STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 24, 2015

Mkwasa aanza mambo Stars amrudisha Barthez

http://1.bp.blogspot.com/-b9ZAk_HHaPY/VYqYeIf4p-I/AAAAAAAHjWU/425CC5N9fxw/s1600/Kocha%2BMkwasa%2B%2528kushoto%2529%2Bna%2Bmsaidizi%2Bwake%2BHemed%2BMorocco%2Bwakiongea%2Bna%2Bwaandishi%2Bwa%2Bhabari.jpgKOCHA Mkuu Mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameanza mambo yake baada ya kutangaza kikosi cha wachezaji 26 akimjumuisha kipa wa Yanga Ally Mustafa 'Barthez'.
Mkwasa alitangaza kikosi hicho kilichowajumuisha pia mshambuliaji wa JKT Ruvu Samuel Kamuntu, huku pia akitangaza jopo lake la Benchi la Ufundi atakalosimamia akisaidiana na Hemed Morocco.
Wachezaji walioitwa kwa ajili ya pambano la marudiano la kuwania kucheza fainali za Chan 2016 dhidi ya Uganda The Cranes ni; Makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).
Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).
Mawinga: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).
Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.
Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahmed Mgoyi.
Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars

Jackson Mayanja atua Coastal, Kabange amfuata Tanga

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABLOVYqUbQ6C2E2ZEoE&midoffset=2_0_0_1_3671977&partid=3&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Kocha Jackson Mayanja akiweka dole gumba katika mkataba wa kuifundisha Coastal msimu ujao anayemuangalia ni Katibu Mkuu, Kassim El Siagi
https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AKh2imIAABLOVYqUbQ6C2E2ZEoE&midoffset=2_0_0_1_3671977&partid=4&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000Na Tariq Kimwaga, Tanga
MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia wa Uganda kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu .
Utiliaji wa saini wa Kocha huyo ulifanyika (leo)jana mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi.
Akizungumza baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi kuu msimu ujao.
Amesema kuwa uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo.
Mayanja ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Vipers  FC ya Bunamwaya  na KCC ya Uganda amesema kutua kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake kwenye kuipa mafanikio.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi.
Amesistiza pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
Katika hatua nyingine aliyekuwa msaidizi wa Mayanja ndani ya Kagera Sugar, Mrage Kabange ameamua kumfuata bosi wake mjini Tanga kwa kusaini African Sports.
Kabange amechukuliwa na Wana Kimanumanu waliopanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kutemeshwa kazi kwa Wakata Miwa mara baada ya msimu wa 2014-2015 kumalizika Mei 9 mwaka huu.