STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 22, 2014

Linex, Prof Jay kuwasindikiza Kalapina, Q.Chilla Maisha Club

Kalapina
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Linex, Mapacha na Q Chillah ni baadhi ya watakaoshiriki kumsindikiza mkali wa Hip Hop nchini, Karama Masoud 'Kalapina' katika onyesho lake maalum.
Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika April 27 Maisha Club, kwa lengo la kuwaenzi wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wa kuisimamisha miondoko ya Hip Hop nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Kalapina alisema katika onyesho hilo ataimba 'live' wimbo wake mpya wa 'Hip Hop is Alive' alioimba na Q Chillah na kusindikizwa na mastaa kibao wa hip hop nchini.
Kalapina aliwataja baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Prof Jay, Kimbunga, Linex, Mapacha, Q Chilla mwenyewe na Masharikanz.
"Yaani itakuwa burudani ya kipekee kwa mashabiki wa Hip Hop na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla kwa namna onyesho hilo maalum litakavyokuwa wakishuhudia Hip Hop is Alive ukiimbwa live," alisema.
Kalapina alisema katika onyesho hilo watapiga pia nyimbo zake zote pamoja na Kikosi cha Mizinga ambazo zilisaidia kuamsha harakati za kijamii kupitia miondoko hiyo ya hip hop nchini.

Nani kuwa Kocha Bora 2013-2014?

http://4.bp.blogspot.com/-RQj_viCJNwE/UrrHiJX4eWI/AAAAAAAAT58/waW_ta_dKac/s1600/mwambusi+coach.jpg
Juma Mwambusi
http://api.ning.com/files/VMB94olbxS1KUXphY0U47D4laBLxC*CFhUlgLRS9F0nyaxUKrUNPfsr0M0JTm2GFIFYUVc9GC7kbzapFvqrS-DcuQ0M-I6aJ/PLUIJMKITAMBI.jpg
Hans Van der Pluijm

http://1.bp.blogspot.com/-68LwLDJvsYQ/Upuh2MtvcLI/AAAAAAAAoLk/FRvtqsT8Gkw/s1600/1482940_668051136568579_1302657830_n.jpg
Joseph Omog
PAZIA la  Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 lilifungwa mwishoni mwa wiki huku Azam ikiwa imeshatangaza ubingwa tangu wiki iliyopita kabla ya ligi hiyo haijafikia tamati.
Azam imetwaa taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya kufikisha pointi 62 na kuingia kwenye rekodi ya kuwa klabu ya tisa nchini kunyakua  ubingwa nchini.
Baada ya ligi hiyo kumalizika, mashabiki wa soka wana hamu kubwa ya kutaka kujua nani atakayeibuka kuwa Mfungaji Bora, Mchezaji Bora na Kipa Bora wa ligi ya msimu huu.
Makocha Juma Mwambusi wa Mbeya City, Hans van der Pluijm wa Yanga na kocha wa Azam Joseph Omog walioziongoza timu zao kushika nafasi tatu za juu wanapewa nafasi kubwa kutwaa tuzo hiyo.
Katika msimu uliopita, kocha Abdallah Kibadeni aliyekuwa akiinoa Kagera Sugar aliibuka kidedea na kunyakua tuzo hiyo baada ya kuiwezesha Kagera Sugar kushika nafasi ya nne, ingawa msimu huu nafasi ya kuitetea inaonekana kuwa ndogo kwa hali ilivyo.
Kocha huyo aliyekuwa akiifundisha Simba, alitimuliwa na kuhamia Ashanti United ambayo ameshindwa kuikoa isirejee Ligi Daraja la Kwanza.
Mwambusi anapewa nafasi zaidi kwa kuipandisha daraja Mbeya City na kuifanya iwe tishio katika ligi licha ya ugeni wake na kumaliza katika nafasi ya tatu ikizidiwa na klabu za Azam na Yanga tu.
Omog aliyechukua nafasi ya Stewart Hall aliyetimuliwa na Azam baada ya kumalizika kwa duru la kwanza naye anapigiwa chapuo kama ilivyo kwa Pluijm wa Yanga aliyeinoa pia duru la pili tu.
Kabla ya hapo Yanga ilikuwa chini ya Mholanzi mwingine, Ernie Brandts aliyetimuliwa baada ya Yanga kufungwa kwenye mechi ya 'bonanza' ya Nani Mtaji Jembe.
Kwa upande wa Mchezaji Bora msimu uliopita alikuwa Kelvin Yondani na kipa akiwa Burhan aliyekuwa Prisons, je msimu huu tuzo hizo zitaenda wapi miongoni mwa wachezaji waliong'ara katika ligi hiyo?
Bila shaka mashabiki wana hamu kubwa ya kuona wachezaji wanaoamini walifanya vyema msimu huu wakinyakua tuzo hizo kama ilivyo kwa makocha na wachezaji chipukizi waliong'ara msimu huu.
Kwenye tuzo ya Mfungaji Bora nafasi ilikuwa ikionekana wazi ikielekea mikononi mwa Mrundi, Amissi Tambwe wa Simba aliyemaliza na mabao 19.
Je, Joseph Kimwaga atatetea tuzo yake ya Mchezaji Bora chipukizi katika msimu huu?Tusubiri tuone baada ya Bodi ya Ligi Tanzania pamoja na wadhamini wake kampuni ya Vodacom watakapoweka bayana orodha katika tuzo hizo kwa msimu wa 2013-2014.

