STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 11, 2013

ALIYEPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI AKATWA MGUU

      
 Na  Antony Sollo  -  Kishapu.

HALI si shwari katika mgodi wa mwadui,wananchi wamezidi kuuawa na kujeruhiwa kwa risasi huku Serikali ikiwa haina majibu kuhusu kashfa zinazotokea katika  mgodi huo jambo ambalo hadio sasa wananchi wana mpango wa kuvamia mgodi huo kwa lengo la kuharibu mali za mgodi huo.
 
Kufuatia hali hiyo,wananchi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mgodi huo wanajipanga kufanya vurugu kubwa katika mgodi huo ili kulipiza kisasi kufuatia kushambuliwa kwa vijana watano ambao waliingia mgodini humo hivi karibuni kama ilivyoripotiwa na Tanzania daima na hatimaye kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao huku mmoja wa vijana hao bwana Geroge Joseph akikatwa mguu.
Hali hii ni mwendelezo wa taarifa nyingi za kuuawa na kujeruhiwa kwa raia  lakini hakuna ufuatiliaji wowote kutoka kwa viongozi wa Serikali hususani vyombo vya ulinzi na usalama kama jeshi la polisi jambo ambalo kwa siku chache zijazo kama hali hii haitarekebishwa watanzania tukashuhudia mapigano makubwa kati ya walinzi wa mgodi na wananchi.
Matukio haya yamegubikwa na usiri mkubwa huku Viongozi mbalimbali wakiendelea kutupiana mpira na kushindwa kueleza bayana juu ya ukweli wa matukio haya na kibaya zaidi majeruhi aliyepata ulemavu huo bwana George Joseph akiwatuhumu viongozi hao akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu kwa kushindwa kufika kwa muda muafaka kumuona na kumuombea ruhusa kwa uongozi wa mgodi ili aende kupata matibabu.
 
Hali hii inatokana na kwamba mgonjwa majeruhi huyo alikuwa akishikiliwa na uongozi wa mgodi huo kwa tuhuma za kuingia mgodini isivyo halali jambo lililosababisha kumchelewesha kwenda kupata matibabu hivyo kuharibika kwa mguu wake na hatimaye kukatwa.
Kijana huyo alilazwa katika hospitali ya mgodi wa mwadui tangu tarehe 9/01/2013 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari wa mgodi huo lakini kukiwa hakuna huduma zilizokuwa zikitolewa jambo lililosababisha aombe kupewa rufaa bila mafanikio ambapo na hatimaye ndugu walifanikiwa kumuondoa hospitalini hapo kwa kutumia nguvu na kumpeleka hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza ambako amelazwa hadi sasa.
Akilalamikia viongozi wa Serikali mgonjwa huyo Bwana George Joseph anasema”ndugu mwandishi,Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya alikuwa ni mtu wa kwanza kumjulisha juu ya tukio hili na aliahidi kufika hospitalini lakini hakufanya hivyo hadi sasa nimethirika na kuwa mlemavu kwa kukatwa mguu wangu.
Kuhusu kauli ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kuwa hana taarifa,inashangaza na inasikitisha sana kwani askari waliokuwa wamekuja hapa kwa ajili ya kufanya operesheni walitoka mkoani Shinyanga.
Askari waliofika  kunichukua maelezo nao pia walitoka ofisi ya upelelezi ya Mkoa wa Shinyanga hata operesheni hii huandaliwa na Mkoa,je haya madai kwamba hana na taarifa yana lengo gani kama si kuficha ukweli wa jambo hili? na anafanya hivyo kwa faida ya nani amehoji bwana George.
Wakiongea na Tanzania daima wananchi waliozungumzia tukio hili walisema ndugu mwandishi, kwa kweli kuna idadi kubwa sana ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika mgodi huu lakini hatuoni viongozi wetu wakifuatilia masuala haya sijui hawana uchungu na wananchi ambao ndiyo rasrimali ya taifa hili.
Kwa sasa tukio hili limetupa hofu kubwa na sasa tunaiomba Serikali ijiandae kuona machafuko makubwa kwa vile tumechoshwa na vitendo hivi katika maeneo yetu.
tuna mpango wa kwenda kuvamia mgodi na kuchoma ofisi mbalimbali pamoja na kufanya uharibifu mkubwaili kuibua na kuweka wazi manyanyaso tunayofanyiwa na mawekezaji wa mgodi wa Williamson mwadui maana kuna usiri mkubwa mno kuhusu matukio ya unyanyasaji wa wananchi wa Maganzo na vitongoji vyake. 
Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea Ofisi za SHILEMA zilizopo katika mji mdogo wa Maganzo, Katibu Msaidizi wa SHILEMA bwana Hamza Yusuph amesema watu wengi wamepoteza maisha na viungo vyao kwa sababu ya kuingia mgodini mwadui pasipo na uhalali wa kuingia mgodini humo,wote tunajua kuwa kuingia mgodini ni kosa la jinai,lakini pia  hatua za watendaji wa jeshi la Polisi  kujichukulia sheria mkononi zinatokana sheria na mamlaka ipi?
 Kwa nini watu hawa wasikamatwe na kufikishwa mbele ya sheria kuliko kufanya ukiukwaji huu wa sheria na kusababisha wimbi la vijana walemavu kuongezeka! Vitendo hivi havikubaliki kabisa alisema bwana Selemani mkaji wa kitongoji cha majimaji mji mdogo wa Maganzo.
Bwana Yusuph amewalalamikia pia viongozi wa kisiasa wanaotumia mwavuli wa kisiasa katika masuala yanayohusu maisha ya watu ili kujijengea umaarufu katika nyakati za uchaguzi huku akiwalaumu viongozi wa kamati ya mzunguko wa mwadui kwa kujali masilahi yao  binafsi na kusahau kwamba wao ni wawakilishi wa wananchi.
Akizungumzia fedha zinazotolewa mgodini hapo bwana Yusuph amesema haelewi kama fedha hizo zinatolewa kama zawadi  au ni wajibu wa kampuni katika kuihudumia jamii hususani huduma za msingi kama Elimu,Afya,Miundo mbinu,Maji,Umeme naBarabara kama ilivyo katika maeneo mengine.
Bwana Yusuph amelaumu pia Serikali kwa kushindwa kuweka wazi mikataba ya Makampuni ya uchimbaji wa madini nchini kwa kuwa wananchi hadi sasa hawaelewi mambo mbalimbali zikiwemo haki zao dhidi ya makampuni ya uwekezaji katika maeneo yao.
 
