoke City  iliilaza Newcastle United mabao 2-1, Swansea City ikaicharaza West Bromwich kwa mabao 3-1 , huku  kocha mpya wa Chelsea Rafa Benitez akiendelea kuambulia sare baada ya kikosi chake kutoka suluhu dhidi ya wageni wao Fulham, nao Everton wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya 1-1 na Arsenal.