STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 29, 2012

ZANZIBAR HEROES USO KWA USO NA AMAVUBI YA NIYONZIMA

Zanzibar Heroes

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MASHUJAA wa visiwani, Zanzibar Heroes leo wanatupa kete yao ya pili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa kumenyana na Rwanda katika mchezo wa Kundi C, utakaoanza saa 12:00 jioni Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
Mchezo huo utatanguliwa na mchezo mwingine, kati ya Malawi na Eritrea ambao utaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja huo.
Zanzibar walilazimishwa sare ya bila kufungana na Eritrea katika mchezo wa kwanza, wakati Malawi ilifungwa mabao 2-0 na Rwanda.
Zanzibar wanahitaji kushinda mechi ya leo, ili kuweka hai matumaini ya kuingia Robo Fainali ya michuano hii, ingawa mbele ya Rwanda huo utakuwa mtihani mgumu kwao.
Moja kati ya burudani zinazotarajiwa kwenye mechi hiyo ni kushuhudia wachezaji wawili wa klabu moja, Yanga SC ya Dar es Salaam, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, wakichuana leo, tena wote wakiwa manahodha wa timu zao za taifa.
Baada ya sare katika mechi ya kwanza, Cannavaro pamoja na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa sare hiyo, lakini pia ameahidi watajituma na kufanya vizuri katika mechi zijazo.  

CHANZO:BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment