STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 28, 2013

Toto Afrika, JKT Ruvu zikishuka dimbani, Ligi yazidi kunoga

Kikosi cha JKT Ruvu

WAKATI vijana wa Toto African leo wakijaribu bahati yao mbele ya wenyeji wa JKT Ruvu katika mechi ya kiporo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, matokeo ya mechi za jana za ligi hiyo zimevuruga msimamo kwa baadhi ya timu nyingine zikinufaika na nyingine zikiporomoka katika nafasi walizokuwa wakizishikilia.
Kipigo cha bao 1-0 ilichopewa Kagera Sugar kimeishusha timu hiyo kutokana nafasi ya tano iliyokuwa ikishikilia hadi nafasi ya sita ikiwapisha ndugu zao Mtibwa Sugar walioambulia suluhu nyumbani kwao Manungu dhidi ya Prisons-Mbeya.
Timu hizo mbili zote zinalingana pointi 28, lakini Mtibwa imeiengua Kagera kwa vile ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, ambapo hazina yake inaonyesha imefunga mabao 21 na kiufungwa 18 wakati ndugu zao wamefunga mabao 19 na kufungwa 17.
Pia ushindi wa Polisi Moro umeifanya timu hiyo kuchupa toka mkiani hadi kwenye nafasi ya 12 ikifikisha pointi 15 na kuirejesha African Lyon kuburuza mkia na pointi zake 13, wakifuatiwa na Toto African ambao jioni ya leo watacheza wakiwa na pointi 15 na iwapo iutashinda itachupa hadi nafasi ya 11 inayoshikiliwa na  wapinzani wa JKT Ruvu.
Kwa mujibu wa ratiba ni kwamba ligi hiyo itaendelea tena Jumatano ijayo kwa mechi tatu, 'vibonde' African Lyon kuikaribisha Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Chamazi, Mgambo JKT kuialika Mtibwa Sugga kwenye dimba la Mkwakwani Tanga na JKT Oljoro wakaikaribisha Prisons ya Mbeya.
Siku inayofuata kutakuwa na pambano moja tu kati ya JKT Ruvu dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Chamazi na mwishoni mwa wiki kushuhudiwa mechi tatu zitakazozihusisha timu zilizopo nafasi nne za juu.
Jumamosi Machi 9, vinara Yanga itawakaribisha ndugu zao Toto African kwenye uwanja wa Taifa, wakati Azam itakayokuwa imerejea toka Sudan Kusini kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho itaialika Polisi Moro kabla ya siku inayoifuata yaani Jumapili 'ndugu' wengine, Simba na Coastal Union kuumana Taifa.

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA
                        P W  D  L  GF GA GD Pts
1. Yanga 18 13 3 2 35   12 23 42

2. Azam 18  11 3 4  31   15  16   36

3. Simba SC 18 8 7 3  26   15   11 31

4. Coastal Union 19  8  4  21 16 5 31

5.
Mtibwa Sugar 19  7  5  21  18    3    28
6. Kagera Sugar 19 7  7 5  19  17      28
7. Ruvu Shooting 17  7 5 5  20 17     3 25
8. Mgambo JKT 19 7 3 9 14  18 -4   24

9. JKT Oljoro 18  5   6  7  19  22   -3 21

10.Tanzania 19  4   8 7  11  16   -5    20

11.JKT Ruvu  17  4 4 9 14  27 -13 16

12. Polisi Moro 18  3 6   9   9   18  -9   15

13.Toto African 18 2 8  8   14 25 -11  14
14.African Lyon 19 3 4 12 13  31 -18 13










































































































































































No comments:

Post a Comment