Wanaoibeza Azam wana wivu-Himid Mao

Himid Mao
BAADHI ya nyota wa klabu ya Azam wamesema wanaowaponda kwa kufanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania ni wasiokubali kushindwa na wenye dhana kuwa nje ya Simba na Yanga hakuna bingwa.
Azam iliweka rekodi ya kunyakua taji hilo baada ya misimu miwili mfululizo ikiishia kuambulia nafasi ya pili nyuma ya Simba na Yanga na kuwa klabu ya tisa kunyakua ubingwa huo tangu mwaka 1965.
Hata hivyo kabla na hata baada ya kunyakua taji hilo kumekuwa na kauli za kejeli dhidi ya mafanikio ya klabu hiyo, kitu kilichowakera baadhi ya nyota wa Azam waliodai wanaoponda wanawaonea gere.
Nahodha msaidizi wa klabu hiyo, Himid Mao, alisema mashabiki wa soka walipaswa kuipongeza Azam kwa kuonyesha ushindani wa kweli na kuweza kuzisimamisha Simba na Yanga na kuleta mapinduzi.
Mao, alisema Azam imechangia kuzika 'ligi ya klabu mbili' na kuonyesha kuwa kumbe hata timu nyingine zinaweza kuwa mabingwa kama zikijipanga, hivyo kupondwa kwao ni kuwakatisha tamaa.
"Nadhani wanaofanya hivyo wanasumbuliwa na wivu wa mafanikio yetu na pia kushindwa kuamini kuwa nje ya Simba na Yanga bingwa anaweza kupatikana tena kwa kuweka rekodi kama wao," alisema.
Alisema anaamini kuwepo kwa Mbeya City na kuongezeka kwa timu kama Ndanda Fc na Stand United kunaweza kuongeza chachu iliyoanzishwa na Azam ili kuifanya ligi iwe na utamu wa kusisimua.
"Ligi ya timu chache haivutii, ndiyo maana leo ligi ya England inavutia na kufuatiliwa kwa sababu haitabiriki kwa ushindani uliopo bila hadhi ya klabu, tumeonyesha uwezo tuungwe mkono tusikatishwe tamaa," alisema Mao mmoja wa 'nguzo' ya Azam tangu ipande daraja.

Abou Diaby arejesha tumaini Arsenal

http://www.images99.com/i99/02/36120/36120.jpg
Abou Diaby
BAADA ya kuwa nje ya dimba kwa karibu mwaka mzima, hatimaye Abou Diaby anatarajiwa kuanza kuonekana kwenye kikosi cha Arsenal.
Mchezaji huyo kutoka Ufaransa alikuwa nje ya dimba baada ya kuumia goti Machi mwaka 2013 wakati wa mechi baina yao na Swansea City.
Kwa mujibu wa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, Diaby 27, amerejea na kungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya timu hiyo na huenda akamtumia katika mechi zilizosalia za ligi hiyo.
"Amerejea jumla kwenye mazoezi na sasa ataonekana uwanjani kuitumia timu," Wenger alinukuliwa na mtandao wa klabu hiyo na kuonyesha furaha yake.

