STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 6, 2015

Berry Black ajiunga Mkubwa na Wanae atoa 'Byebye'

http://4.bp.blogspot.com/-3miIriWWtBw/TeEM8kwi2HI/AAAAAAAASyM/wZrI8_RKde4/s1600/photo+%252818%2529.JPG
Berry Black
MSANII nyota wa zamani wa kundi la 2 Berry, Berry Black amejiunga na 'lebo' ya Mkubwa na Wanae na tayari ametengeneza ngoma mpya iitwayo 'Byebye' alioimba akiwashirikisha wasanii wa Yamoto Band, Maromboso na Aslay.
Akizungumza na MICHARAZO, Mkurugenzi wa Kituo cha Mkubwa na Wanae, Said Fella alisema kuwa, msanii huyo ameingia mkataba wa kufanya kazi chini ya lebo yao na wamesharekodi wimbo mmoja uliotokana sambamba na video yake.
Fella alisema wimbo huo wa 'Byebye' umetengenezwa katika studio za Vibe Records chini ya mtayarishaji wake, Shirko na video imetengenezwa kupitia kampuni ya Kwetu Studio chini ya Msafiri Shaaban.
"Tumeamua kumrejesha hewani Berry Black kwa kumchukua Mkubwa na Wanae na tumeshatengeneza kazi moja ya 'Byebye' aliyoimba na madogo wa Yamoto na tutaiachia hadharani Ijumaa (leo) audio na video yake," alisema Fella.
Fella alidokeza kuwa baada ya kufanya utambulisho wa kazi hiyo ya Berry Black visiwani Zenji wakisindikiza onyesho la Yamoto Band, wataanza mipango ya kumtoa hadharani Ferooz nyota wa zamani na muasisi wa Daz Nundaz ambaye naye yupo Mkubwa na Wanae ambaye amesharekodi nyimbo mbili ambazo hakutaja majina yake

Yamoto Band kupeleka za uzunguni Zenji

http://lh5.ggpht.com/-RrgOXUuAVTw/VK10m3KsQVI/AAAAAAAArkQ/GmOxtlTmQGA/s1600/IMG_20150107_010322.jpgBAADA ya kurejea kutoka Uingereza walipoenda kutumbuiza mjini London kundi la Yamoto Band linatarajiwa kwenda kuonuyesha makali ya ugahibuni visiwani Zanzibar Jumapili hii.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Said Fella aliliambia MICHARAZO kuwa, Yamoto wataenda kutambulisha nyimbo zao mpya na ubunifu waliotoka nao kwa Malkia katika onyesho litakalofanyika Ngome Kongwe, visiwani humo.
Fella alisema onyesho hilo litasindikizwa na wasanii mbalimbali kutoka TMK na wale wa visiwani humo.
"Tumerejea juzi kutoka Uingereza na Jumapili tunatarajiwa kuvuka maji kwenda Zanzibar kwa ajili ya uitambulisho wa mambo mapya ya Yamoto Band, onyesho litafanyika Ngome Kongwe na kusindikizwa na wasanii mbalimbali.
Katika hatua nyingi msanii Nikki Mbishi aliyetangaza hivi karibuni kuachana na fani ya muziki amevunja ukimya kwa kuibuka na wimbo uitwao 'Sihusiki nao' akimshirikisha mshindi wa BSS 2013, Walter Chilambo.
Nikki alitangaza kuachana na muziki na kuibua mjadala mkubwa ambao ulisababisha kushambuliwa na baadhi ya marapa wenzake wakidai 'amechemsha'.