Tanzania daima ilibisha hodi katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Bwana Justine Sheka na kufanya mahojiano naye ambapo alianza kwa kusema,ndugu mwandishi,sisi kama viongozi wa Serikali Wilayani Kishapu tunashangazwa na uongozi wa mgodi wa Mwadui kwa kuendesha shughuli zake kwa ubabe na usiri katika mapato yanayotokana na mgodi huo.
 
Hadi sasa uingiaji ndani ya mgodi huo una urasimu mkubwa kiasi kwamba hata Mbunge wa Jimbo anapohitaji kuingia na kuangalia utendaji wa shughuli za mgodi huo zinavyofanyika ni shida,unaingia ukiwa chini ya ulinzi mkali na mara nyingine yapo madai kuwa ni lazima utoe taarifa mapema kwa uongozi wa mgodi.
 
Lakini pia amesikitishwa na jinsi Serikali ilivyofanya siri kuhusu uwakilishi wake katika kukagua uzalishaji wa madini na namna ya kupata taarifa mbalimbali ili kuweza kuona kama kweli mali inayopatikana ndiyo inayotolewa taarifa  kama ilivyo katika maeneo mengine yaliyo na migodi.
Inasemekana ni muda mrefu mgodi wa Mwadui umekuwa ukiendesha shughuli za uchimbaji wa madini Wilayani Kishapu bila kuwa na mwakilishi wa Serikali ambaye anafanya ukaguzi jambo linalohofiwa kuporwa kwa madini na kuisababishia Hasara Serikali.
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga bwana Evarist Mangala alipotafutwa kujibu malalamiko juu ya tuhuma zinazotolewa na mgonjwa aliyekatwa mguu bwana George Joseph alisisitiza kwamba bado hana taarifa lakini akashauri kwamba mgonjwa aandike barua ya malalamiko juu ya tukio hilo ili aweze kulifanyia kazi.
 
CHANZO:Francis Godwin

Hatma ya Milovan Simba leo

Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic


HATMA ya aliyekuwa kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, kulipwa fidia yake ya kusitisha mkataba wa kuifundisha timu hiyo huenda ikajulikana leo wakati atakapokutana na viongozi wa klabu hiyo kabla ya kurejea kwao baada ya kupata haki yake.
Hata hivyo, Milovan ambaye ameumizwa na sare ambazo Simba imeendelea kuzipata, alisema jana kwamba yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo endapo uongozi utamrejesha.
Milovan anaidai Simba dola za Marekani 24,000 (Sh. milioni 36), ambazo ni malimbikizo ya mishahara yake ya miezi mitatu.
Akizungumza jana, Milovan, alisema kwamba  hadi sasa anafahamu kuwa yeye bado ni kocha halali wa timu hiyo kwani mkataba wake unamalizika Julai Mosi mwaka huu.
Mserbia huyo alisema kwamba ndiyo maana, baada ya kuona viongozi wa klabu hiyo wakikaa kimya, aliamua kuja nchini kufuatilia haki yake na kwamba, hata hoteli anayoishi jijini Dar es Salaam gharama zake zitalipwa na Simba.
"Mimi najua bado ni kocha wa Simba kwa sababu mkataba wangu haujamalizika. Na kama watakuwa tayari kuzungumza na mimi, naweza kurejea kazini. Bila shaka mnajua uwezo wangu na nini nilikifanya katika ligi na mshindano ya kimataifa mwaka jana," alisema kocha huyo.
Aliongeza kwamba kabla ya kukutana leo na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alitarajiwa kukutana jana na katibu mkuu wa timu hiyo, Evodius Mtawala; ambaye ndiye huwasiliana naye mara kwa mara.
"Hata hivyo, naye aliahidi tutakutana leo (jana) asubuhi, lakini sijamuona na alisema kwamba anamsubiri Rage na Kaburu,"  aliongeza Milovan.
Akihojiwa juzi katika kipindi cha michezo cha Radio One, Rage alikiri kocha huyo kuidai Simba lakini akashangazwa na maamuzi yake (Milovan) kufuata malipo yake jijini Dar es Salaam wakati wao walimueleza kuwa watamtumia kwa njia salama za kibenki.
Milovan alitua jijini Jumatano wiki iliyopita na kulieleza gazeti hili kwamba amechukua maamuzi ya kufuata haki yake baada ya kuona ahadi alizopewa kwa njia ya simu hazitekelezwi na kwamba sasa, anafahamu kuwa klabu hiyo inazo fedha baada ya kumuuza kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliyekuwa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi.
 

CHANZO:NIPASHE