Babi azidi kutisha Malaysia atupia mbili kuiokoa UiTM

Babi (kati mbele) ameziodi kudhihirisha ukali wake na kwamba UiTM hawakukosea kumpa unahodha
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Malaysia, Abdi Kassim 'Babi' mwishoni mwa wili aliibeba na kuinusuru timu yake ya UiTM kupata kipigo kwa kutoka nyuma ya mabao 2-0 na kumaliza kwa sare ya 2-2 na Johor katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Malaysia.
Babi alifunga mabao hayo katika dakika ya 70 na 89 na kuifanya timu yake kuambulia pointi moja ugenini iliyochezwa kwenye uwanja wa Pasir Gugand Corporation mjini Pasir Gudang.
Sare hiyo imekuja siku chache baada ya kuisaidia UiTM kupata ushindi wake wa kwanza wa 2-1 dhidi ya Kuala Lumpur SPA baada ya vipigo mfululizo katika ligi ya nchi hiyo.
Mabao hayo mawili yamemfanya Babi aliyeingia mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo kufikisha jumla ya mabao matano tangu ajiunge na UiTM.
Babi ( wa pili kulia) akiwa na wachezaji wenzake wa UiTMya Malaysia

Mchezaji gabon afa kwa kikanyagwa kichwani

Sylvain Azougoui enzi za uhai wake
GOLIKIPA wa timu ya AC Bongoville, Sylvain Azougoui amefariki dunia baada ya kukanyagwa kichwani wakati wa mchezo wa ligi huko nchini Gabon. 
Golikipa huyo alifariki wakati akikimbizwa hospitali baada ya tukio hilo wakati wa mechi dhidi ya timu ya Centre Mberi Sportif. 
Azougoui mwenye umri wa miaka 30 raia wa Togo, alikuwa amezuia shuti lililokwenda langoni mwake lakini mshambuliaji aliyepiga shuti hilo alipoteza mwelekeo katika nyasi zilizokuwa zimelowa na kumkanyaga golikipa huyo kichwani. 
Klabu hiyo ilithibitisha habari za kifo cha golikipa huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook na kueleza masikitiko yake kwa pengo aliloacha klabuni na kwa familia yake.

Kuziona Stars, Burundi buku 5 tu

 http://2.bp.blogspot.com/-NxQE6lj1C7U/UxdHDZ444jI/AAAAAAAASHM/UOWGNKyIcKU/s1600/FKB_1765.JPG
KIINGILIO cha chini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa wa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Kenya.
Burundi inatarajia kuwasili nchini keshokutwa (Aprili 22 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayotajiwa kuwa ya kusisimua. Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10 jioni.
Wachezaji wa Taifa Stars waliopo kambini ni Deogratias Munishi, Mwadini Ali, Aidan Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan Mwasapili, Kelvin Yondani, Said Morad, Amri Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas Mkude, Athanas Mdamu, Haruna Chanongo, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngassa, Ramadhan Singano na Simon Msuva.
Wengine ni Benedicto Mlekwa, Emma Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba, Edward Mayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf Mlipili, Said Ally, Abubakar Mohamed, Hashim Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito, Mohammed Saidi, Ayoub Lipati, Abdurahman Ally na Paul Bundara.

Msiba! Mahabusu wa4 askari Magereza wafa ajalini

MAHABUSU wanne na Askari Magereza mmoja wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyotokea eneo la Mkenge, Mkuranga, Pwani.
Taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa dereva wa gari lililokuwa limewabeba marehemu hao yupo hospitalini katika hali mbaya.
Taarifa zinasema kuwa marehemu hao na dereva walikuwa wakitokea Mkuranga kuja jijini Dar es Salaam na kukutwa na ajali hiyo inayopelezwa ni mbaya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio ni kwamba pick up ya Magereza ilipasuka tairi la kushoto na dereva wake kupoteza muelekeo na kugongana na lori lililokuwa likitokea Kimazichana na gari hilo lililokuwa na mahabusu hao na askari aliyekuwa akiwasindikiza lilipinduka na kusababisha vifo vyao.
Endelea kusoma MICHARAZO MITUPU kupata taarifa kamili, ingawa inaelezwa kuwa majeruhi wamehamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
 

Newz Alert! Moyes hatimaye atimuliwa Man Utd, Giggs apewa shavu

Giggs (kushoto) akiwa na Moyes

Moyes kando ya Giggs, wawili hao wamebadilishana nafasi ya ukocha ndani ya klabu ya Manchester City
HATIMAYE klabu ya Manchester United imetangaza kumfuta kazi kocha wake, David Moyes na mkongwe Ryan Giggs amepewa 'shavu' la kuinoa timu hiyo kuelekea mwisho wa msimu.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa klabu hiyo, Moyes amefutwa kazi baada ya miezi 10 na tayari ameshapewa barua ya kufutwa kazi ikiwa ni baada ya timu yake kupoteza mechi 11.
Nafasi ya kocha huyo imechukuliwa na mchezaji mkongwe wa klabu hiyo aliyedumu nayo kwa muda mrefu, Ryan Giggs wakati mipango ya kocha mpya ikifanywa, japo Louis van Gaal anatajwa kuja kubeba kibarua hicho baadaye.