Ronaldo amfunika Messi kwa utajiri duniani

Ronaldo
Messi
LONDON, England
MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano  Ronaldo  ndiye mwanasoka tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa kiasi cha Pauni Mil. 152 ikiwa ni Pauni 7 zaidi ya mpinzani wake Lionel Messi.
Baada ya kufanya vizuri mwaka 2014 na kushuhudia Ronaldo akiiwezesha Real Madrid kupata mafanikio katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kushinda tuzo ya Ballon d'Or, aliongeza tofauti ya nafasi ya utajiri wake na nyota huyo wa Barcelona na Argentina.
Kwa mujibu wa orodha ya matajiri iliyotolewa na Goal.com Alhamisi, Ronaldo na Messi ndio wanaotamba kwa utajiri zaidi kuliko wanasoka wengine kwa sasa katika soka la kulipwa.
Jumla ya utajiri wao, ambao unatokana na matangazo pamoja na mishahara na bonasi, ni zaidi ya ule alionao Neymar, anayeshika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa thamani ya pauni Milioni 97.9.
Zlatan Ibrahimovic wa Paris Saint-Germain na Sweden anautajiri wa Pauni Milioni 76.1, wakati Wayne Rooney wa Manchester United ndiye anayeongoza kwa utajiri kwa wachezaji Waingereza akishika nafasi ya tano kwa dola Milioni 74.6.
Kaka wa Brazil yeye kwa sasa anashikilia nafasi ya sita akiwa na pauni Milioni 69.6, akifuatia na Samuel Eto'o (pauni Milioni 63.1), Raul (pauni Milioni 61.6) na Ronaldinho (Milioni 60.2).
Kiungo wazamani wa England Frank Lampard, kwa sasa anaichezea Manchester City kabla yakwenda New York City katika Ligi Kuu ya Marekani, anakamilisha orodha ya 10 bora kwa kuwa nba utajiri wenye thamani ya pauni milioni 58.
Wachezaji wengine Waingereza waliopo katika 20 bora ni Rio Ferdinand (nafasi ya 12, pauni Milioni 52.2), Steven Gerrard (nafasi ya 14, pauni Milioni 46.4) na John Terry (nafasi ya 20, pauni Milioni 40.6).
Kuna wachezaji wengine wawili zaidi wa Man City katika orodha hiyo, pamoja na Yaya Toure katika nafasi ya 15 akiwa na utajiri wa pauni Milioni 44.9 na Sergio Aguero katika nafasi ya 19 na utajiri wa pauni Milioni 42.
Mwaka jana orodha ya matajiri wa Goal iliyotolewa ilibainisha kuwa Ronaldo alikuwa na utajiri wenye thamani ya pauni Milioni 122, huku Messi akimkimfuatia kwa nyuma kwa utajiri wa pauni Milioni 120.5.

Wachezaji wa Kano Pillars ya Nigeria wapigwa risasi


Kikosi cha Kano-Pillars ya Nigeria.
ABUJA, Nigeria
WACHEZAJI watano wa timu ya Kano Pillars wamejeruhiwa kwa risasi na watu wenye silaha katika shambulio lililofanywa na kundi la watu wakati wakisarifi kwenda Owerri kwa ajili ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Nigeria.
"Wachezaji watano waliojeruhiwa kutokana risasi hizo ni pamoja na Gambo, Ogbonaya, Eneji Otekpa, Murtala Adamu, na Moses Ekpai," klabu hiyo iliandika katika mtandao wa Twitter. 
"Watu hao wenye silaha pia walichukua simu za mkononi na vitu vingine vya thamani kutoka kwa wachezaji ".
Kutokana na tukio hilo la uvamizi, mchezo wa Jumamosi dhidi ya Heartland ameahirishwa kwa muda usiojulikana.
Timu ya Kano ilikuwa ikisafiri kwa basi ikiwa na watu 25, wakiwemo wachezaji 18, wakati tukio hilo likitokea saa 7:15 mchana kwa saa za hapa.
Wachezaji watano waliojeruhiwa walipata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Centre huko Lokoja.
Kano walikuwa wakijianda kutetea taji la Nigeria, ambapo walianza msimu kwa ushindi dhidi ya Al Malakia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika raundi ya awali wikiendi iliyopita.
Hatahivyo, bado haijajulikana kama ratiba ya mabingwa Kano dhidi ya Moghreb Athletic Tetouane Machi 13 itaendelea kama ilivyopangwa.

VUMBI LA LIGI KUU BARA WIKIENDI HII LIPO HIVI:

Yanga
Azam
Mtibwa Sugar
Ndanda
Simba
VUMBI la Ligi Kuu Tanzania Bara linatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mechi tatu kabla ya Jumapili jiji la Dar kusimama wakati wapinzani wa jadi nchini, Simba na Yanga kumaliza ubishi kwenye uwanja wa Taifa.
MICHARAZO imekuwekea ratiba ya ligi hiyo kwa siku ya kesho na Jumapili kama ifuattavyo na msimamo wa ligi ulivyo kwa sasa na wanaoongoza kwa ufungaji mabao.
Ratiba:
Kesho Jumamosi
Polisi Moro vs Ruvu Shooting
Coastal Union vs Kagera Sugar
JKT Ruvu vs Azam FCr

