WAKATI kukiwa na kila dalili za kocha david Moyes kutupiwa virago Old Trafford kutokana na kufanya vibaya kwa timu yake ya Manchester United, Louis Van Gaal ndiye anayatarajiwa kupewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya kocha huyo aliyemrithi, Sir Alex Ferguson aliyestaafu kwa heshima kubwa klabuni hapo.
Kwa mujibu wa taaraif za duru za soka nchini England, zinadokeza kuwa Van Gaal anayeelezwa kuwa na urafiki wa karibu zaidi na mshambuliaji Robin van Persie aliyewahi kumfundisha kwenye timu ya taifa ya Uholanzi ndiye chaguo la kwanza la mrithi wa Moyes aliyeiongoza timu hiyo watetezi wa Ligi Kuu ya England kupoteza mechi 11 kitu ambacho kimefanya bodi na mashabiki wa klabu ya Manchester United kufikia ukomo wa uvumilivu wao kwa kocha huyo wa zamani wa Everton.
Kipigo cha mabao 2-0 kwenye uwanja wa ugenini dhidi ya klabu yake ya zamani, mwishoni mwa wili ilichangia Moyes kufunguliwa mlango wa kutakiwa kutoka wakiamini ukubwa wa klabu hiyto umemshinda, ingawa taarifa rasmi ya kutimuliwa bado haijatolewa mpaka sasa.
Huu ni wasifu mdogo wa Van Gaal kama kocha:
Klabu alizofundisha
Ajax, Barcelona, AZ Alkmaar, Bayern Munich
Timu ya taifa aliyofundisha
Uholanzi
Makombe akiwa na klabu
Ubingwa wa ligi 7
Ligi ya Mabingwa 1
Kombe la UEFA 1
Makombe ya kawaida 7
makombe mengine Ulaya 3
No comments:
Post a Comment