Manchester City yaua 3-1 yaisogelea Chelsea

KLABU ya Manchester City imerejesha tumaini la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuilaza mabao 3-1 West Bromwich Albion usiku wa kuamkia leo kwenye pambano lililochezwa kwenye Uwanja wa Etihad.
City ambayo katika pambano lao la mwisho iliponea chupuchupu mbele ya 'vibonde; Sunderland kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2, ilip[ata ushindi huo uliowafanya wafikishe jumla ya pointi 74 baada ya kucheza mechi 34 na inaendelea kushikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo nyuma ya Chelsea pointi 75 za mechi 35 na Liverpool pointi 80 za mechi 35.
Ushindi wa City ulianikizwa na mabao Zabaleta aliyefunga dakika ya tatu, Sergio 'kun' Aguero katika dakika ya 10 kabla ya  wageni kupata bao lao la kufutia machozi lililofungwa na Dorrans dakika ya 16 na Demichelis alimalizia kazi kwa kufunga bao la tatu wa wenyeji dakika ya 36.

Wanariadha Alphonce, Jackline wang'ara mbio za Ngorongoro

Wanariadha wa Mbio za Ngorongoro Marathon, Kilometa 21 (Half Marathon) wakianza mbio katika geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu.
Mchuano wa wanariadha ukiendelea kwa kasi.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akitaka kuchomoza ili aweze kushinda.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Ngorongoro Marathon kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akiwatoka wenzake.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Ngorongoro Marathon kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu akimaliza mbio.
Umati wa Wakazi wa Mji wa Karatu wakifuatilia michuano hiyo.
Hapa ndipo zilipoanzia mbio za makampuni... ambapo makampuni yalikimbia kilometa 5.
 Mshindi wa kwanza wa mbio za makampuni akifurahia mara baada ya kumaliza.
Mkururenzi Mtendaji wa Kampuni ya Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia (nyuma) hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo.
Washiriki wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 5 za Makapuni wakimenyana vikali.
Timu ya Kampuni ya Frontline Porter Novelli ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika sura ya furaha mara baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 5 katika Mbio hizo.

Van Gaal kumrithi Moyes Manchester United?

WAKATI kukiwa na kila dalili za kocha david Moyes kutupiwa virago Old Trafford kutokana na kufanya vibaya kwa timu yake ya Manchester United, Louis Van Gaal ndiye anayatarajiwa kupewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya kocha huyo aliyemrithi, Sir Alex Ferguson aliyestaafu kwa heshima kubwa klabuni hapo.
Kwa mujibu wa taaraif za duru za soka nchini England, zinadokeza kuwa Van Gaal anayeelezwa kuwa na urafiki wa karibu zaidi na mshambuliaji Robin van Persie aliyewahi kumfundisha kwenye timu ya taifa ya Uholanzi ndiye chaguo la kwanza la mrithi wa Moyes aliyeiongoza timu hiyo watetezi wa Ligi Kuu ya England kupoteza mechi 11 kitu ambacho kimefanya bodi na mashabiki wa klabu ya Manchester United kufikia ukomo wa uvumilivu wao kwa kocha huyo wa zamani wa Everton.
Kipigo cha mabao 2-0 kwenye uwanja wa ugenini dhidi ya klabu yake ya zamani, mwishoni mwa wili ilichangia Moyes kufunguliwa mlango wa kutakiwa kutoka wakiamini ukubwa wa klabu hiyto umemshinda, ingawa taarifa rasmi ya kutimuliwa bado haijatolewa mpaka sasa.
Huu ni wasifu mdogo wa Van Gaal kama kocha:
Klabu alizofundisha
Ajax, Barcelona, AZ Alkmaar, Bayern Munich
Timu ya taifa aliyofundisha
Uholanzi
Makombe akiwa na klabu
Ubingwa wa ligi 7
Ligi ya Mabingwa 1
Kombe la UEFA 1
Makombe ya kawaida 7
makombe mengine Ulaya 3