Jumapili
Mgambo JKT vs Ndanda FC
Mtibwa Suga vs Mbeya City
Simba vs Yanga

MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA:
                            P   W    D    L   F    A   GD Pts
01.  Yanga           15  09  04   02  21 08  13  31
02.  Azam            15  07  06  02  22  12  10  27
03.  Simba           16  05  08  03  20  12  08  23
04. Coastal Union16  05  07   04  12  10  02  22
05. Mtibwa Sugar 15  05  07  03  17  15  02  22
06. Kagera Sugar 16  05  06  05  12  13  -1   21
07. Stand Utd      17  05  06   06 16  18  -2   21
08. Ruvu Shooting17 05  06   06 12  14  -2   21
09. JKT Ruvu        16  05  05  06 14  15   -1  20
10. Polisi Moro      16  04  07  05 13  15   -2  19
11. Ndanda Fc      16  05  04  07 15  19   -4  19
12. Mbeya City     16  04  06  06  11  15   -4  18
13. Mgambo JKT  14  04  02  08  07  20  -13 14
14. Prisons          17  01  10   06  10  20  -10 13
Wafungaji:
8- Didier Kavumbagu(Azam)
7- Rashid Mandawa, Absalim Chiidebere (Kagera Sugar)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ame Ali (Mtibwa), Simon Msuva (Yanga)
5- Danny Mrwanda (Yanga), Kipre Tchetche (Azam),Emmanuel Okwi (Simba)
4- Rama Salim (Coastal), Ibrahim Hajibu (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Heri Mohammed,(Stand Utd), Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)
3- Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Frank Domayo (Azam), Malimi Busungu (Mgambo), Atupele Green (Kagera), Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa (Yanga)
2- Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma, Elias Maguli (Simba), Salum Kanoni, (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Jerry Tegete, Coutinho (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi), Peter Mapunda (Mbeya City) Lutimba Yayo (Coastal Union)

Dokii afichua kilichomkimbiza Yanga kwenda Azam

Dokii
MUIGIZAJI nyota aliye pia muimbaji wa muziki, Ummy Wenceslaus 'Dokii' ambaye alikuwa mmoja wa mashabiki wakubwa wa Yanga amefichua siri ya kutangaza kuitema timu hiyo na kujiunga kuishangilia Azam FC.
Akizungumza na MICHARAZO katika mahojiano maalum kwa njia ya simu, Dokii alisema ameamua kuitosa Yanga ambayo keshokutwa itashuka dimbani kuvaana na Simba kutokana na kuvutiwa na uwezo wa wachezaji pamoja na viongozi wa klabu hiyo ya Azam.
"Kilichonifanya kuitosa Yanga na kuhamia Azam ni ubora wa wachezaji na uongozi wa jumla," alisema.
Alipoulizwa ataendelea kuishabikia Azam hata kama imeng'oka michuano ya kimataifa alipoibukia kwa mara ya kwanza wakati timu hiyo ikiumana na El Merreikh na kushinda 2-0, Dokii alisema Azam milele kwake kwani ni moja ya timu yenye muono wa mbali wa kimaendeleo.
"Vyovyote iwavyo mimi na Azam, nitaishangilia na kuipa sapoti kokote ilipo hata kama hatuendelei michuano ya kimataifa," alisema Dokii.
Dokii aliyekuwa miongoni mwa wasanii wanaoizimikia Yanga alionekana 'bize' uwanja wa Azam akishangilia timu hiyo akijipamba 'ki-Azam' tofauti na alivyozoeleka na hata kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi alikuwa akiishangilia timu yake ya Yanga iliyotoka robo fainali.

Nyota wa Filamu anusurika kifo ajali ya ndege

http://img2.timeinc.net/people/i/2004/04/30anniversary/sexiestman/hford.jpg 
NYOTA wa filamu wa Hollywood, Harrison Ford, anapatiwa matibabu katika Hospitali moja mjini Los Angels baada ya ndege yake kuukuu kuanguka katika uwanja wa Gofu.
Mcheza filamu huyo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa akiendesha ndege hiyo mwenyewe.
Ndege hiyo ndogo ilinasa kwenye mti wakati ilipokuwa ikitua kwa dharura.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema Harrison Ford alikuwa amejeruhiwa, akionekana kuwa na damu iliyotapakaa usoni.
Matabibu wamesema Ford anaendelea vizuri na kuwa hali yake itatengemaa kabisa.
Muigizaji huyo aliyeanza kuigiza tangu mwaka 1966, amewahi kujeruhiwa wakati wa kuigiza filamu zake ikiwamo mgongo mwaka 1983 na baadaye kifundo cha mguu Juni mwaka jana akiitengeneza  picha iitwayo 'Star Wars: The Force Awakens'.
Ntyota huyo anasifika kwa uigizaji wake makini wa filamu zilizompa ujiko miongoni wa filamu hizo ni American Graffiti, Star Wars, Apocalypse Now, The Frisco Kid, The Empire Strikes Back, Raiders of the Lost Ark, Blade Runner, Return of the Jedi, Indiana Jones and the Temple of Doom na Witness.
Nyingine ni; The Mosquito Coast, Working Girl, Indiana Jones and the Last Crusade, Regarding Henry, Patriot Games, The Fugitive, Clear and Present Danger, Sabrina, Air Force One, Six Days Seven Nights, What Lies Beneath, K-19: The Widowmaker, Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull, Extraordinary Measures, Cowboys & Aliens, 42, Ender's Game na Paranoia.

SIKILIZA NGOMA MPYA YA SNURA ft NAY WAMITEGO- HAWASHI