STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 28, 2013

NI FAINALI YA WANA MADRID WATUPU KOMBE LA MFALME HISPANIA

Ramidel Falcao akiwajibika uwanjani kuipeleka Atletico Madrid fainali ya Kombe la Mfalme kuvaana na mahasimu wao Real Madrid
MAHASIMU wa jiji la Madrid, nchini Hispania, Real Madrid na Atletico Madrid zitatarajiwa kuumana kwenye pambano la fainali za michuano ya Kombe la Mfalme litakalochezwa Mei 18 mwaka huu.
Atletico Madrid iliifuata Real Madrid kwenye fainali baada ya usiku wa kuamkia leo kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sevilla katika mechi ya marudiano ya hatua ya nusu fainali iliyochezwa ugenini.
Mabao ya haraka ya kipindi cha kwanza kutoka kwa nyota wake, Diego Costa na Falcao yalitosha kuivusha Atletico hadi fainali kuwakabili Real iliyoitoa nishai Barcelona juzi usiku kwa kuisasambua mabao 3-1.
WEnyeji walipata bao la kwanza dakika ya 39 lililofungwa na Jesus Navas na kufanya matokeo ya mchezo huo wa jana kusomeka 2-1 wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili wenyeji kilianza kwa kasi na wenyeji walijikuta wakipoteza wachezaji wake wawili kabla ya kusawazisha bao dakika za lala salama na kuepuka aibu ya kulala nyumbani.
Sevilla ilimpoteza Medel dakika ya 76 kabla ya kufuatiwa na Kondogbia aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika moja baada ya kusaidia kupatikana kwa bao la kusawazishwa lililofungwa na Rakitic dakika za nyongeza za pambano hilo.
Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu pambano hilo la fainali, licha ya Real Madrid inayonolewa na kocha Jose Madrid ikipewa nafasi kubwa ya kujifariji kwa kutwaa taji hilo baada ya kuonekana wazi ni vigumu kutetea taji la Ligi Kuu ya nchi hiyo.

MIMBA YATAJWA CHANZO CHA MAUAJI YA MPENZI WA PISTORIUS

Pistorius akiwa katika moja ya mashindano ya mbio za walemavu alizoshiriki.
Johannesburg, Afrika Kusini
MWANARIADHA wa mbio za walemavu, Oscar Pistorius anayekabiliwa na shitaka la kumuua mpenzi wake kwa risasi, amedaiwa kuwa huenda alimuua mwanamitindo huyo wa zamani akiwa mjamzito.
Kama taarifa hizi zitathibitishwa, itakuwa mfululizo wa madai unaomuweka nyota huyo kwenye hatari ya kufungwa kifungo cha maisha – kwa kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp katika nyumba yake katika usiku wa kuamkia Siku ya Wapendanao.
Katika utetezi wake wa awali, Pistorius alidai kumuua Steenkamp kwa bahati mbaya, baada ya kuhisi amevamiwa na jambazi aliyejificha bafuni na kwamba kwa kuwa hakuwa na miguu yake ya bandia, hakuona njia ya kujihami zaidi ya kufyatua risasi mfululizo.
Ni utetezi uliopingwa na waendesha mashtaka wa kesi hiyo – waliodai kuwa tukio limefanyika kwa makusudi baada ya mabishano.
Taarifa zilizochapishwa juzi Jumatatu na gazeti la National Enquirer la hapa zimedai kuwa, huenda mabishano baina ya wawili hao yalitokana na habari kuwa Pistorius alikuwa akikaribia kuitwa baba wa kichanga cha mrembo huyo.
Chanzo cha karibu na uchunguzi kililiambia gazeti la udaku kuwa: 'Polisi inaamini kuwa siri ya ujauzito aliyopewa ilimfanya Pistorius acharuke na kuingia katika mabishano yaliyosababisha kifo cha Reeva – kwa kupigwa risasi nne kichwani, kifuani, mkononi na nyongani.'
Chanzo hicho kiliongeza kuwa: 'Baadaye usiku, majirani walisikia mabishano yaliyofuatiwa na ufyatuaji risasi katika nyumba yao.
'Polisi waliitwa kwa uchunguzi, lakini walijiridhisha tu kuwa ulikuwa ubishani wa kimapenzi, hivyo hawakuwa na uchunguzi wa maana waliotarajiwa wangeulizwa kuhusiana na sakata hilo.'
Likiambatanisha na picha iliyopigwa siku chache kabla ya kifo cha Reeva, gazeti hilo limeripoti wasiwasi huo, sambamba na habari kuhusu ibada maalum ya kumuombea marehemu aliyoandaa Pistorius nyumbani kwa mjomba wake anakoishi kwa hivi sasa.

Toto Afrika, JKT Ruvu zikishuka dimbani, Ligi yazidi kunoga