ATLETICO MADRID, CHELSEA KAMA VITA ULAYA LEO

KINYANG'ANYIRO cha Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kinaanza leo kwa pambano la kukata na shoka baina ya vinara wa Ligi ya Hispania, Atletico Madrid dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho \,Chelsea ya England.
Atletico imetamba imejijiandaa  kumshangaza Mourinho leo katika mechi  hiyo baada ya kumzuia kumaliza msimu wake wa mwisho nchini Hispania bila kombe.
Mourinho ataiongoza Chelsea leo kucheza hatua ya nne bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Calderon dhidi ya Atletico inayoongoza msimamo wa La Liga ikiwa ni mara ya kwanza timu hizo kukutana nusu fainali kwa kipindi cha miaka 40.
Mourinho alitolewa na Borussia Dortmund katika raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2012-13, wakati na Real Madrid huku msimu huo Barcelona ikiutwaa ubingwa wa La Liga na kisha kulikosa Kombe la Mfalme (King’s Cup) katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Bernabeu dhidi ya Atletico.
Bao la kichwa la Miranda katika muda wa nyongeza lilikifanya kikosi cha Diego Simeone kuibuka na ushindi wa 2-1 katika mechi hiyo ya fainali ambayo Mourinho na mshambuliaji Cristiano Ronaldo walitolewa nje kwa kadi.
"Uhitaji kuwa mtabibu kueleza kuwa matokeo ya fainali hayakuwa ya haki, kuwa Atletico si washindi tu," Mourinho aliuambia mkutano wa wanahabari baada ya mechi hiyo.
Tukirudi Chelsea, kwa sasa Mourinho anahitaji kulipa kisasi huku akitaka kuweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu tatu tofauti baada ya kutwaa ‘ndoo’ hiyo wakati akiinoa Porto 2004 na Inter Milan 2010.
Yeye na kikosi chake cha Chelsea atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Atletico ambayo inaongoza msimamo wa La Liga ambayo inakaribia kuutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu 1996, ikiwa na Simeone ambaye ameshatwa La Liga na Kombe la Mfalme mara mbili.
Atletico itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata mwishoni mwa wiki kwenye La Liga dhidi Elche, wakati Chelsea yenyewe ikiwa na huzuni ya kulala 2-1 nyumbani dhidi ya Sunderland, hicho kikiwa ni kipigo cha kwanza cha Mourinho Stamford Bridge katika mechi 78.
Mourinho alikataa kujibu maswali baada ya mechi na kuonekana akimlaumu zaidi mwamuzi kuliko wachezaji wake, akidai ameiua Chelsea, jambo ambalo limepunguza kasi zao za mbio ubingwa.
"Wamefanya kila kitu walichotaka," aliuambia mkutano wa wanahabari.
"Walipigana, kucheza kuanzia mwanzo hadi mwisho wa pili na walistahili hilo (alisifu)," aliongeza kocha huyo mwenye umri wa miaka 51.
"Mara nyingine tunawatukuza wakati tunaposhinda lakini nadhani ni sahihi kuwapongeza wachezaji wangu baada ya kipigo."
Kulikuwapo na hofu kama kipa wa Atletico, Thibaut Courtois, ambaye anaichezea klabu hiyo kwa mkopo akitokea Chelsea, angecheza mechi ya leo dhidi ya timu yake, lakini Simeone alisema baada ya mechi dhidi ya Elche kwamba nyota huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji atajumuishwa.
Mbali na sakata hilo la mkopo, klabu hizo mpili zilikubaliana kuwapo kwa penalti ya kiasi cha fedha endapo Atletico itamchezesha Courtois dhidi ya Chelsea lakini Shirikisho la Soka barani Ulaya (Uefa) limesema makubaliano hayo ni kinyume na sheria za mashindano hayo.
"Hakuna yeyote aliyezungumza lolote na mimi, hivyo kama ilivyo atacheza," alisema Simeone.
Kipigo kwenye Kombe la Mfalme ndicho pekee kilichomkuta Mourinho katika rekodi yake dhidi ya Atletico, kwani mara zingine nane walizokutana alishinda.
Hata hivyo, Atletico ni timu pekee katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo haijafungika na imeshinda mechin zake zote tano ilizocheza nyumbani ikiwa ni pamoja na dhidi ya mabingwa wa zamani AC Milan na Barca.
Mshindi wa jumla wa mechi hiyo na pindi zitakaporudiana, atacheza fainali dhidi ya Real Madrid ama Bayern Munich katika mchezo wa fainali utakaopigwa Lisbon, Ureno.
Hatua nyingine ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itaendelea kesho kati ya Bayern Munich na Real Madrid ambayo imepata ahueni baada ya Cristiano Ronaldo kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua na hivyo kuanza kujifua kwa ajili ya mechi hiyo.