STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 11, 2013

AZAM YAIKAMATA YANGA, WAISHINDILIA MTIBWA 4-1




Kikosi cha Azam  ambacho jana kiliendelea kushinda mechi zake kwa asilimia 100

TIMU ya soka ya Azam jana ilifanikiwa kuikamata Yanga kileleni baada ya kuizabua Mtibwa Sugar kwa mabao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mshambuliaji wake wa kimataifa, Kipre Tchetche akirejea dimbani kwa kishindo akifua mabao mawili kati ya hayo.
Azam ilipata ushindi huo katika mechi pekee iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Manungu, Morogoro na kurejea rekodi kama hiyo waliyoipata mbele ya Mtibwa katika uwanja huo misimu miwili iliyopita.
Kipre Tchetche aliyekuwa majeruihi alirejea kwa kishindo katika kiosi cha Azam kwa kufunga mabao mawili, baada ya kushuhudiwa dakika 45 za kwanza zikiisha kwa sare ya baoa 1-1.
Bao la Azam la kwanza lilifungwa na Humphrey Aturdo kabla ya Vincent Barnabas wa Mtibwa kusawazisha na walipoanza kipindi cha pili, Mganda Brian Umony  alifunga bao la pili kabla ya Tchetche kutupia mengine mawili moja dakika za lala salama.
Kwa ushindi huo, Azam sasa wameikamta Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ya Bara baada ya kufikisha pointi 33, lakini wakiendelea kukamata nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli. Yanga imefunga mabao 29 na kufungwa 12 wakati Azam wamefunga goli 27 na kufungwa 14.
Wenyewe Yanga watashuika dimbani siku ya Jumatano kuvaana na African Lyon katika pambano litakalochezwa uwanja wa Taifa, jijini Dar ambapo tayari wachezaji wa Yanga jana usiku waliingia kambini tayari kwa mchezo huo wakipania kupata ushindi.
Kwa mabao mawili ya jana Kipre Tchetche amefikisha jumla ya mabao 10 na kumzidi Mrundi wa Yanga, Didier Kavumbangu aliyesaliwa na mabao yake nane tangu duru lililopita.
Ligi hiyo itaendelea Jumatano kwa michezo mingine kadhaa mbali na huo wa Yanga na Lyon ambayo imeendelea kugawa pointi kwa wapinzani wao tangu duru la pili lianze.

No comments:

Post a Comment